Kisusi Mohammed
JF-Expert Member
- Aug 10, 2009
- 563
- 470
- Thread starter
- #141
Unahitaji nikuthibitishie vipi?Ni kweli Kaka?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unahitaji nikuthibitishie vipi?Ni kweli Kaka?
Ni kweli kabisa. Kuna siku nilikwenda sheli nikanunua diseli ya sh. 50,000. Mwanadada mhudumu akaniambia nakuwekea kwanza ya sh. 10,000. kisha nitakuwekea ya 40,000. Nikateremka kwenye gari kuangalia. Mwisho nilikuwa na risiti mbili moja ya sh.10.000 na nyingine ya 40,000. NIlijiuliza kwa nini lakini leo nimepata jibuHabari za majukumu wanajamii,
Habari hii ni kupata uzoefu zaidi, kutahadharishana na kuwekana sawa wakati huu mgumu wa uchumi wa kati.
Nimekutana na matukio mawili kwa nyakati tofauti ya kuibiwa na wahudumu wanaotoa huduma ya kuweka mafuta katika kituo kimoja cha mafuta cha TOTAL kilichopo Oysterbay (pale ambapo kuna vituo pacha katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi karibu na mataa ya kwenye makutano ya kuelekea St. Peter, kile kilichopo upande wa FAO, upande ambao kuna JANGID BUILDING).
Mara ya kwanza nilimgundua muhudumu kuwa ameanza kunijazia mafuta hali ya kuwa kwenye pampu kulikuwa kunasomeka Tshs 5,000 ambayo inaonekana alimuwekea mteja aliepita na hakutoa risiti, nikamueleza alichofanya na akakiri kosa lake na kuniwekea mafuta yangu ya Tshs. 5,000 nikaridhika na kimoyomoyo nikasema kuwa haya ni matokeo ya malipo duni kutoka kwa waajiri na ugumu wa maisha, mara ya pili leo (ambayo imenilazimu kuandika uzi huu mrefu), muhudumu kama kawaida kanifanyia ujanja wa kuniita pampu ya mbele halafu baadae akabadili mawazo na kuniambia nisogee nyuma ili aniwekee kutokea pampu ya nyuma (kumbe hii ilikuwa janja yake ya kunifanya nisiweze kusoma vema pale kwenye pampu).
Nami kwa haraka haraka nikakumbuka nilichofanywa mara ya kwanza, nikashuka kwenye gari na kuwahi kusoma kwenye pampu, nikakuta keshaanza kuweka mafuta na kwa sekunde kama 5 tayari pampu imeshafika Tshs 12,000, nikamwambia dada najua umeanzia kwenye elfu 10, akataka kubisha na kuwa mkali, nikamwambia ntakuharibia kazi yako kwa sababu ya Tshs. 10,000 naomba uniwekee mafuta yangu kama pesa niliyokupa. Akataharuki na kuniwekea mafuta yangu yote kulingana na pesa niliyompatia, kwahiyo kwenye pampu ikasoma Tshs 10,000 zaidi ya ile pesa niliyompa aweke mafuta na risiti nikapata ikiwa na Tshs. 10,000 zaidi.
SOMO KWA WAMILIKI WA KITUO
Tafadhali sana wamiliki wa vituo hivi, siwaingilii kwenye biashara yenu ila ni vema kuwashauri kwa ustawi wa biashara yenu: Wale wahudumu sio waaminifu, fanyeni uchunguzi wenu na mkibaini hilo chukueni hatua stahiki, kwa sababu haya wanayoyafanya yatawaharibia biashara zenu na kuleta mdororo. Walipeni vizuri, wapeni mazingira mazuri ya kazi, hakikisheni mnaweka mashine nzuri zinazosomeka kwa ufasaha bila shida.
USHAURI KWA WATUMIAJI WA HUDUMA HII
Tuwe makini wakati wa kuwekewa mafuta, tuhakiki kuwa namba zote kwenye display ya pampu zinaanzia sifuri (zero) kwenye Lita na Kiasi cha pesa. Ikiwezekana tusikubali kuwekewa mafuta mpaka tushuke na kuhakiki kuwa pampu inasomeka vema na inaonesha inaanzia sifuri. Tusiwaamini wahudumu, nao ni binadamu, wanaingiwa na majaribu na vishawishi. Kuna mbinu nyingi za udanganyi kwenye hizi pampu tushirikishane ili tupambane na kuumizana huku ambako hakuna sababu. Tumuogope Mungu na kusema ukweli wakati wote, ikiwezekana unapokutana na uovu kama huu ukomeshe kwa njia yoyote inayowezekana ili kuwaokoa wengine na udhalimu huo.
Ahsanteni sana
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]Tatizo macho na msambwanda huwa vinavutana automatically.
Ulivyoandika mwenyewe unajiona una akiiiiili... Kuweka mafuta ukiwa ndani ya gari ni ku risk sana mkuu... Unashauriwa kushuka ndio maana magari ya abiria hayaruhusiwi kuingia gas station likiwa na abiria...... madereva wanaotoka nje sometimes wanapoteza sana muda especially rush hours. Hivi huwezi kukaa kwenye gari na bado ukasoma vizuri pump? Unless ni semi-trailer na tank liko kule nyuma kabisa ila kwa IST au Vitz, why should you get out of the car to be able to read the pump?
Kibajaji eti dereva "anatoka nje" kuhakiki mafuta; wanakera sana hawa ukiwa na haraka zako.
Aisee, nina uhakika hii 'comment' imehaririwa.[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]Sikupatii picha unavyotumbua hivyo vimacho vyako vya kichina kuangalia misambwandaAisee, nina uhakika hii 'comment' imehaririwa.
Hahahaha, tafadhali rejea uzi unasemaje ewe kikongwe na utuambie kama yaliyozungumzwa yalishakukuta?[emoji1787][emoji1787][emoji1787]Sikupatii picha unsvyotumbua hivyo vimacho vyako vya kichina kuangalia misambwanda
Ndio ndugu yangu, ni mkongwe kidogo, kwani kujoin lini kuna mahusiano yoyote na shughuli za kiuchumi?!Mana nmeona umejoin jf 2009
Swali zuri sana hili maana inashangaza na vipi kuhusu risiti itasomaje?... how possible is this? Kwa sababu, unless ulimkuta ile handle kaishikilia mkononi, ila ikisharudishwa mahali pake na kunyanyuliwa tena automatically ina-clear digits zote to zero. Yaani anawezaje kuanzia kiwango tofauti na zero? Naomba kuelimishwa.
Mmmh yote hayo umeyajuaje?Kuna namna wanaitegesha haifiki mwisho na kuruhusu kutoa risiti, wale binadamu wa mbinu sana, nami nilidhani nawasingizia ila nimekuja kugundua wameshagundua kuwa kuna namna ule mkonga ukiutegesha bila kuufikisha mwisho basi haita-clear zile digits pale kwenye meter reading na risiti haitoki.
... Mkuu; limeshajibiwa. Kwamba, kuna namna wanaegesha ile handle haifiki mwisho hivyo alipoishia namba hazifutiki; zinabaki vile vile. Inakuwa kama ame-hold on.Swali zuri sana hili maana inashangaza na vipi kuhusu risiti itasomaje?
WaTz kwa kulalamika tu tunaongoza walai.
Kimwanamke hicho... kina jeuri balaa!Kaka nitumie basi kwenye namba yangu 0621 111 123, nalia kwa sababu jasho nnalotoka kuipata linaniumiza sana, elfu 5 kwangu napata matunda ya kutosha sana kwenda kuwaongezea vitamin wanangu na kujenga heshima kwa mama yoyoooo. Mimi sitoi tip na wala huwa siendi hizo sehemu za kuacha acha tips, ninakula kwa mama ntilie, huko hakuna tip, tunadai hadi mia inayobaki baada ya kunywa kandoro!
Tatizo jeuri zake hazinisaidii kama hawezi kunitumia hata hiyo buku 5!Kimwanamke hicho... kina jeuri balaa!