Hivi unaongea ukiwa unaifahamu Tz au unasikiaaika tu kuhusu Tz! Ni utamaduni wa kitz mtoto akipaxhikwa mimba anatimuliwa shule na antafita njia mbadala za elimu ya watu wazima!
FYI, huwa siandiki mambo kwa hisia kama mfanyavyo wengine especially watetezi wa mfumo! Kwamba ni "utamaduni wa Kitanzania" maana yake nini?! Taifa haliendeshwi kwa tamaduni bali kwa misingi iliyojiwekea!!
Tafuta online, au nenda pale Wizara ya Elimu waombe document titled:
Huo ni muongozo wa serikali kupitia Wizara ya Elimu ambao ulitolewa April 2009. Section 2.3 ya muongozo inatoa maelekezo kwa wazazi/walezi kwamba:-
- Shall be counseled and guided by the school leadership on the pregnancy of the school girl;
- Shall show empathy and accept to take care of the pregnant girl;
- Shall be guided and counseled by the school leadership concerning maternal health of the pregnant schoolgirl;
- Shall be informed and required to fulfill re-admittance requirements;
- Shall be required to update the school leadership on the health condition during pregnancy and after birth; and
- Shall be involved in deciding on which mode of education (Formal or informal) and school the pregnant girl would like to continue with, after giving birth.
Aidha, section 2.6 ya Muongozo unatoa maelekezo kwa serikali kwamba:-
- Shall educate and sensitize the society/community on the importance of readmitting impregnated school girls;
- Shall educate and sensitize the society/community on the process of readmitting impregnated school girls; and
- Shall empower school leadership on the issue of readmission of pregnant school girls; and
- Shall task the ward social welfare officers to monitor the health welfare of the impregnated school girls.
Huo ndio MWONGOZO halali ambao Magufuli anaukanyaga! Sasa wewe niwekee hapa huo utamaduni unaosema kwamba watoto wa kike wakipata ujauzito, ni marufu kuendelea na elimu rasmi kwa shule za serikali!!!
Maana hatakuwa tena kwenye kundi la watoto bali wazazi! Huu utamaduni kwa kiasi kikubwa umesaidia kuwatisha wototo wa kike kuogopa kushiriki ngono za kizembe!
Kwanini uwatishe badala ya kuweka mikakati inayoeleweka kuhakikisha hakuna ujauzito?! Hivi unaweza kunieleza hapa serikali ina mkakati upi kuhakikisha watoto hawafanyi ngono za mapema au angalau hizo ngono salama?
Btw, kama kuwatisha mbona mimba bado zipo pale pale hata siku hizi ambapo watoto wanaanza shule mapema sana?
Haiingii akilini, mtu mwenye akili timamu aje kutaka wazazi nao waruhuaiwe kusoma na watoto wakati kuna elimu ya watu wazima!
Unamaanisha Wizara ya Elimu hawana akili timamu, au?!
Ukweli ni kwamba, kama nilivyowahi kusema kwenye post moja wapo hapa jamvini, Mh. JPM ni mkurupukaji, na wala hafahamu misingi ya serikali mwenyewe!!
Hapa JPM alikuwa kama wewe tu kwa kuamini "
kutimua shule wanaopata ujauzito ni utamaduni wetu" bila kufahamu mwaka 2009 serikali kupitia wizara ilitengeneza utaratibu wa kuhakikisha watoto wanopata ujauzito hawafukuzwi, bali wanakuwa suspended na kurudi tena shuleni unless kama ataamu mwenyewe kuendelea kwenye mfumo usio rasmi ambao Magufuli na wafuasi wake wanadhani ndo sheria inavyosema!
Hoja ya huyo ziro wako huyo haikuwa na mashiko hata kidogo ndio maana wameidharau hata hao watoa mkopo!
Hoja ya Zitto kivipi?! Kwani Zitto anafanya kazi Wizara ya Elimu au alihusika kwenye kuandaa huo muongozo?
Btw, Wakopeshaji gani waliodharau hoja ya Zitto?!
Hivi umesoma maelezo ya WB au unaongea tu?!
Kipengele kimoja cha taarifa ya World Bank kinasema:-
Of the 60,000 students who drop out of secondary school every year in Tanzania, 5,500 leave due to pregnancy. While there is no government policy that states that students who become pregnant must be expelled from public schools, most pregnant girls do drop out.
Hiyo ndo kauli ya WB ambayo inaakisi sehemu ya mwongozo wa serikali nilioweka hapo juu!
Kwa maana nyingine, suala la wanafunzi kutimuliwa sio la kisera bali ni la JPM na watu wake!!!
Sehemu nyingine ya taarifa hiyo ya WB inasema:-
through discussions during project preparation, the government has reconfirmed its commitment that all children who take Form 4 or Form 6 examinations, regardless of which education institution they have attended, will have the opportunity to continue their education in the public school or college system.
Sasa wewe habari kwamba WB wamempuuza Zitto umezitoa wapi?!
Na labda nikujuze lingine! WB hawatatoa fungu lote kwa pamoja bali watatoa kwa awamu baada ya kuhakikisha serikali inatekeleza masharti waliyopewa, including kuwaacha watoto wajawazito kuendelea na shule kama mwongozo wa wizara unavyosema:-
Of the project funds, 96 percent (US$480 million) are subject to (a) achievement of agreed results verified by an Independent Verification Agent subject to the World Bank’s approval; and (b) submission of evidence that the government has already spent an equivalent amount on eligible expenditures in the secondary education sector. Assuming that these conditions are met each year, the disbursement schedule, is as follows:
- FY 2021 - US$72.47 million
- FY 2022 - US$101.10 million
- FY 2023 - US$114.73 million
- FY 2024 - US$98.52 million
- FY 2025 - US$85.37 million
- FY 2026 - US$27.81 million
Na sio tu kwamba serikali watakuwa wanasema "tumetekeleza kwa kiwango fulani bali hadi pale Independent Verification Agent atakapothibitisha!!!
Kuhusu TL, hayo unayosema sijui umeyatoa wapi!? Tumesikia wenyewe kwa masikio yetu mara nyingi sana hata kabla blankoo hazijamjeruhi, akiwatetea mabeberu na hata kuwapatia habari na taarifa muhimu za namna ya kuikomoa serikali na nchi yetu! Ww umetumwa na nani kwa kuandika gazeti lililosheni uzushi huu! Hata sasa TL ndio kaamua kuonyeza rangi zake za asili kwa yale anayopakazia nxhi yetu kwa jamaa zake mabeberu!
Eti mmesikia wenyewe, achana na hao wengine; niambie wewe ulimsikia wapi kama sio unatumia nukuu za propaganda za Lumumba!!
Ambacho alisema Tundu Lissu, ni hiki hapa chini:-
Hiyo video ni ya dakika 3:43 lakini MATAGA kwa kujua Wa-TZ hamna utamaduni wa kutafuta ukweli, waka wanaongelea maeleo ya dakika 2 za mwanzo na wakawaficha zaidi ya dakika 1 unusu nyingine zilizobaki!
Sasa pamoja na kunitolea povu kwamba eti nimetumwa kuandika uzushi, kwa mwenye akili timamu hapa atajua ni nani aliyetumwa kuleta uzushi kati yangu na wewe! Yote niliyosema hapo kabla nimekuwekea ushahidi, weka hapa ushahidi wa maelezo yako!!!