Uchaguzi 2020 World Bank yapitisha Mkopo wa Zaidi ya Trillion 1 Uliopingwa na Wanasiasa pamoja na Wanaharakati

Uchaguzi 2020 World Bank yapitisha Mkopo wa Zaidi ya Trillion 1 Uliopingwa na Wanasiasa pamoja na Wanaharakati

Chige,
Unawezekana huo utaratibu na hiyo "sheria" ya kuzuia watoto wakipata ujauzito hawatakiwi tena kurudi shuke za serikali ali iko cpy na ku paste kutoka USA!

Huko ndivyo ilivyo! Lakini kwa akili zetu hizi wanatudanganya sisi tufanye mambo ya HOVYO katika shule zetu, Waende zao!
 
Mtapata taabu saaaana mkuu! SHETANI HAJAWAHI KUMSHINDA MWENYE HAKI, zitto mwenyewe katoa pongezi kupitia twiter! Naubaya sasa nayeye zitto yupo copyd.

Niaibu ya mchana kweupe, naitakuwa moja ya siraha yakumpigia zanziber na kigoma.
Kajifunze kuandika kwanza wewe lumumba buku 7!
 
Unawezekana huo utaratibu na hiyo "sheria" ya kuzuia watoto wakipata ujauzito hawatakiwi tena kurudi shuke za serikali ali iko cpy na ku paste kutoka USA! Huko ndivyo ilivyo! Lakini kwa akili zetu hizi wanatudanganya sisi tufanye mambo ya HOVYO katika shule zetu, Waende zao!
Yaani kumruhusu mtoto aendelee na shule ndiyo mambo ya hovyo?! Nyie watu ni watu wa ajabu sana!! Eti hawatakiwi kurudi shule za serikali. Jambazi anaua watu lakini akipelekwa hospitali huwezi kusema huyu hastahili kutibiwa hospitali za serikali!!

Kuna watu wanatumia mihadarati tena wakiwa watu wazima na akili zao lakini bado serikali inawahudumia!!

Kuna wengine wanafanya kazi ya ukahaba tena wakiwa watu wazima wenye akili timamu lakini wakipata maradhi yanayotokana na ngono hakuna anayesema wasitibiwe hospitali za serikali!!

Lakini leo hii, mtoto mdogo... na wengine wakijiingiza kwenye mapenzi bila kujua athari zake, mnatuambia wakipata mimba hawastahili kurudi shule za serikali!!

Undeni serikali zenu za kifamilia ndo mlete hizo sheria za hovyo hovyo!!!

na hapa narudia na nitarudia tena na tena, hizi sheria za kijinga mnazozitetea anayeathirika ni mtoto wa maskini! Mtoto wa mwenye nacho hata akipata mimba mara 7, atasoma tu labda mwenyewe asitake kusoma!!

Binafsi nimemaliza O-Level Private school back in 1996 na wakati tupo Form III, nakumbuka class kulikuwa na demu ana mtoto!! Hiyo ni 1995, hata private schools zenyewe zilikuwa chache! What about hivi sasa ambapo private schools zipo kila kona?! Unategemea kutakuwa na mtoto kutoka kwenye familia yenye uwezo ataacha kuendelea shule eti kisa kapata ujauzito?

And what about wale watoto wa vijijini wanaoenda shule bila hata kunywa chai?! Huo ubavu wa kwenda private schools wanao?!

Halafu hiv nyie watu kwani hao watoto wakiendelea na shule nyie mnapungukiwa na nini?! Wewe kwa mfano, hao watoto wakiendelea na shule wewe binafsi au hata familia yako mnapungukiwa na nini?!
 
Chige,
Halafu TATIZO lako wewe na wenzako, ni kuwa MMEKARIRI KUWA SHULE NI - SHULE YA MSINGI TU! Kwani hukusoma hayo majibu ya wataalam wa Benki yaDunia? Kwao "shule" siyo shule ya msingi na mtotoaliyezaa mtoto aende tena humo; kuna so manya avenues za "shule" kwa waliopata mimba na kuzaa.

Kuna MEMKWA, sijui kama unaifahamu au kuna utataratibu wa Elimu ya Watu Wazima au akivuka hapo kuna QTs au RESITTING na so many other alternative avenues. Msikaririshwe mambo ya hovyo na kuanza kuyatetea kwa mapovu jamani!
 
There is no mutual exclusivity here.

Why do some people see one?

Sent from my typewriter using Tapatalk
 
mukaruka mzee, Eti tumekariri shule ni shule ya msingi tu! Hapo juu nimetoa mfano wa mwanafunzi tuliyekuwa tunasoma nae wakati tupo Form III... ina maana Form III ni shule ya msingi?!

Btw, hayo majibu unayodai ni ya Wataalmu wa Benki ya Dunia umeyasomea wapi?! Benki ya Dunia wenyewe hawa hapa:-
1. Why is the World Bank supporting Tanzania’s education sector through the SEQUIP project?
The main goal of the project is to provide children in Tanzania with better, safer, and more accessible secondary education to help build the country’s human capital. Specifically, the project will: (a) keep children in school and help all secondary school dropouts, including pregnant girls, pursue their secondary education; and (b) provide them with a path back into the formal public education system in the next cycle.[
/QUOTE]Na sehemu ya pili Benki ya Dunia wanasema:-
2. How will SEQUIP support access to secondary school education for girls who drop out of school due to pregnancy?
Of the 60,000 students who drop out of secondary school every year in Tanzania, 5,500 leave due to pregnancy. While there is no government policy that states that students who become pregnant must be expelled from public schools, most pregnant girls do drop out.

Through the project and our ongoing policy dialogue with the government, the World Bank and other development partners will continue to advocate halting the practice of expelling pregnant girls from public schools in Tanzania so that they can continue their education in their existing school if they wish.
Sasa wewe hizo simulizi zako za MEMKWA zimetolewa na Benki ya Dunia ipi?!

Na ikiwa msimamo wao kwa wanafunzi wa sekondari ndo huo, what about primary school dropouts?
 
Basi hilo jeshi jingine chini ya Mfalme wa CDM limsaidie!
Kumbe unaleta ushabiki wa kisiasa hapa... shame on y'all!! Yaani upo radhi kuona watoto wa maskini wanakosa elimu kisa tu Magufuli aonekane alikuwa sahihi?!

Sorry, Magufuli alikurupuka bila kujua mwongozo wa wizara unasemaje na matokeo yake wameufyata!
 
Mataga kama wamekosa majibu nadhani wameitana kikao iliwaje na majibu
 
Update za leo big brother, USA wamepiga pini mkopo huo leo,wamesema wataupugis kura ya veto usitolewe kwa Tanzania Jiwe oyeeeee.
 
.. katika sakata hili Zitto ametoka kidedea. Maoni na mapendekezo yake yamezingatiwa.

..gazeti la mwananchi wameripoti kuwa fedha hazitatoka mpaka 2021.

..pia kutakuwa na ukaguzi wa WB ktk matumizi ya fedha hizo.

..vilevile hazitoki zote kwa wakati mmoja. Maana yake ni kwamba tukiharibu hapo katikati zinaweza kusitishwa.

..lingine ni kwamba huu ni MKOPO. Ni jambo la fedheha kununua ndege zinazotutia hasara halafu tunakwenda kukopa kwa ajili ya elimu.

Cc Chige
 
Kama una uwezo wa kukopeshwa ina maana una uwezo wa kulipa. Pesa unazotumia kulipa ni pesa zako za ndani. Kwa maana hiyo huo mkopo ni kama unatumia pesa zako mwenyewe. Ni tofauti na msaada ambao pesa si zako hivyo mwenye kauli ni yule aliyrkupa msaada.
Mkuu apa umenipa elimu...kumbe nchi au mtu anaweza kutaka tu kukopa ata kama pesa anazo za kufanya ilo jambo. Alafu anakopa kwa masharti na ribs juu...Ahsante kwa Elimu hii
 
Vibaraka wameaibika..haha.

Mungu Ibariki Tanzania.
 
.. katika sakata hili Zitto ametoka kidedea. Maoni na mapendekezo yake yamezingatiwa.

..gazeti la mwananchi wameripoti kuwa fedha hazitatoka mpaka 2021.

..pia kutakuwa na ukaguzi wa WB ktk matumizi ya fedha hizo.

..vilevile hazitoki zote kwa wakati mmoja. Maana yake ni kwamba tukiharibu hapo katikati zinaweza kusitishwa.

..lingine ni kwamba huu ni MKOPO. Ni jambo la fedheha kununua ndege zinazotutia hasara halafu tunakwenda kukopa kwa ajili ya elimu.

Cc Chige
Na kimsingi, kwa sasa hakuna uhakika wa 100% kwamba mkopo utatolewa kwa sababu serikali wana kibarua kingine cha kufanya, na wakikamilisha na kuwa approved na WB, ndipo mkupuo wa kwanza utatoka kwenye FY 2021.

Sehemu ya 10 ya masharti ya mkopo inasema:-
10. When will funds for SEQUIP be disbursed?
No disbursements will be made under the project until it is declared effective. It can only become effective when a detailed Project Operations Manual (POM) is prepared by the government and is reviewed and cleared by the World Bank
Kwa kifungu hicho hapo juu utaona wazi kwamba suala la mkopo kutoka hata kwa hiyo awamu ya kwanza, bado ni conditional.

Kwahiyo serikali wakiandaa POM ambayo haijafikia viwango vya SEQUIP hapo POM yao itarudishwa na kuambiwa waifanyie marekebisho tena na tena hadi itakapokidhi! Which means, awamu ya kwanza inaweza kutolewa kwenye FY 2021 au inaweza ikatolewa kwenye FY zinazofuta kutegemea na POM itakuwa cleared lini!

Na ndo hapo sasa kama ulivyo-conclude... tunafanya investment kwenye biashara kichaa ya ndege wakati hata uwezo wa kuboresha elimu yetu, hatuna!
 
It gives pregnant girls, young mothers, and other vulnerable children who leave school early the possibility to return to the formal system and complete their education.
Hapa sikubaliani nao kabisaa. Ni ujinga.
 
Egnecious,
Huna haja ya kukuza mambo, kumbeza mtu mmoja na kumtukuza mwingine! Almost kilichofanyika ndicho kilikua kilio cha wanaharakati wote kwamba ni lazima yafanyike maboresho ili watoto waliokatiza masomo wapate fursa ya kuendelea na masomo.

Kama umeielewa hiyo article bila shaka utagundua kua mapungufu yaliyopigiwa kelele yameboreshwa. Tusipende kua bendera fuata upepo!
Na kimsingi hayo maboresho yalishafanyika bali Magufuli ndie alitaka kufanya mambo tofauti na na mwongozo wa wizara uliotolewa tangia 2009.

Mwaka 2009, serikali kupitia Wizara ya Eimu walishatoa mwongozo wa namna gani watoto waliopata ujauzito wataendelea na shule.

Mwongozo unasema wazi kwamba, ikiwa mtoto atapata ujauzito basi mzazi au mlezi amuelimishe na kumshawishi kurudi aendelee na masomo mara akishajifungua!

Endapo binti atakataa katakata, ndipo linakuja suala la alternative education.

Kinyume chake, Magu akafanya suala la alternative education ndio njia pekee lakini sio kuendelea na elimu ya sekondari!

Na mwongozo pia unatoa maelekezo kwa serikali kuhakikisha hao watoto wanaendelea na elimu rasmi kama kawaida. Ni kutokana na hilo ndio maana WB wamesema wazi kwamba hakuna sera yoyote inayokataza watoto waliopata ujauzito wasiendelee na shule... ni kwa sababu ya huo mwongozo wa 2009.
 
Chige,
Tangu lini zito akajali masikini ww? Hicho ni kiini macho na siasa za maji taka! Zito aliwajali acasia na wenzie!
Pole sana, mwongozo wa 2009 haukuandaliwa na Ziito!!
Na ustake kutuaminisha mimba wanabeba watoto wa maskini! Na pointi hapa ni kuzuia mimba hizo za utotoni zisitokee!
Tatizo huelewi! Nimeshasema mara kadhaa wote wanapata mimba lakini wanaoathirika ni watoto wa maskini kwa sababu wale wenye uwezo hata wakipata mimba wanaendelea na masomo hata kama ikibidi kwenda Ulaya kusoma... watasoma!

The problem tatizo kama hilo likija kwa mtoto maskini ambae hana option zaidi ya shule za serikali!!

Na hoja nyingine ni kwamba, hata hao watoto wa wenye nazo wakipata ujauzito bado wana uwezekano mkubwa sana wazazi wake wakachoropoa ujauzito na mtoto akaendelea na masomo tofauti na mtoto wa maskini!!

Usichoelewa hapo nini?!

Na kwa kiasi kikubwa sheria zetu ziliwatisha watoto waliokuwa wakijitambua kutoshiriki mapenzi kwa kuhofia kukatiza ndoto zao za kufikia malengo yao kiuchumi!
Mtoto anayejitambua hawezi kupata mimba hata kama anafanya mapenzi, na ndio maana mimba nyingi zipo primary hadi somewhere kidato cha pili kwa sababu bado wanakuwa wadogo wasiolewa lolote!

Watoto wa A-Level wanagongwa kama kawaida lakini ni nadra sana kusikia wamepata ujauzito kwa sababu tayari wanajitambua!!
Wakati huohuo hazikuwatisha kivile wale watoto mbulula wasiojitambua na wasio na malengo waliojipangia kuamua kufupisha safari!
Serikali ni ya wote... vichaa, vilaza, majuha, wendawazimu, wezi, watakatifu, n.k!

Ni kutokana na ukweli huo, jambazi anaweza kufika mahali na kufanya tukio kiasi kwamba anaweza hata kuua watu! Ikiwa kwenye tukio hilo jambazi atajeruhiwa na kukimbizwa hospitali, bado hakuna atakayesema mtu kama huyu hawezi kutibiwa hospitali ya serikali kwa sababu ni mhalifu na muuaji!

Sasa ikiwa hata washenzi kama hao tu wanahudumiwa na serikali, how come mnapinga privilege kama hiyo kupata an innocent child?! Hivi nyie ni watu wa aina gani?!

Narudia hapa kusema ingawaje mwanzoni mlisema "it doesn't matter"! Nyie watetezi wa Magu na serikali hamna hoja ya maana zaidi ya kutokubali kwamba Magu kakurupuka na hatimae kaufyata!

Mlivyo watu wa ajabu endapo Magu huyo huyo angekuwa in favor na hao watoto, pia mngemuunga mkono!!
Pia kuna wazazi ambao wao waliwashawishi watoto wao kutoendelea na masomo na badala yake waolewe!
Hao wanaoshawishiwa ni watoto wa primary, na ndio mara kwa mara tumekuwa tukisikia wakishawishiwa hata mitihani yao vibaya ili wasifaulu!

Na hawa wakishawishiwa, wengine wanakubali kwa sababu ile ile... bado ni watoto na hawana uwezo wa ku-digest mambo! So, hatuwezi kumhumu mtoto hapa wakati yeye ni victim tu!!
Kijumlisha na matukio ya ubakaji wa kibabe, Sceneria zote hizi ndio zilipelekea idadi hiyo ambayo kimsingi ni ndogo ya watoto kuwa wazazi!
Ubakaji ni ubakaji... so longo mtoto hajafikisha 18, hakuna suala la kukubali mwenyewe hapo, bali anakuwa amebakwa!

Na kwahiyo, hao watoto wanakuwa wamebakwa... sasa how come ahukumiwe wakati kabakwa?! Kwa maana kafanya jambo bila ridhaa yake?
Huo muongozo japokuwa ni wa 2009, haujawa 'implemented' kwa kuwa unapingana na all norms za kitz! Hauna mantiki, na hata walioupitisha tungetamani kuwajua!
Norms zinazokiukwa?! Miafrika ndo inaongoza kwa mambo ya hovyo hovyo na ya kipumbavu!! Miafrika ndo inaongoza kwa kupenda ngono! Miafrka ndo ina tabia za kutembea au hata kuoa watoto wadogo! Sasa hizo norms zinazokiukwa ni zipi?!
Hao wanaolazimisha wazazi wasome darasa moja na watoto! Ili iweje?
Kamuulize JPM, ili iweje anakubali wazazi wasome darasa moja na watoto!!

Halafu nyie watu hoja zenu ni za hovyo sijapata kuona!!

Serikali hiyo hiyo mnayoitetea, na si ajabu hata wenyewe, majority kama sio wote mnakubaliana mtoto akipata ujauzito asisome shule za serikali, lakini ana ruhusa ya kusoma shule binafsi!

Sasa kwani hao watoto mnaoogopa kusoma na wazi wapo shule za serikali peke yake na shule binafsi wanaosoma ni watu wazima au wazazi?!

Kama hoja yenu ni kwamba si vizuri mzazi kusoma na watoto, kwanini basi waruhusiwe kusoma shule binafsi?!

Na kama mnaamini wazazi wakisoma na watoto ( shule za serikali) hawa watoto wengine watawaharibiwa, kwanini basi mnataka wakawaharibu watoto wanaosoma shule binafsi?!

Nyie watu mbona hoja yenu haiweleweki?!
Huyu mzazi hata network yake inakuwa imebadirika, akimuwaza mwanae, mapenzi ya baba mtoto, na hata kuwazia makuzi ya mwanae ambae atakuja kumuona babae miaka 30 ijayo!
Kwahiyo akienda kusoma shule za binafsi mnakosema wanaweza kwenda huko, network zao ndo zitasoma sawasawa?!
 
FYI, huwa siandiki mambo kwa hisia kama mfanyavyo wengine especially watetezi wa mfumo! Kwamba ni "utamaduni wa Kitanzania" maana yake nini?! Taifa haliendeshwi kwa tamaduni bali kwa misingi iliyojiwekea!!

Tafuta online, au nenda pale Wizara ya Elimu waombe document titled:
Huo ni muongozo wa serikali kupitia Wizara ya Elimu ambao ulitolewa April 2009. Section 2.3 ya muongozo inatoa maelekezo kwa wazazi/walezi kwamba:-
  • Shall be counseled and guided by the school leadership on the pregnancy of the school girl;
  • Shall show empathy and accept to take care of the pregnant girl;
  • Shall be guided and counseled by the school leadership concerning maternal health of the pregnant schoolgirl;
  • Shall be informed and required to fulfill re-admittance requirements;
  • Shall be required to update the school leadership on the health condition during pregnancy and after birth; and
  • Shall be involved in deciding on which mode of education (Formal or informal) and school the pregnant girl would like to continue with, after giving birth.
Aidha, section 2.6 ya Muongozo unatoa maelekezo kwa serikali kwamba:-
  • Shall educate and sensitize the society/community on the importance of readmitting impregnated school girls;
  • Shall educate and sensitize the society/community on the process of readmitting impregnated school girls; and
  • Shall empower school leadership on the issue of readmission of pregnant school girls; and
  • Shall task the ward social welfare officers to monitor the health welfare of the impregnated school girls.
Huo ndio MWONGOZO halali ambao Magufuli anaukanyaga! Sasa wewe niwekee hapa huo utamaduni unaosema kwamba watoto wa kike wakipata ujauzito, ni marufu kuendelea na elimu rasmi kwa shule za serikali!!!
Kwanini uwatishe badala ya kuweka mikakati inayoeleweka kuhakikisha hakuna ujauzito?! Hivi unaweza kunieleza hapa serikali ina mkakati upi kuhakikisha watoto hawafanyi ngono za mapema au angalau hizo ngono salama?

Btw, kama kuwatisha mbona mimba bado zipo pale pale hata siku hizi ambapo watoto wanaanza shule mapema sana?
Unamaanisha Wizara ya Elimu hawana akili timamu, au?!

Ukweli ni kwamba, kama nilivyowahi kusema kwenye post moja wapo hapa jamvini, Mh. JPM ni mkurupukaji, na wala hafahamu misingi ya serikali mwenyewe!!

Hapa JPM alikuwa kama wewe tu kwa kuamini "kutimua shule wanaopata ujauzito ni utamaduni wetu" bila kufahamu mwaka 2009 serikali kupitia wizara ilitengeneza utaratibu wa kuhakikisha watoto wanopata ujauzito hawafukuzwi, bali wanakuwa suspended na kurudi tena shuleni unless kama ataamu mwenyewe kuendelea kwenye mfumo usio rasmi ambao Magufuli na wafuasi wake wanadhani ndo sheria inavyosema!Hoja ya Zitto kivipi?! Kwani Zitto anafanya kazi Wizara ya Elimu au alihusika kwenye kuandaa huo muongozo?

Btw, Wakopeshaji gani waliodharau hoja ya Zitto?! Hivi umesoma maelezo ya WB au unaongea tu?!

Kipengele kimoja cha taarifa ya World Bank kinasema:-Hiyo ndo kauli ya WB ambayo inaakisi sehemu ya mwongozo wa serikali nilioweka hapo juu!

Kwa maana nyingine, suala la wanafunzi kutimuliwa sio la kisera bali ni la JPM na watu wake!!!

Sehemu nyingine ya taarifa hiyo ya WB inasema:-Sasa wewe habari kwamba WB wamempuuza Zitto umezitoa wapi?!

Na labda nikujuze lingine! WB hawatatoa fungu lote kwa pamoja bali watatoa kwa awamu baada ya kuhakikisha serikali inatekeleza masharti waliyopewa, including kuwaacha watoto wajawazito kuendelea na shule kama mwongozo wa wizara unavyosema:-
Of the project funds, 96 percent (US$480 million) are subject to (a) achievement of agreed results verified by an Independent Verification Agent subject to the World Bank’s approval; and (b) submission of evidence that the government has already spent an equivalent amount on eligible expenditures in the secondary education sector. Assuming that these conditions are met each year, the disbursement schedule, is as follows:
  • FY 2021 - US$72.47 million
  • FY 2022 - US$101.10 million
  • FY 2023 - US$114.73 million
  • FY 2024 - US$98.52 million
  • FY 2025 - US$85.37 million
  • FY 2026 - US$27.81 million
Na sio tu kwamba serikali watakuwa wanasema "tumetekeleza kwa kiwango fulani bali hadi pale Independent Verification Agent atakapothibitisha!!!Eti mmesikia wenyewe, achana na hao wengine; niambie wewe ulimsikia wapi kama sio unatumia nukuu za propaganda za Lumumba!!

Ambacho alisema Tundu Lissu, ni hiki hapa chini:-



Hiyo video ni ya dakika 3:43 lakini MATAGA kwa kujua Wa-TZ hamna utamaduni wa kutafuta ukweli, waka wanaongelea maeleo ya dakika 2 za mwanzo na wakawaficha zaidi ya dakika 1 unusu nyingine zilizobaki!

Sasa pamoja na kunitolea povu kwamba eti nimetumwa kuandika uzushi, kwa mwenye akili timamu hapa atajua ni nani aliyetumwa kuleta uzushi kati yangu na wewe! Yote niliyosema hapo kabla nimekuwekea ushahidi, weka hapa ushahidi wa maelezo yako!!!
Mkuu @Chige,tulikosa nondo zako jukwaani. Ubarikiwe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lakini msimamo wa serikali si upo pale pale? Ukipata mimba altenative program ni veta au kajifunze kijiweni charahani. Kwa mantiki hii aliyeabika ni yule aliyaekurupuka kupinga pesa za mkopo zisitolewe.
Umeelewa kilichoandikwa kwenye barua ya WB!?
Nenda kwa Ras Simba tafadhali,halafu ndio urudi kujadili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom