World Cup 2010 SA: Match updates (From June 11)

Mpaka sasa sijaona timu ya kutwaa ubingwa hapa..Labda tuone Oranje, Brazil na Spain watatuonesha potential gani.

Ujue hizi ni mechi za mwanzo tu kadri mashindano yanavyoendelea baadhi ya timu zinaweza kuongeza kiwango chao cha uchezaji na hata ufungaji wa magoli. Pamoja na matokeo ya leo bado Argentina ni moja ya timu ambazo zinapewa nafasi kubwa kuutwaa ubingwa. Na hizi ni mechi nne tu bado kuna mechi nyingi tu katika raundi ya hii ya kwanza.
 
BTW: Where's Zidane nowadays mkuu?

'On 1 June 2009, Zidane was announced as the Advisor to the President as Florentino Perez was named President of Real Madrid for the second time. He also regularly plays for Real Madrid Veterans team.[20] He along with Jorge Valdano, General Director, and Miguel Pardeza, Sporting Director, will be the key decision makers on the sporting side of the club. Zidane has also made several futsal appearances since his retirement.'
 
Mpaka sasa sijaona timu ya kutwaa ubingwa hapa..Labda tuone Oranje, Brazil na Spain watatuonesha potential gani.

Kweli kabisa Mpemba........Hawa Argentina nao wabovu tu kama France........Nigeria wamecheza vizuri sana dakika 25 za mwisho haa baada ya kuingia Peter na Obafemi...Argentina wachovu tu.........Ngoja tuwaangalie Orange,Spain na Brazil.........Na kwa mbaaaaaaaaaali Portugal na England...........

Mpemba...Unaizunguziaje game ya England na US....Mie naona kaa US wanashinda vile
 
Ngosha,

Timu zote mbili haziwezi kukaa na mpira, hivo tunaona mpambano chapwa pengine likipatikana goli la mapema. Nashindwa kutabri kwa kweli.

Kuhusu muelekeo wa ubingwa bana, hapa ninavoona timu ambayo itakuwa na tactics ndio itakayoshinda hili kombe. Unaeza kushangaa mzee Lippi akaja na nati zake, mambo yakajirudia. France na Argentina ni walewale tu, no excuse hawana mbinu na gemu ya leo wangeweza hata kupoteza wangekutana na timu yenye tactics. Watu wanasahau hii ni cup final, no second chance, usipofanya vizuri mechi za kwanza mechi zinazokuja ndio znakuwa ngumu zaidi, na tension zaidi. Kwene kutoana huko ni tactics tu ndio zinakutoa, ukileta mambo ya pasi 20 kabla ya goli unaeza kutolewa tu na katimu kenye possession 20%.
 
Nafikiri Enyama alikuwa amepewa maelekezo vizuri jinsi mguu wa kushoto wa messi anavyoutumia na mipira yake inavyokwenda.

Yeah.........Enyeama kacheza vizuri sana leo,kaokoa magoli mengi sana............Huyu na yule kipa wa Bafana Bafana Khune wamejitahidi sana kwenye mechi zao hizi za kwanza
 
haya wale big allies kwenye mambo fulani leo for at least 90mins watapambana kufa na kupona,nategemea ushindi mnono kwa ENGLAND,3-1.
 
USA wanashinda leo bana....England wachezea kichapo aisee
 
green,johnson,terry,king,cole,gerrard,lampard,milner,lenon,rooney,heskey.......hio ndio timu ya leo ya england....hii naona imekaa ki-mbiombio tu tutegemee very high pace game
 
nashukuru kusikia unatabiri/unataka usa ishinde....maana yake watafungwa kwa rekodi yako nzuri....lol
Ndio nakwambia mimi, kuna thread nyingi tu........akiniruhusu naweza weka hapa timu alizotabili lakini ikawa kinyume.....achilia ile ya stars na Brazil, ambayo alitabili....alijitaidi kwelikweli....sorry Balantanda
 
Yaani mpaka sasa sijaona skills zinazoitwa

1. Lelastica
2. El regart
3. La bicicreta
4. De spero
5. Estil Laudrup
6. Lespardinha
7. El Barret
8. El triple Barret
9. La vaselina
Nk nk nk nk nk nk....

ndio muamini sasa
No Gaucho
No Football.
 
.......USA watapata kichapo tu leo, England wapo juu kwa soccer.
 
.......USA watapata kichapo tu leo, England wapo juu kwa soccer.

ha ha ha England tatizo lao hawaeleweki wana uzembe uzembe fulani kwenye kukaba. USA ni timu ambayo inacheza kwa kujituma sana na wame-improve sana lately.

ngumu kuitabiri kidogo i will call for a draw.
 
Mechi itakuwa ngumu kwa timu zote, tusubiri mchezo mzuri!
 
Come on USA funga hawa metartarsal boys sijui leo kama Rooney atatoka khe khe khe ati Right Phillips na vikongwe kibao onyesha soka la uhakika England wafungashe makabrasha baada ya raundi ya kwanza.

Mpira wa England uko juu kwenye vyombo vya habari siyo kimchezo ngoja wakamuliwe leo na togwa inywewe.
 
green,johnson,terry,king,cole,gerrard,lampard,milner,lenon,rooney,heskey.......hio ndio timu ya leo ya england....hii naona imekaa ki-mbiombio tu tutegemee very high pace game

Lenon nadhani kama kasharudi kuwa 100% fit atakuwa mwiba sana kwa USA kwenye swala la pace.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…