shukran kwa kushukuru.
Kwa kifupi mafanikio ya wachezaji watatu kwenye WC
Edson.
Akiwa na umri wa miaka 18, aliibeba brazil kuchukua kombe la dunia kwa mara ya kwanza mwaka 1958 alikuwa na umri wa mtoto wa kidato cha nne kwa TZ.
Akawabeba tena brazil wakachukua mwaka 1962.
Mwaka 1966 akalikosa.
Akawabeba tena brazil wakachukua ubingwa tena mwaka 1970.
Mara zote aliifikisha brazil at least robo fainali.
Diego.
Aliwabeba Argentina wakachukua WC mwaka 1986, waliwafunga german fainali.
Akawafikisha fainali mwaka 1990, walifungwa na german goli moja la penati, Andre Brehme alipiga hiyo penati.
Messi.
Hii ni mara ya tatu anashiriki, ana umri wa miaka 26, ameingia fainali ya kwanza ya WC mwaka huu 2014, hatujui kama Wajerumani watamwacha achukue.
Kuhusu Maradona kupigiwa kura awe mfalme wa soka duniani, zilikuwa ni hila kwa sababu Edson ni mweusi tiiiii, weupe mpaka kesho roho zinawauma lakini hakuna atakayefuta record za Edson, wapenda haki walitengua uteuzi wa Diego kwa kuhusisha madawa ya kuongeza nguvu.
Kampeni zipo tu kwenye michezo, media zinatumika kupaisha watu.
Wajerumani wamemrudisha Klose timu ya taifa ili avunje record ya kufunga magoli mengi kwenye WC, walikuwa wanamtengenezea nafasi za kufunga avunje rocord, ndio maana unaona hata goli lake alilowafunga Brazil mtoaji pasi alikuwa na uwezo wa kufunga wakampa yeye apige tena na tena.
Yote hiyo ni ili mtu wao ndiye awe ameweka record.