Wosia wa Ballali kuwaumbua wengi!

Wosia wa Ballali kuwaumbua wengi!

Dk. Ballali kuumbua vigogo

  • Wosia wake wataja walioshinikiza EPA
  • Wanasiasa, wanasheria wauhifadhi
Mwandishi Wetu Mei 21, 2008

KIFO cha aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu (BoT) Dk. Daudi Timoth Said Ballali (65) kinazidi kuibua mambo mengi, sasa waliokuwa karibu naye wanataka undani wa wosia aliouandika kwa mkono wake na maelezo aliyoandika alipohojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kabla ya kuondoka nchini kwenda Marekani, uanikwe.

Watu mbalimbali walio karibu na familia ya Ballali, wakiwamo wanasiasa na wanasheria, waliozungumza na Raia Mwema wiki hii, wamesema ni wakati mwafaka kwa sasa mambo yote aliyoyaacha gavana huyo wa zamani yawekwe wazi ili kuondoa utata kwamba kuna jambo linalofichwa.

Wakati hayo yakiendelea, habari zinasema kwamba kuna mkakati maalumu wa kuhakikisha kwamba siri ya waraka huo haitolewi hadharani na baadhi ya watu mashuhuri wamethubutu kusafiri hadi nchini Marekani kufanikisha mkakati huo bila kujua mengi zaidi yapo nyumbani Tanzania.

Akizungumza na Raia Mwema wiki hii, mwanasheria mmoja mashuhuri amesema anafahamu na ameuona waraka aliouandika Ballali kwa mkono wake akielezea mambo mengi ya msingi aliyotuhumiwa nayo ikiwamo lile sakata la fedha za Mfuko wa Madeni ya Nje (EPA) uliokuwa ukisimamiwa na BoT, ambako zaidi ya Sh. bilioni 133 zinadaiwa kupotea.

“Ballali aliandika kwa mkono bila kupigwa chapa mambo yote yaliyotokea ambayo anatuhumiwa kuyafanya kama mhalifu na amewataja watu wote kwa majina na muda bila kuacha katika waraka wake huo ambao ameweka saini na kuhitimisha kwa alama za vidole,” anasema mwanasheria huyo ambaye hajawahi kutajwa popote kuwa na mahusiano na Ballali wala BoT.

Maelezo ya mwanasheria huyo yameshabihiana karibu kwa kila kitu na Mbunge mmoja wa Upinzani ambaye pia ni mmoja wa viongozi muhimu katika kambi ya upinzani ambaye naye amekiri kuuona waraka. Mwanasiasa huyo hakukiri wala kukanusha kuwa na nakala ya waraka huo wa Ballali.

Wote wawili wanasema kwamba waraka huo unaweza ama uko mikononi mwa watu zaidi ya watano wakiwamo wanasheria, wanasiasa wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wa sasa na wa zamani, wanasiasa wawili wa kambi ya upinzani na baadhi ya wanafamilia na hivyo ni vigumu sana kwa mtu yeyote kuubadili ama kuuficha “milele”..

Kwa mujibu wa habari hizo, sehemu ya waraka huo inaelezwa kuelezea kwa kina kuhusu nini hasa kilichofanyika hadi BoT ikaidhinisha kutolewa kwa kiasi cha Sh bilioni 133/- na Ballali anaeleza kwa uwazi wahusika wote wakuu wakiwamo viongozi wa juu wa Serikali na wanasiasa walioshinikiza na waliochukua sehemu kubwa ya fedha za EPA pamoja na watendaji wa BoT walioshiriki katika zoezi hilo.

Waraka huo ambao kwa sasa unatafutwa kwa udi na uvumba unadhihirisha kuwapo kwa usiri mkubwa ndani ya Serikali kutokana na baadhi ya wahusika muhimu wanaotajwa na Ballali kutozungumzwa popote linapozungumzwa suala la EPA na hata katika vyombo vya habari.

Kwa mujibu wa waliouona waraka huo wa wosia, Ballali, kwa mfano, anaeleza jinsi alivyosita kuidhinisha malipo ya Kampuni ya Kagoda Agriculture Limited, ambayo pekee ilikabidhiwa kiasi cha Dola za Marekani 30,732,658.82 (takriban Sh. bilioni 40/-) kwa kutumia nyaraka za kughushi.

“Ballali ameeleza katika waraka ule kwamba alikataa kuidhinisha malipo hayo akielezea jinsi isivyo sahihi kutumia nyaraka za kughushi lakini aliitwa na mwanasiasa mmoja akiwa na mwanasiasa mwingine mkongwe mwenye ushawishi hadi sasa ambako aliamrishwa kuidhinisha malipo hayo mara moja.

“Unajua alivyoitwa aliwaeleza athari za kutumia nyaraka za kughushi wakamlazimisha na baada ya kuona wanamlazimisha akawaambia kama BoT itaidhinisha basi mtu anayatakiwa kukabidhiwa fedha hizo hastahili kwa kuwa kuna fedha nyingine zaidi ya Dola za milioni 60 alizotakiwa kurejesha kwanza kabla ya kukabidhiwa fedha zozote, lakini akalazimishwa kumlipa huyo huyo,” anasema mwanasheria aliyezungumza na Raia Mwema.

Mwanasheria huyo anasema mfanyabiashara huyo ambaye ni mwanasiasa mwenye ushawishi mkubwa katika siasa za Tanzania alikuwa akiwasiliana na wanasiasa waliomshinikiza Ballali amlipe kiasi cha kumpigia simu Ballali kabla hata ya kuondoka viwanja vya majengo alikokutana nao.

“Unajua inatisha kwani Ballali anasema katika waraka wake huo kwamba alipotoka tu kuzungumza na wazee wale kabla hata ya kuondoka akapigiwa simu na mfanyabiashara huyo akimuuliza kama alikwisha kupata maelekezo na yeye kumtaka aende ofisini ambako atakutana na msaidizi wake ambaye ndiye anayeshughulikia fedha za EPA,” anasema.

Mwanasheria huyo anasema mfanyabiashara aliyekabidhiwa fedha hizo ana uhusiano wa karibu sana kibiashara na kijamii na ofisa wa BoT aliyehusika pia na sehemu ya mchakato wa EPA, jambo ambalo limeelezwa kwamba linazidi kuibua utata baada ya wote wawili kutotajwa popote katika sakata hilo.

“Sijasikia popote huyo ofisa wa BoT akitajwa maana hata nafasi ya ugavana alikuwa akitajwa kuwa anaweza kupewa lakini bahati ndiyo akateuliwa Profesa Benno Ndulu, maana angeteuliwa (anamtaja jina) mambo yangeendelea kuwa mabaya zaidi na siri nyingi zingefichwa lakini sasa najua mambo yatajulikana tu,” anasema.

Kampuni ya Kagoda Agriculture Limited ambayo inatajwa kuchota zaidi ya Sh. bilioni 40/- hadi sasa haijulikani ilipo pamoja na kuwapo madai kwamba ilikabidhiwa kwa mfanyabiashara mmoja mwenye kashfa nyingi nchini ili ionekane kuwa ni ya kwake lakini hadi sasa haijaelezwa bayana hasa ni mali ya nani.

Kampuni hiyo kwa kumbukumbu za Msajili wa Makampuni (BRELA) inaonyeshwa kwamba ofisi zake zipo Kipawa Industrial Area Plot namba 87, Temeke, Dar es Salaam lakini eneo hilo lina kampuni tofauti jirani lakini namba hiyo haionekani na kinachoonekana ni viwanja kuanzia Plot 77 na hata Plot 86 na Plot 88 katika eneo hilo maarufu la viwanda lakini plot ilipo Kagoda haionekani popote.

Aliyesimamia na kufuatilia BoT na hatimaye chukua fedha za kampuni hiyo katika Benki ya CRDB Limited tawi la Azikiwe anajulikana waziwazi na wafanyakazi wa maeneo hayo, lakini kumbukumbu zake zinaelezwa kupotea ama kufichwa na wahusika kwa nia ya kuwasaidia watuhumiwa ama kwa sababu za kichunguzi.

Hata hivyo, inaelezwa kwamba wapelelezi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) walikwisha kuchukua nyaraka zote muhimu ikiwa ni pamoja na kadi ya benki iliyotumika kufungulia akaunti tawi la Azikiwe, ikiwa na picha na saini za wahusika wote muhimu kwa uhakika zaidi.

Sakata la BoT na zaidi akaunti ya EPA lilichukua sura mpya baada ya kuelezwa kwamba sasa mkakati wa Serikali ni kuhakikisha fedha zote kiasi cha Sh. bilioni 133 zinarejeshwa kabla ya kuchukuliwa hatua kwa wale waliofanya makosa ya kijinai katika kupata fedha hizo.

Imeelezwa katika hali ya kutatanisha tayari hata fedha kutoka kwa wamiliki wa Kagoda nazo zimekwishakuanza kurejeshwa japo kwa awamu, jambo linalodhihirisha kwamba Serikali inawafahamu kwa hakika kabisa wamiliki wa Kagoda na inawaficha ama inataka kuwalinda kwa sababu za kisiasa zaidi.

Katika uchunguzi wa awali wa mkaguzi wa nje, Samuel Sithole wa kampuni ya kimataifa ya Deloitte & Touche tawi la Afrika Kusini alionya kuhusu matendo ya kihalifu ndani ya Kagoda kabla ya kuandikiwa barua na Waziri wa Fedha, Zakia Meghji kwamba fedha hizo zilienda katika mambo “nyeti” ya kiusalama.

Hata hivyo, siku nne baada ya kuandika barua hiyo, Meghji alifuta barua hiyo akielezea kupotoshwa na Gavana Ballali, uamuzi ambao ulimgharimu kwa kiasi kikubwa mwanamama huyo ambaye sasa ameachwa nje ya Baraza la Mawaziri.

Baada ya kifo cha Ballali sasa inaelezwa kwamba uchunguzi unaoendelea dhidi ya wanaotajwa kuchukua fedha za EPA unaweza kufungwa kwa kuwa shahidi muhimu atakuwa hawezi kutoa maelezo yake mahakamani jambo ambalo linaelezwa kuweza kuichafua zaidi serikali.

Ballali ambaye amefariki dunia akiwa nchini Marekani na kuzikwa huko huko anaelezwa kuondoka na siri nzito ikiwa ni pamoja na mazingira ya kuondoka kwake, kuugua na hata kifo kumkuta huku serikali ikiendelea ‘kuweweseka’ na ‘kutapatapa’ kutokana mkanganyiko mkubwa wa yaliyomsibu gavana huyo wa zamani.

Hata mahali na siku aliyofariki Ballali ni mambo yaliyoelezwa kuwa na utata hasa baada ya kuwapo kwa taarifa kwamba alifia Boston, huku wengine wakisema alifia nyumbani kwake Washington DC Ijumaa ya Mei 16, 2008 na baadaye taarifa zake kutangazwa Jumanne usiku ikiwa ni siku tano baadaye, huku baadhi wakianza kudai kwamba alifariki Jumapili ya Mei 18, 2008. Hata mazishi yake yalifanywa kuwa siri na ni wanafamilia wachache tu waliobahatika kuuona mwili wake Jumanne Mei 20, 2008.


KANISA la Mt. Stephen Shahidi

Mwili wa marehemu Ballali ulihifadhiwa katika Nyumba ya Maziko ya De Vol iliyoko Washington DC, kabla ya ibada iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Mt. Stephen Shahidi mjini Washington DC. Kanisa hilo lipo 2436 Pennsylvania Ave, NW Washington, DC 20037 na baadaye kuzikwa kwa faragha katika makaburi ya Wakatoliki ya Gate of Heaven eneo la Silver Spring, Maryland.

Pamoja na kashfa nyingi zilizoandikwa na vyombo mbalimbali, hasa magazeti na kutangazwa majukwaani, Ballali hakuwahi kushtakiwa rasmi pamoja na kuwapo taarifa kwamba aliwahi kuhojiwa na TAKUKURU.

Mmoja wa wanasiasa wakongwe nchini, Jaji Joseph Warioba akizungumzia kifo hicho cha Dk. Ballali wiki hii, ameiambia Raia Mwema kwamba anaona unafiki wa hali ya juu katika matamshi na matendo ya wanasiasa.

“Huu ni unafiki mkubwa. Muacheni Ballali apumzike kwa amani. Kwanza walimwita ni fisadi, sasa wanasema shahidi muhimu amekufa. Katoka kuwa fisadi wakati wa uhai kuwa shahidi katika mauti,” alisema Warioba katika mahojiano ya simu mwanzoni mwa wiki hii.

Aliongeza Warioba: “Amekuwa kafara. Taarifa ya Serikali kuhusu fedha za EPA ilionyesha wazi Ballali amechukuliwa hatua katika utaratibu wa kawaida wa kuwajibika. Haikumtuhumu kwamba alikuwa ameiba fedha. Fedha zile bilioni 133 ni jumla ya fedha zote zilizochukuliwa na kampuni 22 zilizotajwa katika taarifa ya Serikali.

“Ballali hakutajwa katika orodha ya kampuni hizo. Hilo Serikali inajua, viongozi wa siasa wanajua na vyombo vya habari vinajua. Lakini wote hao, kwa kipindi chote alichokuwa hai walimhukumu kama mtu aliyekuwa ameiba fedha. Lakini waliochukua fedha zile wanafahamika.

“Kwa muda wa miezi mitano Kamati (ya uchunguzi wa kashafa ya EPA) imekuwa ikiwaambia wananchi inakusanya fedha hizo kutoka kwa watu wanaoitwa. Ilipoulizwa kuhusu Ballali ilisema haimuhitaji. Maana yake hakuwamo katika orodha ya waliochukua fedha zile. Lakini sasa amefariki wimbo umebadilika. Wanasiasa na vyombo vya habari vinamwita si fisadi tena, bali shahidi muhimu wa wizi wa EPA.

“Huu ni unafiki mkubwa. Kuna visingizio kwamba ugonjwa wa Ballali haujulikani, lakini Serikali inajua kwani alikuwa analipiwa matibabu na Benki Kuu. Alikuwa Boston, Marekani, ile nchi iko wazi mtu angetaka kujua angejua. Lakini sasa wanasiasa na vyombo vya habari vinalalamika kwamba ugonjwa wake ulifanywa siri. Kumbe ni uzembe wao.

“ Sasa tumeanza kutafuta mchawi huku. Na hapa ikisha kutamkwa neno fisadi tu, basi hata kama mtu hana ushahidi unakuwa fisadi. Lakini yote haya hakuna anayekuambia Ballali aliiba kiasi gani. Wamuache apumzike kwa amani, siku moja ukweli utafahamika.”

Ballali ambaye ameacha mke na familia, amekuwa akitamka wazi kwamba hajawahi kuiba hata senti moja ya umma katika kipindi chote akiwa BoT na kuwashutumu watu ‘aliowakwamisha’ kuwa chanzo cha kuandamwa kwake na tuhuma mbalimbali kabla ya kukataliwa kujiuzulu na hatimaye uteuzi wake kutenguliwa na Rais Jakaya Kikwete.

Marehemu Ballali alijiunga na Benki kama Gavana Julai 14, 1998 hadi Januari 8, 2008.

Ballali alikwenda ghafla nchini Marekani mwishoni mwa mwaka jana akiwa na nia ya kurejea nchini, alikwama huko baada ya kubainika na matatizo makubwa tumboni kabla ya kulazwa hospitali na kufanyiwa upasuaji mkubwa.

Kwa mujibu wa habari za awali, Ballali aliieleza familia yake kwamba alikuwa akihofia kula kitu chenye madhara makubwa hasa baada ya madaktari wa Marekani kumfanyia uchunguzi mara tu alipowasili nchini humo, madhara ambayo alionyesha kuhisi kuyapata alipokuwa nyumbani hasa kati ya miji ya Dar es Salaan na Dodoma.

Wakati akiendelea na matibabu, Ballali aliandika barua kuelezea nia yake ya kuomba kujiuzulu kutokana na kuendelea kuzorota kwa afya yake huku akiwa bado na majukumu mazito ya kusimamia uchumi wa Taifa.

Hata hivyo, hakukuwa na taarifa zozote za upande wa Serikali kuthibitisha kupokea barua ya kujiuzulu kwa Ballali siku kadhaa kabla ya serikali kutangaza matokeo ya ukaguzi wa kampuni ya nje iliyopewa kazi ya kukagua hesabu za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA).

Ni baada ya Rais Jakaya Kikwete kutangaza kupitia ripoti ya wakaguzi hao, ndipo alipotamka kumfuta kazi Ballali bila kuzungumzia lolote kuhusu kujiuzulu kwake.
 
Haya sasa ndiyo maneno ya JF sio upuuzi ulioko kwenye mazingira ya kifo cha Balali wakati swala hapa ni kuwashughulikia waharifu..tuna loose focus kwa sababu ya upuuuzi wa baadhi yetu kuhoji kila kitu nje ya tatizo.
 
ttu-focus namna ya kupata wosia wa balali, na wanasheria mmtusaidie namna ya kuwapata au kwashinikiza wote walitajwa waende mkumbo mmoja na lowasa,karamagi, chenge etc, ikiwezekana wakawe mgeni wa zombe huko gerezani
 
Kama kweli hizi nyaraka ziko nje namna hiyo basi Watanzania wategemee kuziona hapa JF muda mfupi kuanzia sasa .JF hawalali na tuko for our Country bwana .Yalisemwa mengi lakini kila lenye mwanzo huwa lina mwisho pia .Tokea mwanzo nilikuwa na msimamo Balali hakuiba ila anatumiwa na wana siasa akina Meghji .Tutajua ukweli maana tumeingia kazini sasa .
 
npl1lk.jpg
 
Ballali aliacha mikanda ya video

Mwandishi Wetu Juni 11, 2008
Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo

Ni katika asasi nyeti Marekani

TAKRIBAN mwezi mmoja tangu aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Dk. Daudi Ballali (65) afariki dunia, kile kinachoitwa wosia ama ushahidi aliouacha kinazidi kuwatesa wengi na habari zinasema aliukabidhi pia katika taasisi nyeti za fedha duniani kama Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF).

Habari kutoka vyanzo mbalimbali vya habari zinaeleza kwamba watu kadhaa wanaohofia kuumizwa na wosia huo wamekuwa wakihaha kuhakikisha wanaupata ama kuzuia kuenea kwake na wengine kutaka kueneza propaganda za kupunguza makali yake ndani na nje ya nchi.

Wiki hii Raia Mwema imeambiwa kwamba pamoja na kuwa kuna nyaraka ambazo Dk. Ballali aliziweka katika mikono salama nchini, alipokuwa akiugulia Marekani nako alipata wasaa wa kuweka nyaraka nyingine muhimu katika mikono ya asasi kubwa za kimataifa ambako zinalindwa hadi muda utakapowadia wa kuziweka hadharani.

“Ni kweli Ballali ameacha wosia na amerekodi kaseti ya video akielezea yaliyotokea BoT na maelezo mengine kayaweka kwa maandishi. Unajua alihofia familia yake kusumbuliwa kwa hiyo akaamua kuacha katika mikono ya vyombo vya kimataifa na kwa wanasheria,” anasema mkongwe mmoja wa siasa za Tanzania ambaye kwa sababu za wazi Raia Mwema haitamtaja jina.

Kauli ya mzee huyo inaungwa mkono na chanzo kingine cha habari kutoka nchini Marekani kinachoeleza bayana kwamba asasi za kimataifa ambazo zimekabidhiwa video hiyo zinaweza kuanika hadharani ama kutumia ushahidi huo katika wakati mwafaka.

Imeelezwa kwamba asasi hizo zinaweza kutumia ushahidi huo kuibana Serikali ya Tanzania kuhusiana na kutowagusa kabisa wahusika wakuu wa upotevu wa fedha ndani ya BoT pamoja na kuwa wanafahamika katika duru mbalimbali serikalini, BoT kwenyewe, benki mbalimbali na katika baadhi ya kampuni za uwakili.

Raia Mwema imearifiwa kwamba Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) ambako Dk. Ballali alipata kufanya kazi kwa miaka mingi, na ambako alijizolea sifa kubwa, liliwakilishwa katika mazishi yake na mmoja wa maofisa wake ambaye alimsifia Dk. Ballali kwa kazi nzuri aliyofanya akiwa ofisa wa IMF nchini Ghana, Tanzania na Zimbabwe.

Alikuwa amekuja Tanzania, yeye na aliyekuja kuwa mkewe, Anna Muganda, katika miaka ya katikati ya 1990, baada ya Rais wa wakati huo, Benjamin Mkapa, kuomba kwa IMF na Benki ya Dunia (WB) msaada wa mtaalamu wa fedha ambaye angeongoza marekebisho mbalimbali ya kiuchumi yaliyokuwa yakifanywa.

Hatimaye, mwaka 1998, Mkapa alimtangaza Dk. Ballali kuwa gavana akichukua nafasi iliyokuwa imeachwa na Mkurugenzi wa sasa wa Kampuni ya Umeme (TANESCO), Dk. Idrisa Rashid.

Pamoja na kashfa za wizi wa fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya BoT ambayo imetawala katika mijadala mbalimbali nchini baada ya kuibuliwa mwaka jana, na ukweli kwamba kuna maeneo aliyafumbia macho ama alikubali kuendeshwa na mashinikizo ya kisiasa, bado IMF ilikuwa ikimwona Dk. Ballali kama mmoja wa maofisa wake waliokuwa wachapa kazi vizuri na habari zinasema ni heshima hiyo iliyosababisha ofisa wake kushiriki mazishi na mawasiliano ya karibu yaliyokuwapo kwa pande hizo mbili katika siku za mwisho za uhai wake.

Taarifa za wiki hii baada ya Raia Mwema kubainisha maoni na baadhi ya vielelezo kadhaa vya eneo moja tu la wizi huo wa EPA katika toleo lake la wiki iliyopita, zinaonyesha kwamba kulikuwa na kasi ya ajabu, ambayo si ya kawaida katika jinsi maofisa wa ngazi mbalimbali ndani ya BoT walivyokuwa wakihaha kufanikisha malipo hayo.

Waraka mmoja ambao Raia Mwema imefanikiwa kuuona unaonyesha kwamba katika muda mfupi, maamuzi mengine yakifanywa ndani ya saa chache tu, kwa mfano, nyaraka za kampuni ya Kagoda Agriculture, zilipita ngazi mbalimbali katika kasi inayoashiria kwamba maofisa wa BoT walikuwa wakifukuzana na mafaili hayo kutoka ofisi moja hadi nyingine.

Mtaalamu mmoja wa masuala ya ununuzi wa madeni ya nje anasema hivi kuhusu kasi hiyo: “Suala la ununuzi madeni si suala la kutafuta taarifa leo na kupata leo. Kwamba watu ndani ya BoT na hao waliokuwa wakifuatilia ununuzi wa madeni hayo waliweza kuifanya kazi hiyo ndani ya wiki, tena inaelekea kwa kampuni karibu zote 20, ni jambo ambalo linatia shaka kuhusu usahihi wa madeni yenyewe na inawezekana hata hayo madeni hayakuwapo.”

Tangu kufariki dunia kwa Dk. Ballali kumezuka mawazo miongoni mwa wana jamii kwamba huo ndio utakaokuwa mwisho wa suala la wizi wa EPA. Na japo haijazungumzwa wazi, kumekuwapo na jitihada katika idara mbalimbali serikalini za kutaka suala hilo “life na Dk. Ballali”.

Aidha, Raia Mwema imearifiwa kwamba kumekuwapo pia na uwezekano wa Kamati ya Rais ya kuchunguza EPA inayoundwa na Inspekta Jenerali wa Polisi, Said Mwema, Mwanasheria Mkuu, Johnson Mwanyika na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Edward Hosea ikaongezewa muda katika kile kinachoelezwa kwamba ni kuchelewesha tu na kuvuta muda ili EPA isahaulike.

Sambamba na hayo, kuna maoni pia kwamba jitihada zimekuwa zikifanyika kutaka baadhi ya washiriki wa wizi wa EPA kubebewa mizigo na watu ambao wamejitoa kafara ili kuepusha muanguko wa kisiasa wa baadhi yao ambao machoni wamekuwa wakionekana kama wanasiasa na wafanyabiashara maarufu, lakini ambao wako katikati ya wizi wa EPA.

“Tayari sasa imekuwa rasmi kwamba…. (anamtaja jina) ndiye mhusika mkuu wa fedha za EPA na …..(anamtaja jina) kwa sasa hayupo kabisa na hatajwi popote na wachunguzi wa timu ya Mwanyika,” kinaeleza chanzo cha habari chenye mawasiliano ya karibu na watendaji serikalini.

Hata hivyo, mtoa habari huyo ameliambia Raia Mwema kwamba mkakati huo wa Serikali ni wa muda mfupi kwa kuwa kuna maelezo yenye nguvu ambayo yanamhusisha moja kwa moja mwanasiasa anayekingiwa kifua.

“Kuna maandishi ya kisheria ambayo yanaeleza kwa kina yaliyotokea BoT na zaidi kuhusu fedha za EPA na kwa kina maelezo hayo yanataja ni jinsi gani mfanyabiashara huyo alivyohusika katika mchakato mzima wa malipo ya fedha hizo,” anasema.

Mbali ya wosia huo ambao sasa ni gumzo la kila mtu anayejali, Ballali anaelezwa kuhojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kabla ya kuondoka nchini kwenda Marekani, maelezo ambayo hadi sasa hayajawekwa wazi.

Habari za awali zilieleza kwamba watu mbalimbali walio karibu na Marehemu Ballali, wakiwamo wanasiasa na wanasheria wamekabidhiwa nakala ya maelezo ya gavana huyo wa zamani wa BoT.

Mwanasheria aliyeuona waraka aliouandika Ballali kwa mkono wake anasema umeeleza mambo mengi ya msingi aliyotuhumiwa nayo ikiwamo sakata la fedha za EPA zilizokuwa zikisimamiwa na BoT, zinazokadiriwa kuwa zaidi ya Sh bilioni 133.

Kwa mujibu wa waliouona waraka huo wa wosia, Ballali anaeleza, kwa mfano, jinsi alivyosita kuidhinisha malipo ya Kampuni ya Kagoda Agricultural Limited, ambayo pekee ilikabidhiwa kiasi cha Dola za Marekani 30,732,658.82 (takriban Shilingi Bilioni 40/-) kwa kutumia nyaraka za kughushi.

“Ballali ameeleza katika waraka ule kwamba alikataa kuidhinisha malipo hayo akielezea jinsi isivyo sahihi kutumia nyaraka za kughushi lakini aliitwa na mkubwa na kuamrishwa kuidhinisha malipo hayo mara moja. Kampuni ya Kagoda Agricultural Limited inatajwa kuchota zaidi ya Sh bilioni 40.

Kampuni hiyo, kwa mujibu wa kumbukumbu za Msajili wa Makampuni (BRELA), ina ofisi Kipawa Industrial Area Plot namba 87, Temeke, Dar es Salaam lakini eneo hilo lina makampuni tofauti jirani na namba hiyo haionekani na kinachoonekana ni viwanja kuanzia Plot 77 na hata Plot 86 na Plot 88 katika eneo hilo maarufu la viwanda.

Lakini habari zinasema, kama itabidi, maofisa wa BoT na baadhi ya wanasheria, kwa kuokoa nafsi zao, watalazimika kutaja ni nani alikuwa akifuatilia fedha hizo za EPA katika kampuni ya Kagoda; hasa kwa kuwa nyaraka za kisheria zipo za kuhusu mchakato mzima wa unununuzi huo hewa wa madeni.

Raia Mwema imearifiwa kwamba kama ulivyo wosia wa Dk. Ballali, vivuli vya hundi kadhaa, zinazoonyesha ni wapi fedha hizo zilikwenda na nyaraka nyingine zinazoonyesha nani walihusika, ziko katika hifadhi za watu mbalimbali na kwamba wakati utakapofika mambo yote yatawekwa hadharani ama Mahakamani, katika majukwaa ya kisiasa au kwenye vyombo vya habari.

Kamati ya Mwanyika imekuwa ikisema kwamba mkakati wake ni kuhakikisha fedha zote, shilingi bilioni 133, zinarejeshwa kabla ya kuchukuliwa hatua kwa wale waliofanya makosa ya kijinai katika kupata fedha hizo.

Imeelezwa kwamba tayari hata fedha ilizochukua kampuni ya Kagoda nazo zimekwishakuanza kurejeshwa japo kwa awamu, jambo linalodhihirisha kwamba wahusika wanafahamika lakini, pengine, kwa kuwa ni vigogo, wametunziwa heshima.

Uchunguzi wa awali wa mkaguzi wa nje wa BoT, Samuel Sithole, kutoka kampuni ya Kimataifa ya Deloitte & Touche ya Afrika Kusini ulionya kuhusu matendo ya kihalifu ndani ya Kagoda kabla ya kuandikiwa barua na Waziri wa Fedha, Zakia Meghji kwamba fedha hizo zilikwenda katika matumizi “nyeti” ya usalama wa nchi.

Lakini siku nne baada ya kuandika barua hiyo, Meghji aliifuta akielezea kupotoshwa na Gavana, Dk. Ballali, ambaye tayari wakati huo alikwisha kwenda katika matibabu Marekani. Meghji hakurejeshwa katika uwaziri baada ya mabadiliko ya Februari.

Katika mikutano yake michache na vyombo vya habari wakati wa uhai wake, Dk.Ballali, ambaye ameacha mke na familia, alikuwa akitamka wazi kwamba hakuwahi kuiba hata senti moja ya umma katika kipindi chote akiwa BoT na alikuwa akiwashutumu watu “aliowakwamisha” kuwa chanzo cha kuandamwa kwake na tuhuma mbalimbali kabla ya kukataliwa kujiuzulu na hatimaye uteuzi wake kutenguliwa na Rais Jakaya Kikwete Januari mwaka huu.
 
.......mhhh, mambo yanavyokwenda,huyu marehemu anaweza kuja kupata sympath ya wengi
 
Ukisoma vizuri hii habari, hakuna jipya zaidi ya yale ambayo yaliandikwa hapa JF na Mzee Mwanakijiji na pia FMES.

Mwanzo ilikuwa kwamba eti anajilinda yeye, sasa wanasema aliogopa familia yake kusumbuliwa.

Nafikiri tunaendelea kurushiwa changa la macho.

Siamini kabisa habari yoyote ya Ballali mpaka watoe hizo video. Yeye kapotea, wanaogopa nini kuzitoa kama zipo?

JF na kujulikana kote kwa watu walioko karibu na Ballali, kweli tungeshindwa kupata copy? Eti copy inapelekwa IMF? Mimi haiingii akilini.
 
Duh! JF bwana kweli tuko mbali sana, yaani hizi dataz tulizimwaga last two weeks wao ndio kwanza wamezipata saa hizi, anyways saafi sana inaonyesha tu JF ni mambo yote!

Wakuu wangu mpo hapa, Jf mbele zaidi! Alyways one step ahead, kwa nyongeza tu ni kwamba aliacha pia tape records na hizo documents kuna ambazo ziko kwa wakulu wa IMF na World Bank, ila effectiveness yake bado hakuna mwenye uhakika, tupo ukurasa mmoja hapa watu wa magazeti!
 
JF na kujulikana kote kwa watu walioko karibu na Ballali, kweli tungeshindwa kupata copy? Eti copy inapelekwa IMF? Mimi haiingii akilini.

Mimi swala la copy kulindwa siliafiki, inawezekana kuandika lakini nafikiri ngoma yote aliondoka nayo labda Mukono ambaye pia ni mfanya biashara mzuri.

Sina uhakika kama tutapata kitu tena.
 
Duh! JF bwana kweli tuko mbali sana, yaani hizi dataz tulizimwaga last two weeks wao ndio kwanza wamezipata saa hizi, anyways saafi sana inaonyesha tu JF ni mambo yote!

Wakuu wangu mpo hapa, Jf mbele zaidi! Alyways one step ahead, kwa nyongeza tu ni kwamba aliacha pia tape records na hizo documents kuna ambazo ziko kwa wakulu wa IMF na World Bank, ila effectiveness yake bado hakuna mwenye uhakika, tupo ukurasa mmoja hapa watu wa magazeti!

FMES,

Niliposoma tu nikasema naijua hii source, ni FMES kwi kwi kwi!!!!
 
Ukisoma vizuri hii habari, hakuna jipya zaidi ya yale ambayo yaliandikwa hapa JF na Mzee Mwanakijiji na pia FMES.

Mwanzo ilikuwa kwamba eti anajilinda yeye, sasa wanasema aliogopa familia yake kusumbuliwa.

Nafikiri tunaendelea kurushiwa changa la macho.

Siamini kabisa habari yoyote ya Ballali mpaka watoe hizo video. Yeye kapotea, wanaogopa nini kuzitoa kama zipo?

JF na kujulikana kote kwa watu walioko karibu na Ballali, kweli tungeshindwa kupata copy? Eti copy inapelekwa IMF? Mimi haiingii akilini.

Kaka Mtanzania na si Video tu!,Kuna maelezo kuwa kuna hata Documents nyingine muhimu Mzee Balalli aliziacha mikononi mwa watu ikiwa ni Ushahidi wa kuonyesha nini kilitokea kwenye a/c ya EPA.Kwa Taarifa kuna jamaa wanazitafuta Docs hizo,kwa ufahamu wangu nimeambiwa Mbwiga hao wapo DC,Watakwenda New York na South Carolina.Hao jamaa wamekuja kutoka Tanzania kwa kazi hiyo...Kuna kitu kinafichwa hapa,hawa watawala wanaogopa hizi docs zisipite mikononi mwa akina Halisi kwa sababu zitawekwa wazi hapa...hata wafanye nini ukweli wa kifo cha Balalli utakuwa wazi tu....
 
Heshima kwa JF mkuu sio mimi lol! JF juu zaidi maana vitu huanzia hapa Mkuu wangu Kuhani Mkuu mzee wa bazee unasikia hii kutoka kwa station FMES maneno mbele, kumkoma nyani giladi wallahi I Love JF!

Mkuu wangu Mtanzania tuendelee kumkoma nyani nilisema mkuu siku hiziz dataz mpaka taifa sio local tu, lakini tisa yote kumi JF zaidi, always one step ahead!

Love JF!
 
Kaka Mtanzania na si Video tu!,Kuna maelezo kuwa kuna hata Documents nyingine muhimu Mzee Balalli aliziacha mikononi mwa watu ikiwa ni Ushahidi wa kuonyesha nini kilitokea kwenye a/c ya EPA.Kwa Taarifa kuna jamaa wanazitafuta Docs hizo,kwa ufahamu wangu nimeambiwa Mbwiga hao wapo DC,Watakwenda New York na South Carolina.Hao jamaa wamekuja kutoka Tanzania kwa kazi hiyo...Kuna kitu kinafichwa hapa,hawa watawala wanaogopa hizi docs zisipite mikononi mwa akina Halisi kwa sababu zitawekwa wazi hapa...hata wafanye nini ukweli wa kifo cha Balalli utakuwa wazi tu....

Mwawado,

Ndugu yangu endelea kusubiri hiyo mikanda. Ukiwa na muda rudi kwenye threads zote za Ballali kuanzia mwezi wa tisa mwaka jana, mpangilio ni ule ule, kuna kampeni za kuwadanganya Watanzania.

Hata mimi nilikuwa nasubiri ya Ballali, ila sasa sisubiri tena maana aliyedanganya mara tisa utamwamini mara ya kumi?

Eti kaacha copy IMF? Kwi kwi kwi!!!, kwanini azunguke kote huko mbali? Hata watunza EPA wanajua kuna JF. Wana risk kazi na maisha yao kuleta hizo habari JF, jamaa aliyekuwa anakufa eti kaona chombo muhimu ni IMF, changa la macho hilo.
 
Mimi nafikiri mtoe hoja za msingi wana JF wana sifa za kusema kweli na wala siyo habali za kubuni mwaga data na siyo hekeya za abunuwasi
 
Narudia swali nililouliza kwenye thread inayofanana na hii

Hivi kweli inaingia kichwani kwamba Balali ange shoot video ya ushahidi badala ya kuuambia umma ukweli wa mambo?
 
zamani nilikuwa naamini kuwa kwenye mwezi kuna mwana mama ambaye ana mtoto mgongoni na amebeba kuni. Nilisimuliwa kuwa hiyo ilikuwa ni adhabu ya kufanya kazi "jumapili". Katika jamii nyingine watu huamini kuwa mwezi umetengenezwa kwa jibini..au samli .. hivyo utakuta kuwa imani kuhusu mwezi ziko za aina nyingi na zinazotofautiana sana.

Baada ya kusoma elimu ya geologia na mambo ya sayari.. na kuzidi kujua jinsi ulimwengu ulivyounda tangia ule "Mlipuko Mkuu" nimeacha kuamini mambo ya mama na kuni zake kwenye mwezi.
 
Back
Top Bottom