Mkuu Heshima mbele,
Wale wote wenye hizo dataz sio wajinga, na haiwezekani wote tukawa waongo kuhusu kuwepo kwake, kuanzia mimi, Mwawado, mpaka Indume Yene yaani wote tume-co-ordinate kwa pamoja ku-create huu uongo?
Kila kitu kina wakati wake, ninaamini in due time zitamwagwa hapa, ingawa kumwagwa ni one thing na context zake ni another ishu! Lakini ninaamini kuwa zinakuja hapa sooon!
Mkuu FMES,
Unajua maana ya SPIN? Huenda source ya hizo info au data zenu zote ni mtu mmoja ambaye amekaa chini na kunywa whisky yake akishangilia kudanganya Watanzania.
Labda niulize swali lingine, kati ya nyie nyote kuna mtu ameona hizo video?
Mwanzoni niliuliza kati ya wote wanaosema Ballali amekufa, kuna mtu anaweza au amewahi kusema publically kwamba kauona mwili? Naona hakuna jibu.
Hai make sense kwamba miezi tisa aliyokuwa nayo Ballali hakusema kitu kuhusu alivyoshirkiana na wengine kuchota pesa zetu, eti wakati anakaribia kutoroka kimoja ndio
anatengeneza video na kuzisambaza sehemu mbalimbali.
Pia hakuna siri ya watu kumi, laiti Ballali angeacha copies zote hizo, leo hii hapa JF tungelikuwa na copy.
Mimi naamini huo ni uwongo mwingine dhidi ya Watanzania ambao unaanzia kule kule juu yaani kwa mama Muganda. Ni yale yale ya sumu Dodoma au Othman kushangaa eti Ballali hajafa, hivi kweli inaingia kichwani, mtu anakuja kukuona, kisha anakuambia anashangaa hujafa?
Nyingine ni Ballali kutumiwa na makachero watano sijui saba, kama kweli Othman alijua alikokuwa Ballali, kweli hao makamanda wake iweje wasijue mpaka waanze kuvinjari USA nzima kumtafuta? Kuna mtu anasema walitumwa na Apson, lakini labda hawajui kwamba
Othman ni mtoto wa Apson (kimpangilio), wanaelewana mno, haiwezekani kwamba yeye anajua kitu, boss wake wa zamani anataka kujua na akafichwa. Eti alionwa na Othman zamani, na akahama, mtu anayesema hivyo hajui hawa makachero wanavyofanya kazi, wakishajua ulipo ni ngumu sana kuwapoteza. Kama kweli Othman alimwona basi jua hapo
aliacha vijana wake karibu wakipumua mgongoni mwa Ballali.
Hii habari nzima hai make sense.