Uchaguzi 2020 World Bank yapitisha Mkopo wa Zaidi ya Trillion 1 Uliopingwa na Wanasiasa pamoja na Wanaharakati

Haki ya Mungu hapa kijana Zitto na wenzake wanajipiga vidole kwa hasira huku wakinywa dozi ya Hand Sanitizer kuondoa haibu.
 
ZITTO KABWE AUMBUKA.

Kampeni yake chafu dhidi ya Tanzania yakwama.
_
Benki ya Dunia yaidhinisha Mabilioni ya fedha za kusaidia Elimu alizotaka Tanzania inyimwe.

Saa chache zilizopita Benki ya Dunia kupitia Bodi ya Wakurugenzi Watendaji ya Chama cha Maendeleo ya Kimataifa (IDA) imefanya maamuzi ya kihistoria ya kuruhusu mkopo wa Dola za Marekani Milioni 500 utolewe kwa Tanzania kwa ajili ya kusaidia kuboresha elimu ya Sekondari baada ya mjadala mrefu uliochukua miezi zaidi ya mitatu.

Uamuzi wa Benki ya Dunia umezima kampeni ya kidhalimu iliyofanywa na Mwanasiasa mpuuzi Zitto Kabwe aliyeandika barua kwenda benki hiyo akitumia nembo za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutaka Tanzania inyimwe mkopo huo bila kujali athari zake kwa wananchi hasa wanyonge na maskini.

Zitto Kabwe akishirikiana na mabeberu wanaomfadhili alifanya uharamia kwa kuchochea uongo kuwa Tanzania inakandamiza wanafunzi wa kike kwa kuwanyima fursa ya kuendelea na masomo baada ya kupata ujauzito ilihali anajua kuwa sio kweli na kuna utaratibu ulio wazi wa watoto hao kupata elimu kupitia programu mbalimbali za Elimu ya Watu Wazima, Mpango wa Elimu kwa walioikosa na vyuo mbalimbali.

Hili ni pigo jingine baya sana kwa Zitto Kabwe na washirika wake ambao wamekuwa wakiichonganisha na kuichafua Serikali ya Tanzania na Mashirika ya Kitamaifa kwa kutafuta umaarufu wa kisiasa bila kujali athari ambazo wananchi wanazipata kutokana na kuinanga Tanzania ama kukwamisha miradi mikubwa na washirika wa maendeleo.

Katika safari ndefu ya mjadala ambao ulianza tangu Januari mwaka huu wa 2020, Benki ya Dunia imepiga chini msimamo wa mabeberu waliotaka Tanzania inyimwe fedha hizo baada ya kuingizwa mkenge na Zitto Kabwe.

Watu wengi wanaweza kujiuliza kwa nini Zitto Kabwe na wafadhili wake walikuwa wanashupalia Tanzania inyimwe fedha hizo? Ukweli ni kwamba Zitto na wadhalimu wenzake hawakuzuia fedha hizo kwa sababu ya kupigania wanafunzi wa kike wanaopata ujauzito wakiwa shule kama wanavyodai, bali walishupalia Tanzania isipewe fedha hizo baada ya msimamo wa Serikali ya Awamu ya Tano kukataa kukopeshwa fedha ambazo zingeingizwa nchi kupitia mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO) na miradi ambayo haina matokeo kwa wananchi ili baadaye zitumike kwa maslahi ya siasa za upinzani na sio wananchi.

Kwenye hili, Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Jemedali Rais Dk. John Pombe Joseph Magufuli inastahili pongezi za dhati kwa msimamo thabiti usiyoyumba na ushindi mkubwa dhidi ya kibaraka Zitto Kabwe na washirika wake ambao wamekuwa wakipiga tripu kwenda mabeberu hao kufanya kampeni ya kuiangamiza Tanzania eti wakitaka kuiondoa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) madarakani.

Kongole Rais Magufuli, hongera Watanzania wote kwa ushindi huu mkubwa. Zitto Kabwe na washirika wake washindwe na walegee.

Sasa Tanzania itapata Dola za Marekani Milioni 500 sawa na zaidi ya shilingi Trilioni 1 na Bilioni 135 kwa ajili ya kuongeza idadi ya wanafunzi wanaopata elimu ya Sekondari, kuboresha mazingira ya elimu kwa wasichana na kuinua ubora wa elimu kwa wasichana na wavulana.

Mkopo huu ni wa gharama nafuu na sio fedha za bure. Watanzania watazilipa, lakini sasa watalipa fedha ambazo zinakopwa na kuelekezwa kuwasaidia mamilioni ya Watoto wa Tanzania na sio kwenda kwenye NGO na miradi ya kupitisha fedha zinazokwenda kwa wachumia tumbo akina Zitto Kabwe na washirika wake.

Tunaamini Serikali ya Tanzania itatoa mchanganuo wa fedha hizi zinakwenda wapi na zitawanufaishaje Wanzania.

Kila la kheri Watanzania na pole sana Zitto Kabwe kwa kuangukia pua katika mchazo huu mchafu. Tambua kuwa Mwenyezi Mungu husimama na wenye haki na katika hili amesimama na Watanzania wenye haki na Rais wao mpendwa Dk. John Pombe Joseph Magufuli.

Taarifa hii haina uhusiano na siku ya Wajinga Duniani. Ni ukweli mtupu na inapatikana katika tovuti mbalimbali za Kimataifa. Waweza kuisoma hapa kwenye tovuti ya Benki ya Dunia yenyewe

New Financing to Make Secondary Education Safer, Better, and More Accessible for Tanzanian Girls and Boys

Mwl. Damas Masele MPJ
Mkufunzi Mstaafu.
31 Machi, 2020.

Sent using Jamii Forums mobile app
Over the past two years, about 300,000 children, half of them girls, have been unable to continue their lower secondary education due to insufficient space in public schools. In addition, an estimated 5,500 Tanzanian girls who are pregnant drop out every year. SEQUIP has been designed to enable more adolescent girls and boys to transition to upper secondary education. It gives pregnant girls, young mothers, and other vulnerable children who leave school early the possibility to return to the formal system and complete their education. The project tackles the issues facing pregnant girls with an approach informed by civil society organizations and NGOs, in Tanzania and around the world.

“SEQUIP’s design strives to give pregnant girls and young mothers a better chance to complete their education,” said Caren Grown, Senior Director of the Gender Group at the World Bank. “The Bank has stepped up its work to create a new generation of education programs that emphasize safe school environments for girls and boys, including measures that reduce gender-based violence, corporal punishment, bullying, and other forms of violence in and around schools. It gives girls better quality choices and opportunities for completing their secondary education.”
 
Mkuu sisi si tunatumia pesa zetu za ndani kwenye kila kitu...mkopo wa nini tena jamani? ET2019,

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama una uwezo wa kukopeshwa ina maana una uwezo wa kulipa. Pesa unazotumia kulipa ni pesa zako za ndani. Kwa maana hiyo huo mkopo ni kama unatumia pesa zako mwenyewe. Ni tofauti na msaada ambao pesa si zako hivyo mwenye kauli ni yule aliyrkupa msaada.
 
Hii ni habari mbaya sana ambayo hatukutegemea kamanda. Tubaki kujifaragua tu.
Masharti yamefikiwa!
1.Watoto wa kike watakaojifungua kurudi shule katika mfumo rasmi!
2.Mkopo hautoki kwa pamoja!
Naona hoja za Zitto zimetoboa!

Over the past two years, about 300,000 children, half of them girls, have been unable to continue their lower secondary education due to insufficient space in public schools. In addition, an estimated 5,500 Tanzanian girls who are pregnant drop out every year. SEQUIP has been designed to enable more adolescent girls and boys to transition to upper secondary education. It gives pregnant girls, young mothers, and other vulnerable children who leave school early the possibility to return to the formal system and complete their education. The project tackles the issues facing pregnant girls with an approach informed by civil society organizations and NGOs, in Tanzania and around the world.

“SEQUIP’s design strives to give pregnant girls and young mothers a better chance to complete their education,” said Caren Grown, Senior Director of the Gender Group at the World Bank. “The Bank has stepped up its work to create a new generation of education programs that emphasize safe school environments for girls and boys, including measures that reduce gender-based violence, corporal punishment, bullying, and other forms of violence in and around schools. It gives girls better quality choices and opportunities for completing their secondary education.”
 
Haki ya Mungu hapa kijana Zitto na wenzake wanajipiga vidole kwa hasira huku wakinywa dozi ya Hand Sanitizer kuondoa haibu.
Sasa kama masharti yamefikiwa huoni ni win win situation?Mtoto wa kike atakayepata ujauzito atarejea shuleni baada ya kujifungua,hilo ndio la msingi!
 
Sawa! Issue nipesa kutolewa! Na issue ya pili ni ukipigwa mimba nenda qt au veta.
Hayo mashart mengine yte nimazuri maana yamelenga kulinda mkopo utumike sawasawa.
Hoja mbili za Zitto kuzuia mkopo huo ni hizi:
-Wanafunzi wajawazito
-Pesa kutotolewa kipindi hiki cha uchaguzi!

Yote hayo Zitto kayapata!

Over the past two years, about 300,000 children, half of them girls, have been unable to continue their lower secondary education due to insufficient space in public schools. In addition, an estimated 5,500 Tanzanian girls who are pregnant drop out every year. SEQUIP has been designed to enable more adolescent girls and boys to transition to upper secondary education. It gives pregnant girls, young mothers, and other vulnerable children who leave school early the possibility to return to the formal system and complete their education. The project tackles the issues facing pregnant girls with an approach informed by civil society organizations and NGOs, in Tanzania and around the world.

“SEQUIP’s design strives to give pregnant girls and young mothers a better chance to complete their education,” said Caren Grown, Senior Director of the Gender Group at the World Bank. “The Bank has stepped up its work to create a new generation of education programs that emphasize safe school environments for girls and boys, including measures that reduce gender-based violence, corporal punishment, bullying, and other forms of violence in and around schools. It gives girls better quality choices and opportunities for completing their secondary education.”
 
Kha vizuri sana, Magufuli komaa tu watakuelewa mzee, kazi yako inaonekana na kukubalika Afrika yote na dunia yote.
 
Kwa kuangalia mjadala huu, alisema wazi kwamba kuzuia watoto waliopata ujauzito ni kuwabagua, na kwahiyo sio sahii WB kutoa mkopo utakaobagua hususani watoto wa maskini!

Now tell me: Hivi unaamini kabisa mtoto angalau wa mtumishi anayelipwa Laki 5 kwa mwezi atashindwa kuendelea na masomo kisa kapata ujauzito?!

Hivi unaamini kabisa mtoto wa mfanyabiashara mwenye uwezo wake anaweza kushindwa kuendelea na elimu ya sekondari wakati private schools zimejaa kila kona?!

In contrast, hivi unaamini kabisa mtoto wa maskini kule kijijini akipata uja uzito wazazi wake watakuwa na uwezo wa kumpeleka private school kama wanavyoweza kufanya wazazi wengine wenye kipato?!

Ina maana hadi hapo hujaona umuhimu wa hoja ya akina Zitto na Wanaharakati wengine?!

Hilo la Tundu Lissu nimeshaliongea sana hadi naona uvivu kurudia rudia lakini itoshe tu kusema kwamba, dana dana za Acacia zilikuwa nyingi kwa sababu serikali haikutaka kumsikiliza Lissu!!

Wakati hoja ya msingi ya Lissu ilikuwa kama kweli unataka kupambana na multinational companies basi serikali ijiondoe kwanza kwenye mikataba ya kimataifa inayowalinda sana foreign investors kuliko host countries, wafuasi wa Magu waka-twist na kusema TL amesema serikali iki-deal na Acacia tutapelekwa mahakamani huku wakitamba mbona hawatupeleki basi!!

Swali ambalo mara zote nimekuwa nikiuliza bila kupaat jibu ni kipi kitakachowafanya Acacia watupeleke kwenye mazingira yaliyopo!!

Tulisema tunawadai matrioni ya shilingi, hadi kesho hata senti tano haijatoka na HAITATOKA!!

Wenyewe wakaahidi watatoa kishika uchumba cha USD 300M lakini hadi kesho hadi senti 5 haijatoka!! Hii inaweza kutoka lakini itatoka kwa kuangalia masharti waliyoweka jambo ambalo ndilo linafanya hadi sasa wasiwe wametoa hata sent moja kwa sababu hatujatekeleza masharti yao!

Sasa kwanini Acacia walileta danadana zote hizo?! Kwa sababu walijua hatuwezi kuwafanya chochote wakati wanalindwa na Mikataba ya Uwekezaji! Lakini kama serikali ingejitoa MiGA (ambayo pia ni risk), Acacia wasingefanya danadana kwa sababu wangefahamu wasingekuwa na kwa kukimbilia!!
Hivi unaongea ukiwa unaifahamu Tz au unasikiaaika tu kuhusu Tz! Ni utamaduni wa kitz mtoto akipaxhikwa mimba anatimuliwa shule na antafita njia mbadala za elimu ya watu wazima! Maana hatakuwa tena kwenye kundi la watoto bali wazazi! Huu utamaduni kwa kiasi kikubwa umesaidia kuwatisha wototo wa kike kuogopa kushiriki ngono za kizembe! Haiingii akilini, mtu mwenye akili timamu aje kutaka wazazi nao waruhuaiwe kusoma na watoto wakati kuna elimu ya watu wazima! Hoja ya huyo ziro wako huyo haikuwa na mashiko hata kidogo ndio maana wameidharau hata hao watoa mkopo! Kuhusu TL, hayo unayosema sijui umeyatoa wapi!? Tumesikia wenyewe kwa masikio yetu mara nyingi sana hata kabla blankoo hazijamjeruhi, akiwatetea mabeberu na hata kuwapatia habari na taarifa muhimu za namna ya kuikomoa serikali na nchi yetu! Ww umetumwa na nani kwa kuandika gazeti lililosheni uzushi huu! Hata sasa TL ndio kaamua kuonyeza rangi zake za asili kwa yale anayopakazia nxhi yetu kwa jamaa zake mabeberu!
 
Tuendelee kujibaraguza tu kamanda. Hii habari hatukuitegemea kabisaa.
Ilitegemewa kwani tulijua lazima serikali ibadili msimamo!Halafu huo ulikuwa msimamo binafsi wa JPM wala sio serikali nzima so tulijua itakuwa rahisi kubadili maamuzi yake!So its okay kwangu kwa hayo mambo mawili-
1.Fedha kutoka baada ya uchaguzi
2.Watoto wakaojifungua kupewa nafasi katika mfumo rasmi!
Kwa hayo,nimeridhika na moyo mweupee kabisaaa!😀
 
Kamanda leo tutaandika insha nyingi. Hii habari imetukera kwa kweli.
 
Hivi unaongea ukiwa unaifahamu Tz au unasikiaaika tu kuhusu Tz! Ni utamaduni wa kitz mtoto akipaxhikwa mimba anatimuliwa shule na antafita njia mbadala za elimu ya watu wazima! Maana hatakuwa tena kwenye kundi la watoto bali wazazi! Huu utamaduni kwa kiasi kikubwa umesaidia kuwatisha wototo wa kike kuogopa kushiriki ngono za kizembe! Haiingii akilini, mtu mwenye akili timamu aje kutaka wazazi nao waruhuaiwe kusoma na watoto wakati kuna elimu ya watu wazima! Hoja ya huyo ziro wako huyo haikuwa na mashiko hata kidogo ndio maana wameidharau hata hao watoa mkopo! Kuhusu TL, hayo unayosema sijui umeyatoa wapi!? Tumesikia wenyewe kwa masikio yetu mara nyingi sana hata kabla blankoo hazijamjeruhi, akiwatetea mabeberu na hata kuwapatia habari na taarifa muhimu za namna ya kuikomoa serikali na nchi yetu! Ww umetumwa na nani kwa kuandika gazeti lililosheni uzushi huu! Hata sasa TL ndio kaamua kuonyeza rangi zake za asili kwa yale anayopakazia nxhi yetu kwa jamaa zake mabeberu!
Watoto 5500 kila mwaka wana drop out kutokana na kupigwa mimba,wewe unasema wanaogopa kutokana na kufukuzwa shule!Are you serious?Wengi wao wanapigwa mimba kutokana na mazingira ya kusomea kutokuwa rafiki kwao!

Back
Top Bottom