World Cup 2014, Brazil: June 12 - July 13

Utakuwa mbaguzi wa rangi wewe.
Hapana, ila najiona kama nitakua naendeleza ile dhana "Mzungu anaweza kila kitu" wakati muda huo ushapita. Istoshe, hili ni kombe la Dunia (linahusisha mabara yote) Kwahiyo najiona mwehu kumshangilia mzungu (asie nihusu) wakati waa_Africa wenzangu wapo. Labda ingekua URO.
 
Jamani leo naamka saa kumi usiku kwa ajili yenu,sasa msiniangushe wapigeni hao Wajapan.
 
Hata mimi ni mpenzi wa Soccer la ulaya. Lakini linapokuja swala la michuano ya changanyikeni (mfano COPA MUNDIALI) nakua sina kabisa msisimko na wazungu. Binafsi ni mpenzi wa UNITED kibongobongo AZAM, lakini ikatokea zikakutana timu hizo, lazima nitakua upande wa AZAM.
 
Last edited by a moderator:
Ndio bado roho ya ubaguzi ipo wewe shangilia unachopenda sawa na basi usishangilie hizo timu za Africa za wenzako shangilia Taifa stars tu sababu ukileta kipimo cha u africa na European utakuwa umewekea ubaguzi usiige roho zao mbaya wewe Kuwa Mfano Mzuri tu ila Sema tu Mie naishabikia timu za Africa ila sio kwa sababu Fulani mzungu au Fulani mwarabu au Fulani mweusi ndomana timu yetu ya Taifa haina wahindi wakati wapo ni raia.
 
Tulipoteza kwa goli moja, lakini refa katunyima penalty yetu. Ila bado ninaimani na watu weusi wenzangu. Vp mwenzangu, kati ya mabeberu yaliyo twangana jana lipi lilikua beberu lako?

mabeberu lol
 
hamna mchezaji mwenye asili ya afrca hata moja acha wapigwe 2,kwanza ni wabaguzi

nadhani mechi na chile watavaa jezi zao nyekundu. haya mambo ya rangi ya jezi nakumbuka miaka ile hata yanga na simba yaliwahusu sana 🙂
 

Pazi,leo Italia anakupiga ngapi?sema meeenyewe!
 
Afrika bado sana may be algeria na nigeria ila hao wengne wana hati hati.
 
Leo utapata wapinzani wengi sana hapa ila watakaa kimya baada ya dakika 90

cc Katavi rubaman

Tatizo la England hamkawii kulaumiana katika media. Subiri utakavyoona wakina Hodgson,Welbeck, SG, Hart watakavyolaumiwa mkishatolewa. Vitisho vya maisha vitafuata
 
Tatizo la England hamkawii kulaumiana katika media. Subiri utakavyoona wakina Hodgson,Welbeck, SG, Hart watakavyolaumiwa mkishatolewa. Vitisho vya maisha vitafuata
Hiyo ni kweli ndio tabia Yao ila Italy Leo wataokota nyavuni sana Pirlo Leo Pasi hatoweza kutoa basi sioni Pirlo kufikisha Pasi Leo.
 
Ketembea mjini leo mpaka unasikia raha, kila mtu ana smile tuu "Dalili za ushindi"
 
Tatizo la England hamkawii kulaumiana katika media. Subiri utakavyoona wakina Hodgson,Welbeck, SG, Hart watakavyolaumiwa mkishatolewa. Vitisho vya maisha vitafuata

Timu yeyote yenye malengo makubwa kutokana na kuwa kiwango kikubwa ilichonacho iki underperform lazima mjiulize tatizo ni nini, kama leo England itashangaa sana kama itafungwa na Italy lol

#TeamEngland
 
usijali bwana 072,Spain watarudi,daima wanateleza ila kamwe hawaanguki,hawa Holland ni wazuri na wana kocha mzuri ambae anawajua vizuri waspain hususan kizazi cha La Masia Barcelona ambako ndipo aliwafundisha akiwa kocha na msaidizi wake Mourinho,kibinafsi nakiri Spain wana kitu kimoja wakiwa frustrated(mfadhaiko)basi wanakuwa wanapagawa sana,na hata sub zinakuwa zinamchanganya kocha Del Bosque anashindwa kuelewa afanye nini,ila yote 9,bado wana nafasi ya kufika mbali na hata huenda wakatetea kombe maana Spain wapo juu kisoka,inatokea dhahama inawakumba ila wakijirudi wanakuwa moto mechi hiyo,nadhani Casillas na costa walikuwa wamepagawa sana Costa kitendo cha kuzomewa dk zote akigusa mpira na Casillas kujiamini kulipungua,nadhani kuna haja kina De Gea au Reina kupewa nafasi mechi ijayo,na hata beki Juan Fran ambae anaweza kusaidia patna ya Ramos na Pique ambayo bado haijaelewa kidogo,ila in La Furia Roja tunaamini.
 
Ketembea mjini leo mpaka unasikia raha, kila mtu ana smile tuu "Dalili za ushindi"

Hapo angekuwepo Fgrt angefaidi ulabu wa karibia bure. Anyway, England huwa wanatafuta sababu ndogo sana ya kukusanyika kunywa lagers mfungwe msifungwe kelele zitapigwa na pints zitanyweka kama uswahilini kwetu. Kesho mtaanza kutukanana katika TalkSport radio
 

Nasubiri mechi ya Belgium.
 
What? Kuna mchezaji wa Colombia ana miaka 48 au nimesikia vibaya?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…