World Cup 2014, Brazil: June 12 - July 13

World Cup 2014, Brazil: June 12 - July 13

Safari hii mpira hautabiriki ndugu.

Kuna timu zinachezesha watoto wanawapelekesha watu wazima na ustaa wao !
 
wameshaaga hao

Hapana mkuu ile mechi ya jana FIFA wamefuta matokeo kwa Chile maana walimchezesha mcheza Ahgiluta ambaye hana uthibitisho kuwa ni raia wa Chile hivyo Spain wamepewa ushindi wa magoli matatu na point 3......Source ni Espn.
 
Mkuu kipindi kile analogy sauti ilikuwa inawahi picha inachelewa kwa hiyo alikuwa sawa tu!

hapana kwa sababu Diop hakukokota mpira kwenda kufunga, Diop alipigiwa crosspass akaslide na kuugusa mara moja tu mpira ukaingia golini. Ni mtangazaji alikuwa anampenda Diop, wakati mpira unaanza tu yeye anamuongelea Diop tu.

Angalia hii clip hakuna delay ya sauti.

https://www.youtube.com/watch?v=JigE4eC7XeI
 
World Cup Report coming up next - we look ahead to England's game tonight & assess what's next for Spain after their group stage exit
 
Hana wasiwasi akifukuzwa mitaa ya Catalan atarudi "Home" Emirates Stadium

Lol tumemtolea nje Cesc ndo tutamchukuwa Song? nilisikia mnamtaka kumreplace Fletcher. Dah kumbe hawa wala nyani na ngedere walifungwa 4 bila. Bora nililala mapema baada ya kufungwa goli la pili.
 
Kabisa mkuu, wanalilia posho tuuuu

Hongera kwa Croatia,nimeangalia marudio Dstv aiseee ni aibu bora nilivyoenda kulala!!,vipi naomba ufafanuzi niliona kipande kama wachezaji wa cameroon wenyewe kwa wenyewe wanagombana ilitokea nini????
 
Africa ni kichwa cha mwendawazimu...yaani timu zote shiriki inayoleta matumaini ni ivory costs tuu..

huu ni ushenzi sanaa...ndoo mana mechi ya cameroon jana saikutaka hata kupoteza usingizi wangu...nyambafu zao...

Hivi taifa stars ndo tulikuwa tunang'ang'ania kushiriki si ingekuwa historia ya magoli kuwahi kutokea
 
Siku ya saba ya michuano hii ilainzia mji wa Porto Alegre.
Ikaishia takriban maili 2000 kutoka hapo (naam, Brazil kubwa ati), Ambapo
Uholanzi na Chile wakapata tiketi kuingia raundi ya 16 bora na mchezo mkononi.


Hapo Australia, Spain na Cameroon ndio wameshafungashiwa
virago, huko Croatia ikiwa imeshinda vizuri kujiweka katika kinyang'anyiro cha
utatu na Brazil na Mexico kuwania tiketi mbili za kuingilia hatua ya mtoano.


Kituko cha siku kilikuwa wakati wa mchezo wa Cameroon na
Croatia ambapo katika dakika za majeruhi huku wakiwa chini kwa bao 4-0, beki wa
Cameroon Benoit Assou-Ekotto alimpiga
kichwa mchezaji mwenzie Benjamin Moukandjo (kushoto). Na hasira za kufungwa za Assou-Ekotto
ziliendelea mpaka chumba cha kuvalia baada ya kipyenga cha mwisho na kumlazimu Samuel Eto'o aingilie kati.
 
article-2661968-1EE7BFC200000578-250_634x373.jpg
 
Back
Top Bottom