1.5Ivory coast
Watu wengi walilaumu ile penati lakini ukiangalia utaona matatizo mengi ya ivory cost mfano
-kwenye mechi zote tatu za makundi mid field walifanya makosa yale yale ya kupoteza mpira eneo la hatari na kufungwa na hakuna marekebisho yaliyofanyika.
-walikuja na mtindo wao ule ule wa kuacha kucheza kitimu na kila mmoja kutumia uwezo wake mfano ulikua ukiona uchoyo wa kutoa pasi wa gervinho na kalou.
-kupanga majina na kuacha watu wenye uwezo, wachezaji kama drogba, zokora na hata kalou kiwango kimeisha lakini wakawa wanawapanga tu, lakini wakaacha kuwangepanga wachezaji kama bony, ambao wangecheza na vijana wenzao wenye njaa ya mafanikio kama sergi aurier au didier Ya konan tungeweza kuona mafanikio.
2.Ghana
-ukiangalia ghana nao ni matatizo yale yale ya kwanza kupanga majina, ukiangalia mchezaji kama gyan asamoh huwa anakosa magoli mengi ya wazi ambayo midfield ya ghana huwa inayatengeneza lakini anapagwa tu na hata substution hafanyiwi na mara nyingi unakuta wanaocheza dakika chache kama ayew brother ndo wanakuja kufunga magoli
-siasa kwenye mpira, ukiangalia mechi ya mwisho walikuwa washawatimua muntari na prince-boateng ila ugomvi mkubwa ni masuala ya posho na kuhudumia timu, maana inasemekana wachezaji wa ghana walikuwa wanadai posho ya dola milioni 2 ambayo ni kama yale mambo ya cameroon
Sasa haya mambo yanakuwa yakijirudia worldcup zote lakini sisi waafrica tunasema tunaonewa tunaonewa nini na wakati timu zetu zimejaa mambo niliyoyaeleza hapo juu, watu wengine wanalaumu lile tukio la suarez kunawa mpira south, ivi kwa mfano ingekuwa ni taifa star inacheza wewe ni beki unaona kabisa mpira unaingia nyavuni ungeuacha kwa sababu ya fair play kuliko kurisk penati..?nilimsikia issa hayatou akisema wanataka timu kutoka africa ziongezwe nikajiuliza kuna haja kweli kama hizo zilizopo zenye CAF wanashidwa kuzisimamia na kutoa ushauri..!
NB: Modes naomba msiunganishe huu uzi ili tuweze kuchambua mambo kwa mtazamo mwingine