World Cup 2014, Brazil: June 12 - July 13

World Cup 2014, Brazil: June 12 - July 13

Ngabu I am not sure kama unafuatilia mpira......hasa Eoropean Champions league...hiki kilichotekea bRAZIL kimewahi itokea timu za Spain mwaka jana..Barcelona na Real Madrid.... walipigwa hivi hivi na tinu za Ujerumani....Barca walipigwa saba na Bayern na Barca hiii hii yenye Messi.....wataalamu wanasema kuna kitu kimebadilika kwenye mpira...ndo maana unaona Brazil anafungwa huku anaongoza 'ball possessions '.......wanahitajika wajifunze European way of defending....Argentina wana defend European way...sio kama zamani tena.....so kikubwa ni tactic na technincs

Hapana, sikubaliani na wewe. Sidhani kabisa kama mpira umebadilika kihivyo maana hata timu zingine za Ulaya (Hispania, Uingereza, Ureno, Italia, na zinginezo) nazo hazikufanya vizuri.

Nadhani kilichotokea, hususan kwa Brasil, ni ile cyclical nature ya team sports. Huwezi kuwa juu kila siku na huwezi kuwa na timu bora kila mwaka.

Wakati mwingine lows na failures kama hizi zinahitajika (kama reminders) ili kuweza kufanya tathmini na hatimaye kuja na timu bora.

Hao Wajerumani wenyewe hawajashinda kombe la dunia kwa miaka 24. Kama ni mtu, mtu huyo ni mkubwa kuweza kuwa na familia yake kabisa. Na hata kombe la dunia lilipofanyika Ujerumani mwaka 2006 (miaka nane tu iliyopita), Ujerumani ilitolewa kwenye nusu fainali. Imagine Ujerumani wakatolewa nyumbani kwao (yale yale kama ya Brasil mwaka huu na Italia mwaka 1990).

Tukubali tu kuwa mwaka huu Brasil hawakuwa na timu nzuri. Kwanza wana bahati sana hata kuvuka raundi ya pili maana Chile aliwapelekesha vibaya mno. Na isingekuwa ile nduki ya yule jamaa kugonga mwamba dakika ya 119, basi wangetolewa kwenye raundi ya pili.

Mimi bado nawaaminia sana kwa sababu miaka nenda rudi wameweza kuzalisha vikosi ambavyo ni tishio. Kikosi kikali cha mwisho kilikuwa cha akina Romario na Bebeto mwaka 1994 Marekani.

Hata kikosi cha 2002 cha akina Ronaldo, Gilberto Silva, Roberto Carlos, Rivaldo, na Ronadinho nacho kilikuwa kikali. Na guess what...kilishinda kombe la dunia kwa kuifunga Ujerumani 2-0.

Na vikosi vyote hivyo vilikuwa na legitimate goal scorers...tena zaidi ya mmoja.

Brasil will be back better and stronger than ever. After all, this is the most successful country in world cup competition. They didn't become 5 time world champions because of luck.

They'll be back. Trust me. Na sidhani kwamba mpira umebadilika hivyo. Ni kwamba tu mwaka huu, for whatever reason(s), wame field timu dhaifu sana.

Till the death of me, in Brasil I trust.
 
Back
Top Bottom