World Bank to officially declare Tanzania a Middle Income Country (MIC) on July 01, 2020

World Bank to officially declare Tanzania a Middle Income Country (MIC) on July 01, 2020

Hahaha yani mnataka JPM aitishe press na kutangaza TZ kuingia MIC!? Hiyo kitu haipo, kwanza kwa mipango ya maendeleo ya nchi ilikuwa tunajua bado kufikia huko middle income. Ni kihere here tu cha WB kutupeleka huko. Hivyo sio ishu kubwa ya hivyo. Najua ingekuwa ni hapo kunyaland mngefanya dhifa kubwa ikulu na kuteketeza a lot of tax payers money.
Na ukitegemea kuna faida zitokanazo na kuwa LDC, hii inaweza ikawa ni habari mbaya kwao
 
The World Bank is to officially declare Tanzania a middle income country as of 1st July 2020. Jumuiya ya Afrika Mashariki sasa inakuwa na mataifa mawili kwenye kundi la MICs.

Swali: Itakuwaje kuhusu East African Community - European Union Economic Partnership Agreement? Maana Tanzania iligoma ikiamini kwamba italindwa na ile special arrangement kwa nchi maskini. Yetu macho!
Hongereni watanzania!

Hongera watanzania sio hongera JPM
Tumepata nini sisi?
Hongera kwake yeye anayefaidika kisiasa.
 
Soma hii comment [emoji23][emoji23][emoji23]
Cicero,
Huu ni uongo mtupu. Dunia itapasuka katikati kabla ya hili kufanyika.
Wana wivu wa kijinga mnoo.
[emoji116][emoji116][emoji3][emoji3][emoji3]

1. Denial

2. Negotiation

3. Acceptance

Na huwa wanapita hzo hatua kwa kasi ya umeme [emoji3][emoji3][emoji3]
 
Kuwa makini kabla ya kulalamika kila wakati. Rudi nyuma kasome post nambari 185 ya Meela Gift. Amekuwekea link ya World Bank ambayo inaonyesha wazi World Bank wamebadilisha TZ kutoka Ldc hadi Mic. Jifunze saa zingine kuclick link na kusoma. Link haipo hapo kwa sababu ya mapambo. Uvivu wa kusoma ndio unayo.
Huyo ni kundi fulani huku Tz tunaita Nyumbu. Kazi yao ni kupinga tu.
 
Kaka wewe ni mmoja wa Watanzania ambao huwa naona wana akili hata kwenye kupanga hoja zao, na nikijadili na watu kama wewe huwa inabidi niweke pembeni mambo ya ligi na kuvuta aerial ili tuendane vizuri, ila hapa najaribu nikuelewe nashindwa nini haswa unachobishia, utawalaumu vipi wale watoa mikopo, wao hushinikiza itumiwe vizuri lakini hawana uwezo wa kuja kukagua tofali kwa tofali, hilo sio jukumu lao.
Mimi nimefanya miradi kadhaa iliyogharamikiwa na Benki kuu ya dunia (WB), walikua wanatuma wakaguzi mara moja moja kufanya high level survey, na kila tukikamilisha tulikua tunawapa reports, ila hawakua na uwezo kuingia kwenye kila kitu kukagua, ilikua jukumu la maafisa wa serikali kuhakikisha ubora wa miradi yenyewe sio WB.
Sasa hapo unakuta hao maafisa kwanza wanapiga hela kupita maelezo na hamna mwenye jeuri ya kuwahoji. Lakini upande wa pili miradi yenyewe ilikua na umuhimu mkubwa kwa jamii.

Mkuu kwanza shukrani kwa kutambua kwamba kwenye baadhi ya mambo nna uelewa japo kidogo.
Pili, sibishi chochote hapa Kaka, naomba nifupishe maneno kwa kusema kwamba, malengo ya WB na UN siku zote ni kulinda maslahi ya wenyewe. Kwa muktadha huo, watawapamba na kulingana na wao wanataka kitu gani na endapo maslahi yao hayaathiriki. Naweza kuwa siko sahihi ila kwa kuwa nimefanya nao kazi muda mrefu, huo ndio mtazamo wangu.

Hapa tulitakiwa tuwe tunajadili sababu gani au vigezo vipi vimetufikisha hapo, na je, ukuaji huo wa uchumi unafika kwa wananchi? Kuna namna tunaweza ongeza zaidi ufanisi wa utendaji kuendelea kufanya vizuri zaidi? Kuna hatari ya kuporomoka endapo baadhi ya mambo hayatachukuliwa umakini unaostahili? Nnachostaajabu hoja imekua tutawapita Kenya, mara hamtuwezi, mtasalimu amri n.k tumelewa sifa.

Unakumbuka China wamewahi kukataa kwa nguvu zote ukuaji wa uchumi wao kukua kwa kasi kiasi cha kuwa hatarishi kwa US?

Ni sawa na mtu aniambie niko smart wakati nauelewa uwezo wangu na lengo lake ni kutaka anitumie kwa manufaa yake. (Itategemea ana malengo gani na anatumia vigezo vipi).
 
Back
Top Bottom