Siku ya saba ya michuano hii ilainzia mji wa Porto Alegre.
Ikaishia takriban maili 2000 kutoka hapo (naam, Brazil kubwa ati), Ambapo
Uholanzi na Chile wakapata tiketi kuingia raundi ya 16 bora na mchezo mkononi.
Hapo Australia, Spain na Cameroon ndio wameshafungashiwa
virago, huko Croatia ikiwa imeshinda vizuri kujiweka katika kinyang'anyiro cha
utatu na Brazil na Mexico kuwania tiketi mbili za kuingilia hatua ya mtoano.
Kituko cha siku kilikuwa wakati wa mchezo wa Cameroon na
Croatia ambapo katika dakika za majeruhi huku wakiwa chini kwa bao 4-0, beki wa
Cameroon Benoit Assou-Ekotto alimpiga
kichwa mchezaji mwenzie Benjamin Moukandjo (kushoto). Na hasira za kufungwa za Assou-Ekotto
ziliendelea mpaka chumba cha kuvalia baada ya kipyenga cha mwisho na kumlazimu Samuel Eto'o aingilie kati.