Whether namtetea Magu kwa jinsi ufahamu wako ukutumavyo au naelezea mambo ambayo uwezo wako kwa sasa ni mdogo sana kuelewa, hayo siyo muhimu kwa sasa! Sina tatizo na hiyo fedha, ninatatizo na future ya watoto wa kike nchini ukitekeleza utaratibu unaowaonyesha kutokuwa na tangible consequences za kubeba mimba kama kupoteza nafasi ya mfumo rasmi wa shule
Huo mwongozo umeanza 2009, unataka kusema kabla ya 2009 mimba mashuleni zilikuwa chache kwavile walikuwa wanahofia hizo consequencies na hivi sasa zipo maradufu kwa sababu they have nothing to fear?
Hivi unafahamu kwamba hapa tunazungumzia watoto wenye umri kuanzia 13 years, na majority ya waathirika ni young primary school gals, na wachache wa O-Level ambao na wenyewe bado wanakuwa na ufahamu mdogo?
Hivi unaamini kabisa kwamba watoto kama hao wakiona hawawezi kufukuzwa shule ndo basi tena watazaa hovyo hovyo kwa sababu hawana cha kuhofia?!
Hivi kabisa unaamini wale wasiopata mimba hawafanyi mapenzi kwa sababu wanahofia kufukuzwa shule?!
Hivi ulishawahi kujiuliza ni kwanini hili tatizo lipo sana vijijini ambako kwa kawaida ufahamu ni mdogo zaidi ukilinganisha na mijini?
Hivi ulishawahi kujiuliza ni kwanini mimba za hovyo hovyo vyuoni hazipo ingawaje sio haramu kupata mimba vyuoni?!!
Au hapa natakiwa kukukumbusha kwmba hizi mimba zinapatikana kutokana na kukosa uelewa na wala si kwa sababu ya kufanya ngono, na ndio maana wasichana kuanzia A-Level hadi vyuo "hawapati" mimba licha kwamba huenda wao ndio wanacharazwa zaidi kuliko hao wanaopata mimba!!!
Tunafahamu moja ya sheria kali kabisa Tanzania ni kumpa ujauzito mwanafunzi!
Now take an example of this gal: she's 15 or even less! Kwa sababu yoyote ile, anapata ujauzito! Unamtimua shule! Aliyempa mimba anaenda jela miaka 30! Na si ajabu anatoka kwenye poor family!!
Ulishawahi kujiuliza ni namna gani future ya mtoto kama huyo na yule atakayemzaa itakavyokuwa?!
Sheria zetu, na karibu duniani kote ukifanya ngono na msichana chini ya miaka 18 unaambiwa umembaka, na ukisema "alikubali mwenyewe" unaonekana mpuuzi!
Kwanini sheria inasema hivyo?! Au hapa unatakiwa tena kukumbushwa kwamba inaonekana msichana wa aina hiyo hana uwezo wa kufanya maamuzi sahihi?!
Sasa ikiwa hata 17 years girl anaonekana hana ukomavu wa akili wa kuweza kufanya maamuzi sahihi, what about wale wa primary schools ambao majority wapo under 15?!
Sitaki hata kuwaza kizazi gani tutakachokuwa tunatengeneza(kizazi cha watoto wazazi)
Tangu muanze kuwatimua shule, hicho kizazi cha watoto wazazi kimepungua?!
Narudia tena, misimamo yenu inaowaumiza ni watoto wa maskini wa vjijini kuliko watoto wa wenye uwezo na wale wa mijini! Ni kutokana na hilo ndo maana akina Zitto walisema wazi kwamba WB wakitoa mkopo watakuwa wanatoa mkopo unao-stimulate ubaguzi kati ya watoto walio nacho na wasio nacho!!
Hata mtoto wa Mwalimu wa Shule ya Msingi hawezi kupata mimba na akashindwa kuendelea na masomo, LAZIMA ATASOMA tu... tatizo ni kwa maskini!