World Cup 2014, Brazil: June 12 - July 13

Italian tactician, wametudisapoint sana Mabuluda. Kwenye mashindano haya italy ilikuwa na makocha wa3.
1. Alberto Zaccherron akiwanoa Japani.
2. Fabio Capello akiwa na Russia na
3. Cecerra Pradelli akiwa na Italia. Wote wametoka patupu. Wameshindwa hata kuqualify kwenda knock out stage, hii inaonyesha wale makocha wa aina ya Lippi, Sacchi ni adimu pale italy, kwa timu yao ya taifa.

Cc: juve2012, Mourinho, Gang Chomba
 
Last edited by a moderator:


Mtoa uzi ni mtu ambaye hajui mpira; ila ni mshabiki wa matokeo tu. Kwa nini asijadili kuporomoka kwa soka la Ulaya?
England, Spain, Portugal wote wametoka raundi ya kwanza...

Huu ni uchambuzi wa kitoto sana. Hasa ukizingatia JF HOME OF GREAT THINKERS.
 


nakuunga mkono.
 
kwani AFRIKA ilipeleka nchi mbili tu kombe la dunia?


Swali: kuhusu kuonea si jambo geni. sema wewe hujui mpira hata nikikuambia kitu huwezi kuelewa.
Hujui kwamba kwenye mpira kuna fitina, kwa nini FIFA wanalaumiwa hata na nchi za Ulaya; WEWE hujui kitu aisee!
 

Ambapo sisi tunategemea mafanikio yaje km "uyoga"...bila kuwekeza,bila juhudi zozote....always politic tu hata kwenye masuala yanayohitaji mikakati muhimu....tutabaki kuwa si "kichwa cha mwandawazimu" bali mwandawazimu mwenyewe!
 
Na jinsi league inavyozidi kushamiri na football kuwa mchezo unaoanza kutoa ushindani mkubwa kwa American Football na Baseball si muda mrefu ujao USA itakuwa ni moja ya timu za kuogopewa duniani.

USA wanauzalendo fulani ambao nchi nyingi haina. Wako real ikifika kwenye jambo linalohusisha nchi yao
 
Reactions: BAK

Hii timu yao ikivuka hapa ilipo na kufika robo fainali watakuja mashabiki wengi sana wa USA, ikifika finals ndio hadi raisi wao atakuja kabisa
 
Siwezi kusema ni ubaguzi au nini. Nawaachia wenyewe na maamuzi na mapendezeo yao, labda wanataka wabebe au wafanye vizuri kwa England born players.
England wanaojua mpira ni weusi weng wao na sio wazungu na waache kuwasifia sana kina rooney mpka wanajihis ni wa maana sana wakati hata hafikii kiwango cha Balotel. Wajifunze kwa Holland na France au USA na Brasil.
 
South America kati ya timu nane saba zimevuka sawa na 87%, Europe kati ya team 12, 6 zimevuka sawa na 50%, Africa kati ya team 5, 2 zimevuka 40%, Asio hakuna iliovuka , Soth America USA kavuka..... kama ntakua sijakosea ..
 
Europe:germany,Belgium,Greece, Switzerland,Holland na France. South america:Brazil, Argentina, Uruguay, Chile, Colombia. North America: USA, Mexico, Costa Rica. Africa:Nigeria na Algeria
 
irigi ni mkenya aliyechukua uraia wa ubelijiji



Uraia haukotwi.....mimi ni mtanzania ila mwanangu wa kwanza ni muingereza because nilitaka azaliwe kule na apewe uraia wa kule kwa manufaa yake ya baadaye. Ni chaguo la mtu kuchukua uraia unaotaka kutoka kwa nchi uliyo zaliwa ama ya wazazi wako. Origi ametaka kuwa mbelgiji kwa sababu amezaliwa na kukulia ubelgiji. Hizi hapa ni facts zake hatusimuliwi story za dala dala hapa.

[TABLE="class: profilheader, width: 0"]
[TR="bgcolor: #FFFFFF"]
[TH="bgcolor: #FFFFFF, align: left"]Date of birth:[/TH]
[TD="class: wsnw, align: left"]Apr 18, 1995 in Oostende [/TD]
[/TR]
[TR="bgcolor: #FFFFFF"]
[TH="bgcolor: #FFFFFF, align: left"]Age:[/TH]
[TD="align: left"]19[/TD]
[/TR]
[TR="bgcolor: #FFFFFF"]
[TH="bgcolor: #FFFFFF, align: left"]Nationality:[/TH]
[TD="align: left"] Belgium[/TD]
[/TR]
[TR="bgcolor: #FFFFFF"]
[TH="bgcolor: #FFFFFF, align: left"]Height:[/TH]
[TD="align: left"]1,85 m[/TD]
[/TR]
[TR="bgcolor: #FFFFFF"]
[TH="bgcolor: #FFFFFF, align: left"]In the team since:[/TH]
[TD="align: left"]Jul 1, 2013[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Source: Divock Origi - player profile - Transfermarkt
 

Mimi namkubali kabisa kuwa ana uwezo mkubwa na juhudi binafsi ila tatizo ndiyo hilo mjivuni sana na ni bora wametolewa yaani angetamba hata kamera angepasua, mwenzake Messi huyoooo anapepea ndani ya pipa la 16 bora wakati yeye mjivuni anakwea pipa la kurudi ureno akakae kwenye kideo akimkodolea mwenzake akifanya mavitu kwa ustadi na nidhamu na heshima ya hali ya juu.
 
wataiga kung'atana au


Kwa wachezaji wa kibongo wasivyo na akili wao wanaona dili. Utaona tu mtu anamn'gata refa au mchezaji mwenzake ili tu aandikwe gazetini kesho yake na kutangazwa redioni. Au utaona mchezaji muislam anaingia uwanjani kuchukua nafasi ya fulani kisha anaonyesha/piga ishara ya msalaba. Hii ilinishangaza sana kwani nilishaonaga uwanja wa taifa. Yaani wachezaji wetu kwa kweli wachovu sana kama wasanii wa bongo fleva, yaani mtu akiona kitu tu kwenye TV basi atataka kuiga hata kama hakina maana kwake na jamii, ili mradi tu.
 
Ile staılı ya Cr7 ya kunyoa ıtaıgwa saana katıka VPL


Mpira wa Tanzania ni mpira wa kijinga sana. Chuja wachezaji wote wazalendo Simba na Yanga utakuta wachezaji wenye vipaji kweli labda ni wawili tu wengine wote ni wasanii/wachawi na ndiyo maana wanacheza mpira usio na formation ila wao tu ndiyo wanaona kuwa wana formation. Mimi bado nashangazwa na maximo kuja kufundisha Yanga wakati yeye mwenyewe aliwahi kutamka mpira wa Yanga na Simba si mpira ni ubabe tu kwani hauna msisimko na vipaji kama timu za mikoani. Lakini kwa kuwa ametaka pesa yote kasahau.
 
Wc 2014, leo saa 1:00 ni timu gani zinakutana ???

Naomba mnijuze wenye ratiba.
 
Kumbe wewe huwa huangalii mpira:
Ghana wamefunga magoli 4 kwenye kombe la Dunia mwaka huu; Wafungaji wa magoli hayo ni:
1.Asamoah Gyan = 2.
2. Andre 'Dede' Ayew = 2.

Niambie sub gani aliyeingia na kufunga goli. Acha uzushi wewe.

Kuhusu timu za AFRIKA kutolewa; si ajabu hata za ULAYA zimetolewa, tena nyingi tu.
1.England
2.Bosnia
3.Italia
4.Urusi
5.Ureno
6.Hispania





 
South America kati ya timu nane saba zimevuka sawa na 87%, Europe kati ya team 12, 6 zimevuka sawa na 50%, Africa kati ya team 5, 2 zimevuka 40%, Asio hakuna iliovuka , Soth America USA kavuka..... kama ntakua sijakosea ..

Mkuu hapo red fanya marekebisho. South america wana timu 6.
1. Brazil (host)
2. Argentina
3. Uruguay
4. Colombia
5. Chile
6. Ecuador. kule north zipo 4. Mexico, USA, Costa rica, na Honduras.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…