World Cup 2014, Brazil: June 12 - July 13

World Cup 2014, Brazil: June 12 - July 13

Mkuu Mag3 mie timu nilizopenda uchezaji wake ni Colombia na Chile, wachezaji Robben, Di Maria, Sanchez, Rodriguez na makipa Algeria, Ghana na Nigeria.

Mashabiki wa bongo mnatia huruma...wapo waliotangaza toka awali kabisa kuwa bingwa wa kombe la Dunia 2014 anayesubiri tu kukabidhiwa kombe rasmi ni Brazil ; sisi wengine tunaofuatilia kandanda linavyotandazwa uwanjani tukaguna nnh! Mashabiki hao hao sasa wamegeuka wanapowaponda wachezaji wale wale wa Brazil eti kwa kuonesha viwango duni! Mimi najikuta naguna tena nnh! Najiuliza, hivi ingekuwaje kama Brazil ndio ingeifunga Ujerumani, hao akina Luiz, Marcelo, Dante, Alves, Victor na mlinda mlango Ceaser mngewaponda kweli? Kwa nini hamko tayari kukubali kirahisi kuwa timu ya Ujerumani ni timu bora kuliko ya Brazil?

Badala ya kuwakashifu hao wachezaji mnaowapenda, kwa nini msielekeze sifa pale kunakostahili kwa wachezaji wa Ujerumani? Haya, imetokea tena leo; pamoja na Silva kuwa ndani Brazil imezidi kuvuna ilichopanda, kwa nini Mholanzi asipewe sifa? Kwa nini Roben, Ron, Paul, Joel na kipa wao Michael hamuwapi haki yao? Okay kesho kuna kinyang'anyiro kingine kati ya Argentina na Ujerumani na mpaka sasa ni Ujerumani ndiyo imeonesha kiwango cha juu katika haya mashindano...nawaomba muwe tayari kupokea matokeo bila kinyongo; msiruhusu ushabiki uwafunike macho hadi mshindwe kuenjoy gozi linavyosakatwa hadi mshindi apatikane na kupongezwa. Usiku mwema!
 
Last edited by a moderator:
Leo kiwanja cha nyumbani Ukonga-Gongo la mboto bar inaitwa Chadibwa karibu sana na makabuli ya Mzee Njenje!
Nipo hapa hadi saa 2 usiku!!Wakuu njooni tujadili soka!!
 
Back
Top Bottom