Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Wengi tutakimbia sred hii maana imeingiliwa na watu wazima kuandikiana maneno ya kashfa!
Tupo hapa kujadili soka tu na si vinginevyo!Plese @Bwan'chuchu na @ Mourinho turudi kwenye mstari tumalizie sred hii Jimapili kwa amani kama siku zote!!
Hata mimi nashangaa hizo kashfa zimotokea wapi!
Huyu Murinyo out of nowhere katokea tu kuanza kulipuka na kashfa
Akaja na huyo Chombwa naye.......
Kosa langu liko wapi?
Mkuu yaishe haya!Tumechangia hapa mwezi mzima huu kama ndugu bila mkwaruzano!Jumapili tuagane hapa bila kununiana
Team Argentina!!Messi;Aguero;Di Maria na Higuain ni tofauti kabisa na Gustavo;Paulinhno;Fred na Bernard!
Messi and Co. hawata-capitulate kama hao masharobaro wa Brasil.
Nilikuwa naangalia clip ya Scolari na Carlos Alberto Pereira ya mkutano wao na waandishi wa habari Jumatano, Scolari kasema hajui kilichotokea hadi kikapelekea kufungwa magoli manne ndani ya dakika sita.
Hana maelezo kabisa. Halafu eti bila hata aibu anasema asilimia 70 ya kikosi hiki kitakuwepo Russia 2018!
He can't be serious. Binafsi ambao naona walau wanaweza kuwepo kwenye hicho kikosi ni Bernard na Neymar tu. Hata huyo Neymar naye nina mashaka naye maana anaonekana ni sleki sana.
Hulk tupa kule, Fred ndo kabisaaaa hafai.
Mzee Scolari kabaki kubwabwaja tu katika jitihada za kutetea kitumbua chake kisiingie mchanga. Nitashangaa sana kama bado atakuwa kocha wa Brazil katika mashindano ya Copa America 2016 yatakayofanyika USA.
Katika Ulimwengu huu wa leo kama bado unaviona vitu/mambo/watu in black and white then you are clearly misinformed, misguided and ignorant, in fact ulichokiandika kinapingana na historia.
Do your homework sonny!
Kuna any Jamiiforums member hapa Sisi kwa Sisi Bar-Mburahati?Mm ishafika hapa naanza na supu ya kongolo asubuhi hii!Njooni jamani tujadili mpira
Edson.
Akiwa na umri wa miaka 18, aliibeba brazil kuchukua kombe la dunia kwa mara ya kwanza mwaka 1958 alikuwa na umri wa mtoto wa kidato cha nne kwa TZ.
Akawabeba tena brazil wakachukua mwaka 1962.
Mwaka 1966 akalikosa.
Akawabeba tena brazil wakachukua ubingwa tena mwaka 1970.
Mara zote aliifikisha brazil at least robo fainali.
Diego.
Aliwabeba Argentina wakachukua WC mwaka 1986, waliwafunga german fainali.
Akawafikisha fainali mwaka 1990, walifungwa na german goli moja la penati, Andre Brehme alipiga hiyo penati.
Messi.
Hii ni mara ya tatu anashiriki, ana umri wa miaka 26, ameingia fainali ya kwanza ya WC mwaka huu 2014, hatujui kama Wajerumani watamwacha achukue.
Kesho baada ya game wanamfukuza hata yy Scolari analijua hilo
Mourinho unaweza nipa sababu kubwa kwa nn wadau wengi wanasema Germany atamfunga Argentina Jumapili?
Kuna any Jamiiforums member hapa Sisi kwa Sisi Bar-Mburahati?Mm ishafika hapa naanza na supu ya kongolo asubuhi hii!Njooni jamani tujadili mpira
Nikiwa kama Refa wa kujitolea humu na kwa niaba ya wanasport wote humu, ndugu Katavi popote pale ulipo tunakuomba sana tena sana USITAJE timu unayoishabikia,wewe umekuwa ni zaidi ya Mtabiri humu,hatukunyanyapai ila tunakupenda sana.
cc MEANDU BAK Malafyale Bantu lady, Victoire, Heaven on Earth, Bulldog, @BWAN'CHUCHU, adolay, s.crony mournho Skype DEMBA na wengine wote.
hapa Malafyale utakuwa umeelewa sasa!Sababu za wadau wengi sina, ninazo sababu zangu na ziko hivii;
1.Mkoloni ana kitu kinaitwa 'team' inayoanza (1st 11) na inayoanzia bench ni kitu kimoja tofauti na nchi nyingi ambazo zina 'vikosi' tu lakini hakuna 'team' kama wale waliokula wiki
2. Hii team imekaa muda mrefu pamoja na kocha mmoja ingawa kuna some few new additions, hivyo wanajuana na wanauzoefu na mechi kubwa, 2010 walifika 1/2 ya WC kule Bondeni, wakafika tena 1/2 ya Euro mwaka 2012, msimu wa 2012-2013 tumeona all germans
final kwenye Champios league na team hizi ziko dominated na wazawa. Kwa kuongezea kikosi hiki cha mkoloni kina wachezaji 6 waliokua pamoja kwenye U-20 na walichukua ubingwa wa ulaya, hivyo inaonesha kiasi gani hawa watu wanajuana
3. Wametoka katika kundi gumu na kuna mechi hawakucheza vizuri sana lakini waliyapata matokeo waliyoyahitaji, kwa maana hiyo hata match ikiwa ngumu bado wanauwezo wa kupata matokeo
4. Hakuna mchezaji pekee anayeibeba wala mwenye presha ya kuibeba Ujerumani tofauti na Argentina ambao kama tulivyoona juzi Vs Holland ukimbana Messi wanashindwa kabisa kufika kwa kipa, ukimkaba Muller yupo Kroos, ukimkaba Kroos yupo Khedira, ukimkaba huyo yupo Ozil, Goetze, Klose n.k