Woga mkubwa wa Wabunge ni uchaguzi huru

Woga mkubwa wa Wabunge ni uchaguzi huru

Wabunge wengi wanajifanya wanapenda mipango ya mpendwa wetu Magufuli lakini kelele zote za kusema Mama afanye ya Magufuli ni woga wa uchaguzi huru. Kama wabunge wanafanya kazi ya wananchi na wamechaguliwa kihalali uoga wa nini?

Tuwape siri tu mipango yenu sio mipango ya Mungu na kama wewe umepata kinyemela Mungu atatafuta njia za kurekebisha ili haki ipatikane.

Mama anapenda haki na sio muda ataweka viongozi kwenye tume ya uchaguzi ambao wana nia ya kupeleka nchi mbele na sio kutumia pesa kunyanyasa wananchi. Mama katokea Zanzibar ambao kule kuna ushindani ukiacha huu uchaguzi haramu wa mwaka jana. Sio kitu cha ajabu kule Zanzibar kufanya kazi pamoja kwasababu wanajua fika jinsi gani uhasama unaweza kuzuia maendeleo.

Hivyo ndugu zangu tuwapuuzie hawa wabunge ambao hawana nia na nchi. Badala ya kujali nchi wanajali matumbo mpaka leo hawana lipya. Hii ni awamu ya sita na Mama atanyoosha nchi kwasababu ana akili, anajua kujieleza, anaelewa mifumo ya serikali na matatizo ya Watanzania. Lakini Mama vilevile anajua cha kufanya ni nini. Kaimu wake Mpango anajua miradi yote ya Tanzania.

Tusubiri Tanzania iende mbele zaidi. Kuna watu wanapenda ugomvi kila siku watapata shida maana mama hana drama hizo.
Yaani ukiwaangalia usoni utadhani wanamtaka ayaenzi yale mema ya magu lakini moyoni na dhamira zao zinamtaka aendeleze udikteta, wizi, ubabe na Utekaji ili vitumbua vyao viwe salama.

Wana hofu kama Mama akiridhia mchakato wa katiba mpya.
 
Tatizo upumbavu ndio unaowasumbua miaka yote, huyo unayemuita Ibilisi sasa hivi mwanzo mwa utawala wake mlimsifia sana hapa ila akaanza kubadilika kidogo kidogo sasa naona upumbavu hamjaacha mnarudia tena yaleyale kwa huyu Mama hata miezi sita hana hapo madarakani. Najua tu mlivyo wapumbavu najua tu lazima mtakuja tu kumtukana Mama wa watu maana ndio mpo hivyo miaka yote maana mnajulikana kwa upumbavu wenu.

Mimi nasisitiza tu kuwa huyo Mama ni Ccm.
Ibilisi mkubwa mwendazake.
 
Tafuta popote nilipowahi kumsifia ibilisi, sio akiwa rais hata alipokuwa waziri tu. Huyu mimi sijaanza kumsifu hadi zifike siku 100, ila kwasasa ni kwamba kaamua kujitenga na tabia za dhalimu.
Sasa si ndio umemsifu hapo au hata kusifu hujui ni nini?
 
Zama zile ukisikia jina Mbunge, lilikuwa jina la heshima sana, kwasasa wamekuwa vituko
Cha ajabu vituko vimeongezeka Mimi binafsi Halima na wenzie 18 nawaona hawana tofauti na kibajaji. Halima ananiuma kama kidonda ananyang'anywa ushindi WA halali halafu anatupiwa makombo kama mbwa. Naamini hana Raha ni basi Tu majukumu na hofu ya kuishi kama shetani.
 
Tatizo upumbavu ndio unaowasumbua miaka yote, huyo unayemuita Ibilisi sasa hivi mwanzo mwa utawala wake mlimsifia sana hapa ila akaanza kubadilika kidogo kidogo sasa naona upumbavu hamjaacha mnarudia tena yaleyale kwa huyu Mama hata miezi sita hana hapo madarakani. Najua tu mlivyo wapumbavu najua tu lazima mtakuja tu kumtukana Mama wa watu maana ndio mpo hivyo miaka yote maana mnajulikana kwa upumbavu wenu.

Mimi nasisitiza tu kuwa huyo Mama ni Ccm.
Unajua Ibilisi/Shetani/Lucifer naye alikuwa malaika huko Mbinguni!!??
Baadaye unajua nini kilitokea.
 
Wajumbe bado tunawamind wale wote waliopitishwa kimazabe na yule mwengine
Nalog off
 
Ndio, nimemsifu ili usiseme ninapinga kila kitu.
Sio nisiseme bali hivyo ndio mlivyo,kupinga kila kitu ndio style yenu na mkiambiwa mnasema kwa sababu ni wapinzani. Huyu mama ni suala la muda tu mtaanza kupinga hadi mnayoyapendekeza sasa hivi, hapo utanielewa kwanini nawaita wapumbavu.
 
Back
Top Bottom