Sababu za wadau wengi sina, ninazo sababu zangu na ziko hivii;
1.Mkoloni ana kitu kinaitwa 'team' inayoanza (1st 11) na inayoanzia bench ni kitu kimoja tofauti na nchi nyingi ambazo zina 'vikosi' tu lakini hakuna 'team' kama wale waliokula wiki
2. Hii team imekaa muda mrefu pamoja na kocha mmoja ingawa kuna some few new additions, hivyo wanajuana na wanauzoefu na mechi kubwa, 2010 walifika 1/2 ya WC kule Bondeni, wakafika tena 1/2 ya Euro mwaka 2012, msimu wa 2012-2013 tumeona all germans
final kwenye Champios league na team hizi ziko dominated na wazawa. Kwa kuongezea kikosi hiki cha mkoloni kina wachezaji 6 waliokua pamoja kwenye U-20 na walichukua ubingwa wa ulaya, hivyo inaonesha kiasi gani hawa watu wanajuana
3. Wametoka katika kundi gumu na kuna mechi hawakucheza vizuri sana lakini waliyapata matokeo waliyoyahitaji, kwa maana hiyo hata match ikiwa ngumu bado wanauwezo wa kupata matokeo
4. Hakuna mchezaji pekee anayeibeba wala mwenye presha ya kuibeba Ujerumani tofauti na Argentina ambao kama tulivyoona juzi Vs Holland ukimbana Messi wanashindwa kabisa kufika kwa kipa, ukimkaba Muller yupo Kroos, ukimkaba Kroos yupo Khedira, ukimkaba huyo yupo Ozil, Goetze, Klose n.k