World Cup 2010 SA: Match updates (From June 11)

World Cup 2010 SA: Match updates (From June 11)

Ghana made us happy & sad as well. Kilichotokea kwa A.Gyan ni bahati mbaya zaidi kuliko makosa ya kibinadam, any body angeweza kukosea, Ghana hawakuwa na bahati zaidi jana kwa kweli, bendera ya nchi yao na Africa kwa ujumla imepeperushwa vema.

BWT, Hivi hawa FIFA kwa nini wasiweke sheria kwamba, kama mchezaji akizuia mpira ambao unaelekea golini na hakuna uwezekano kwamba goal keeper anangeweza kuuzuia liwe goli mmoja kwa moja kuliko kutoa adhabu ya penalty? Ghana jana wamenyang'anywa ushindi kwa mchezaji wa Uruguay kuurudisha mpira uliokuwa unaenda golini kwa mikono miwili, lile lilikuwa ni goli moja kwa moja! FIFA need to review their sherias kwa kweli!
 
Nawapongeza sana wanaGhana kwa kuionyesha dunia kuwa Africa inaweza soka.

Hongera nyingi kwa Gyan, kijana mwenye kujituma. Kujikwaa si kuanguka kijana.
 
Yule refa naye hatosahulika na Afrika kwa kushindwa kutambua kuw lile lilikuwa goli la wazi kwani yule Mruguway aliuzuia mpira ndani goli.

Jana nilisikitika sana na leo sijatamani hata kusoma gazeti kwenye kurasa za michezo. It was our time to win but referee twisted us
 
Nakunaliana na Next Level kwa kweli. Sheria hii ibadilishwe. Mtu karudisha kwa mikono mpira uelekeao golini kabisa. Kumpa red haitoshi! Lihesabike ni goli kabsaa na hii itawafanya wachezaji kutokunawa mpira hovyo.
Du nilikufa ganzi kabisaaaaaaaa.
 
Siku zote football ni mchezo wa maumivu makali. Pale ambapo watu mnategemea kufurahi ndipo hapo mambo huwa kinyume. Asamoga G. ni mpigaji penati mzuri sana na ndio maana hata kocha wake alimuamini kwa mara nyingine kuanza kupiga penati tena baada ya muda wa dakika 120....Nadhani kwa mtazamo wangu kilichompata Asamoah ni exitement ya kuweka historia katika soka la Afrika so na umakini ulitoweka maana hakuweza hata kuvuta na kushusha pumzi kuonyesha kuwa mwili na akili yake viko pamoja nae...Ni bahati mbaya na ndivyo soka ilivyo lakini wameonyesha kuwa wanaweza na Uruguay licha kuingia semi-final kazi wameifanya!!
 
Mimi nafikiri ni kwamba Africa haitamsahau Suarez, kama huyu asingedaka mpira ni wazi lile lingekuwa goal na kulikuwa hakuna haja ya penalty wala nini ambayo ni pressure.

Ila Uruguay kwao huyu ni hero na walimbeba juu juu kuliko hata goalkeeper aliyeokoa mikwaju ya penalty
376,http%3A%2F%2Fa323.yahoofs.com%2Fymg%2Farmchair_pundit%2Farmchair_pundit-579727046-1278111923.jpg%3FymzSAZDDak4lKfOu
 
Ama kweli kisicho ridhiki hakiliki. Mie bado nimekufa ganzi hadi sasa. Nipo kazini lakini duh nimeshafanya makosa katika kazi zangu za leo! Loh!!!
 
1. Refa alichezesha haki tupu na kidogo aliwapenda waghana,amini usiamiamini.
2. Sheria namba kumi inaeleza wazi kuwa ili goli lihesabike ni goli ni lazima mpira wote uvuke msitari wa goli ardhini katikati ya nguzo za goli, au hewani na usisindikizwe na mkono isipokuwa wa golikipa.
3.ghana waliutaka sana ushindi ule,ule mpira ulioolekea golini kudakwa uliwamaliza nguvu kabisa,katika hali kama hiyo utapiga penati kweli?....ndio maana wawili walikosa na golikipa hakuzuia mkwaju wowote,walishaathirika kisaikolojia.na ndio maana hata ile penati ya mwanzo walikosa. Red card na penati ni uamuzi sahihi kabisa

hayo ni maoni yangu.
 
Leo ndio tutaona kama Maradona ni kocha kweli wa kuweza kukabiliana na challenges za ukocha.
 
Klorokwini hujui kukosea...... Naona ujerumani imeanza kunifurahisha mapema sana
 
yule refa naye hatosahulika na afrika kwa kushindwa kutambua kuw lile lilikuwa goli la wazi kwani yule mruguway aliuzuia mpira ndani goli.

Jana nilisikitika sana na leo sijatamani hata kusoma gazeti kwenye kurasa za michezo. It was our time to win but referee twisted us
pole waafrica wote hatukupenda ghana ifungwe, refa alichezesha haki kwa mujibu wa sheria 17 za mpira wa miguu.
 
Back
Top Bottom