Wosia wa Mirathi ya Dkt. Reginald Mengi: Jacqueline Ntuyabaliwe adondokea pua

Wosia wa Mirathi ya Dkt. Reginald Mengi: Jacqueline Ntuyabaliwe adondokea pua

Kesi Ya Mirathi ya ya Dr. Reginald Mengi: Former Miss Tanzania Jackline Ntuyabaliwe adondokea pua kwa Mara Ya nane tena katika Rufaa

View attachment 1790872

Mahakama Kuu ya Tanzania Masijala ya Dar es Salaam imetoa uamuzi kuwa mtoto wa Marehemu Reginald Mengi;-Abdiel na kaka wa marehemu, Bw. Benjamin Mengi kuwa wasimamizi wa mirathi ya mali alizoacha marehemu (Reginald Mengi). Katika uamuzi huo, mahakama imeagiza usimamizi na mgawanyo wa mirathi uanze mara moja.

Akisoma hukumu hiyo yenye kurasa 72 mnamo Mei 18/2021 Jaji Mlyambina alisema kuwa wosia wa mwisho wa Marehemu Dkt. Mengi ulioandikwa Agosti 17,2017 haukuzingatia misingi ya kisheria ya uandishi wa wosia.

Katika shauri hilo watoto wa marehemu Dkt. Mengi walikuwa wakipinga wosia uliodaiwa kuachwa na Marehemu baba yao kwa madai kwamba wosia huo haukufungwa ‘sealed’ na saini iliyopo kwenye wosia huo ni tofauti na sahihi zingine za Marehemu na pia kwa wakati huo baba yao hakuwa na uwezo wa kuandika kutokana na matatizo makubwa ya kiafya aliyokuwa nayo tangu mwaka 2016.

Aidha watoto hao walidai kuwa wosia uliwabagua na urithi wote aliachiwa mkewe mpya na watoto mapacha na hivyo wosia huo ulikuwa kinyume na sheria sababu uliwabagua watoto bila sababu za msingi na za kisheria.

=====

Dar es Salaam. Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imeukataa wosia uliokuwa ukidaiwa kuandikwa na aliyekuwa mfanyabiashara maarufu nchini marehemu Reginald Mengi pamoja na mambo mengine ikieleza kuwa haukidhi matakwa ya kisheria ili kuwa wosia halali.

Uamuzi huo ulitolewa jana na Jaji Yose Mlyambina kufuatia shauri la mirathi lililokuwa limefunguliwa na watu wanne wakiwemo ndugu wa marehemu, wakiomba kuteuliwa kuwa wasimamizi wa mirathi hiyo.

Jaji Mlyambina amefikia uamuzi huo baada ya kukubaliana na hoja za pingamizi lililowekwa na mmoja wa watoto wakubwa wa marehemu Mengi pamoja na ndugu yake marehemu Mengi, waliokuwa wakipinga uhalali wa wosia huo.

Shauri hilo la mirathi namba 39 la mwaka 2019 lilifunguliwa na Benson Benjamin Mengi, William Onesmo Mushi, Zoebu Hassuji na Sylvia Novatus Mushi wakiomba kuteuliwa kuwa wasimamizi mirathi hiyo kwa mujibu wa wosia huo.

Hata hivyo, mtoto wa Marehemu Mengi, Abdiel Reginald Mengi na ndugu wa marehemu Mengi, Benjamin Abraham Mengi, waliweka pingamizi dhidi ya wosia huo, wakipinga uhalali wake huku wakiwasilisha jumla ya sababu nne za kuupinga.

Sababu hizo ni pamoja na kwamba haukwa umepigwa mhuri na saini iliyokuwepo ilikuwa ni tofauti na saini ya kawaida ya marehemu Mengi na kwamba haukushuhudiwa na ndugu au mke wa marehemu.

Pia walikuwa wakidai kuwa marehemu hakuwa na uwezo wa kuandaa wosia kwa kuwa alikuwa na matatizo ya kiafya tangu mwaka 2016 na kwamba unaondoa katika urithi, watoto bila kuzingatia mila za Kichaga au kuhusisha ndugu.

Mahakama Kuu baada ya kusikiliza hoja za pande zote katika hukumu yake iliyosomwa juzi na Jaji Mlyambina na nakala yake kupatikana jana kwa matumizi ya umma, alikubaliana na hoja za pingamizi hilo dhidi ya wosia huo na kuikataa kuwa ni batili.

Jaji Mlyambina alikubaliana na sababu hizo za pingamizi na pamoja na mambo mengine, amesema kuwa inawanyima urithi wanaye bila kutoa sababu, na kwamba ziliiingizwa mali za mke wake mkubwa.

Kwa uamuzi huo, Jaji Mlyambina hakuwateua waombaji hao kuwa wasimamizi wa mirathi na badala yake aliwateua Abdiel na Benjamini kuwa wasimamizi wa mirathi na akaelekeza mali za marehemu zigawiwe warithi wanaostahili kwa utaratibu wa kawaida kama wa mtu ambaye hakuacha wosia.

Awali mjane wa marehemu Mengi, Jacquiline alijaribu kuingia katika shauri hilo bila mafanikio baada ya mahakama hiyo kutupilia mbali maombi yake mara tatu.

Credit: Mwananchi

Zaidi soma;

1). Thread 'Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi: Nimezuiwa kuingia kwenye kaburi la mume wangu. Nimechoka na sitakubali' Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi: Nimezuiwa kuingia kwenye kaburi la mume wangu. Nimechoka na sitakubali

2). Thread 'Hatimaye K Lyn (Jacqueline Ntuyabaliwe) achumbiwa na Reginald Mengi' Hatimaye K Lyn (Jacqueline Ntuyabaliwe) achumbiwa na Reginald Mengi

3). Thread 'Watoto wa Mengi wamburuza mahakamani Jacqueline Mengi "Klynn"' Watoto wa Mengi wamburuza mahakamani Jacqueline Mengi "Klynn"

4). Thread 'Unaodaiwa kuwa wosia wa Reginald Mengi huu hapa, mali zote ni za Jacqueline na watoto wake mapacha' Unaodaiwa kuwa wosia wa Reginald Mengi huu hapa, mali zote ni za Jacqueline na watoto wake mapacha

5). Thread 'Miaka 5 ya Anniversary ya Reginald Mengi na Jackline Mengi wote wafunguka' Miaka 5 ya Anniversary ya Reginald Mengi na Jackline Mengi wote wafunguka

6). Thread 'TANZIA: Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Abraham Mengi afariki dunia akiwa Dubai, UAE' TANZIA: Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Abraham Mengi afariki dunia akiwa Dubai, UAE
Hivi mtu akighushi wosia kunakuwa na dhabu gani? au anatakiwa achukuliwe hatua za kisheria zipi?
 
Hivi mtu akighushi wosia kunakuwa na dhabu gani? au anatakiwa achukuliwe hatua za kisheria zipi?
Jk ndo anazingua hapa na wema wake na ustaarabu[emoji23][emoji23] hili kahana lina mengi yanamuelemea basi tu watanzania ni wakarimu
 
Huyu dada kashindwa kutafuta hela zake mwenyewe, anataka kutumbua za huyu Mzee wa watu aliyechuma miaka nenda rudi tena kwa shida kubwa.
Dada alijisahau sana tena sana, kile kitendo cha kuishi tu na Mzee machache kilimtosha yeye mwenyewe na watoto wake kutokutegemea urithi, mambo ya kughushi urithi ni sawa na mtu ambaye ni muuaji kwa kuwa alitegemea akimua marehemu atachukua urithi wa mali. Sijui kile kiwanda cha Amore kimeishia wapi masikini.
 
Coz I’m on a whole different galaxy when it comes to this shit.

I’m a wordsmith!

You can call me Mr. Smith.
Well.... I guess i gosta come up with my presentation statement haaah,................ i mean am a real Mac from way back, one of the original player from the Himalayas...... [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Well.... I guess i gosta come up with my presentation statement haaah,................ i mean am a real Mac from way back, one of the original player from the Himalayas...... [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Nigga, stop it. You sound corny as fcuk.

Cut that shit, man.
 
Yaani alikosa washauri kbs yule dada .
Ila hata sasa naona bado anapenda maisha ya uslay sana...uwii umri w 40 yrs jaman uslay wa nn!
Hakuna maisha mengine anayoyajua. Wewe kama akina Wema kuna siku watabadilika wale?. Wanahisi umri unabaki hapo hapo. Tena ningekuwa ndio mimi mtoto mkubwa wa Mengi nilieshinda mirathi aendelee kumbana na pande zingine zote mpaka abakie na manyoya tu.
 
Ila ni haki yao yule ni baba yao. Na hao madogo ni wadogo zao so hata iweje hao ni ndugu hawawezi kuwatupa wadogo zao.
Ni sawa. Nadhani Mzee Mengi akutazama hivyo. Tatizo ni baba mdogo na familia za zingine za kando yaani ndugu wa Mzee.
 
Ila ni haki yao yule ni baba yao. Na hao madogo ni wadogo zao so hata iweje hao ni ndugu hawawezi kuwatupa wadogo zao.
Kilichoandikwa my frnd. Na mashosty wanazengea. Ndugu awana neno. Shida ni baba mdogo na washangazi. Watoto awanashida
 
Ukiisoma andaa na panadol kabisa..... Maana ile English ni ya ajabu balaa.
Niwekee hapa niisome nione huo upuuzi wa mwanamke mwenzetu.

Mdada huyu hana shukrani, mengi alimstili akampa heshima ya ndoa kwa nini asijifunze kula na kipofu?

Ningekuwa mm baada ya kifo cha mengi ningekaa kimya wagawe watakachoona kinanifaa na wanangu watanipa.

Mjina sana anawezaje kusema kuwa mengi hakuwapa watoto wake wakubwa mali? Kwahiyo wanae ndo watoto tu?

Mimi siwezi ingia tamaa ya namna hiyo.
 
Mengi alikuwa na misunderstandings na familia yake kwa mke wa kwanza, sijui kama walimalizana hizo tofauti ila zilikuwapo.
Hivi ni kweli misunderstandings hizo ndo zipelekee Mzee kuwatoa watoto wake kwenye urithi???mchaga wa wapi huyo anaweza fanya ivyo...
 
Back
Top Bottom