Kuna kina sisi ambao toka game 1 ya Brazil tulilalamika kuhusu kiwango chao kibovu na kubebwa na marefa, kwenye mechi kama ya Vs Colombia tuliiona Brazil inayocheza kama Stoke City na mimi binafsi niliambiwa nina chuki binafsi na Brazil kwa kukosoa mchezo wao mbovu kama rugby
Brazil ilikua mbovu kutokana na mambo mengi, kuanzia selection of players, mfumo waliocheza uwanjani, kocha ambaye anaonekana kuishiwa mbinu kila uchao, team kumtegemea sana Neymar na kuongozwa sana na emotions kuliko professionalism
Sijawahi kuona team so emotional kama Brazil hii, walikua wanalia sana wakivuka round, wakiimba wimbo wa Taifa mpaka wakongwe wao waliwakosoa hasa captain wa team na juzi kwenye mechi na Ujerumani nilishangaa kuona mpaka kocha anaingia uwanjani kavaa kofia imeandikwa "forca Neymar" na kabla ya hapo walishaita psychologist awasaidie vijana kuhusiana ana suala la Neymar, real? Halafu kabla ya mechi wakaingia na jezi ya Neymar utafikiri dogo labla kafa au kapata ulemavu wa maisha, na kocha wao aliruhusu hili bila kujua soka ni mchezo wa watu 11, this was lack of professionalism and they got punished for it
Pamoja na hayo watu hawataki to acknowledge that the Germans were far more superior than any Brazilian on the pitch, goal la kwanza la Muller unalosema aliachwa free mapundits/wachezaji wastaafu wanakwambia ile move ilitengenezwa kwenye training ground, Luiz alikua blocked na Klose ndio Muller akapata nafasi ya kufunga hakuna bahati wala magic ni ufundi tu, kama huamini tafuta replays
Goal la pili ni uzembe wa Marcelo kwa kiasi kikubwa, na baada ya hapo Wajerumani kwa sababu ni top professionals walisense jamaa wanaanza kucrack na wakaitumia nafasi hiyo vyema kumaliza mpira kabla hata ya half time, waliwapress Brazil high up on the pitch kupata hizo goli tatu, hakuna easy goal scoring hapo, kama ni hivyo kwanini team zote zilizocheza na Brazil mpaka juzi zilishindwa kufanya alichokifanya mkoloni?
Kwa kumalizia ili kujua Wajerumani walikua top professionals juzi, Mats Hummels anakwambia wakiwa mapumziko walikubaliana not to humiliate the Brazilians in their own WC na hujasikia mchezaji wa Ujerumani akisema ile ilikua revenge ya 2002 or whatsoever lakini unasikia kina Muller wakisema Brazil hawakustahili kipigo kizito kile tena wakiwa nyumbani kwao.
Kaka hamna kitu pale. Brasil ilikuwa ni takataka. Niliangalia game ya Ghana na Ujeruman ulimi nje, wakaambulia draw ya 2-2! Sifa hizo unazowapa hawana. Niliangalia mechi na France walipata goli1 ambacho ni kitu cha kawaida. Uzembe wa Brasil usisababishe kuwapa vichwa Wajerumani ambapo si halali yao. Ninachoweza kusema Ujerumani ni wa kiwango sawa kabisa na Mexico, US, Colombia, Argentina, Uholanzi, Spain nk. Hii ya ushindi wa 1-7 haiwezi kuwa kipimo kikubwa. Ngoja wakutane na watu wenye nidham ya mpira utakumbuka maneno yangu. Germany ni.wa kawaida kabisa!