Wosia wa Mirathi ya Dkt. Reginald Mengi: Jacqueline Ntuyabaliwe adondokea pua

Wosia wa Mirathi ya Dkt. Reginald Mengi: Jacqueline Ntuyabaliwe adondokea pua

Jewelry 92% wanazifanya wenzetu wahindi sijui tunafeli wapi waafrica...yaan kuutwa alikua anashinda na wale maslayqueen wake kujiselfie aisee mm mwaka mmoja nasimamisha bonge ya kampuni ..unachakarika had unahakikisha inesimama .naudhika sana na aina ya wanawake aina ile ..
Ningehakikisha nna vitalu vya uchimbaji eneo kubwa, vitalu ya uwindaji eneo lankutosha yaan sehemu zenye fweza angesimamisha kampuni za maana...mafala tu wale
Ujuaji wako tu unafikiri vinapatikana kirahisi? Hata kama Mengi alikuwa boya sio namna hiyo
 
Hoja 1: ni usimamizi wa mirathi

Hoja 2:mgawanyo ufanyike kwa wahusika wote mara moja ikiwa ni pamoja na huyo mrembo.

Mytake:sasa shida iko wapi maana naona wachangiaji wote wanamshambulia jack.

Hakuna mchangiaji hata mmoja aliyeelewa tafsiri ya hiyo hukumu....over
Jaçk atapewa kitachomsababishia stress

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ata-enjoy urithi wa watoto wakati ameshazeeka!!!

Kwavile ameshaonesha makucha hatari since Day One, LAZIMA atachaguliwa mtu mwingine kuwa Msimamizi wa mali za watoto hadi watakapofika 18 or even 21. Na kwavile watoto bado wadogo sana, inaweza kufunguliwa hata formal trust ili kuhakikisha mali za watoto hazipotei!

Na kwavile ameshaonekana ni nyoka, there's no way huo usimamizi akaja kupewa Jack... sana sana atatafutwa kutoka miongoni mwa Ukoo wa Mengi!
Kaka zao wapo watasimamia show

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa inawakuwaje watoto waliozaliwa na jaq wanatambuliwa ila mama(jaq) wamtenge? Sheria si zinasema mkishakaa na m/ke(me) zaidi ya miezi sita ni mkeo/mme by default.
Hata Jaq anatambuliwa, mgao bado hawajagawana. Hata ukae na mwanamke miaka 20 bila kufunga ndoa huyo sio mke wako, hilo unalosema ni stori za mtaani tu.
 
Mahakama imetenda haki.

Kwenye kile kifungu kwenye wosia eti atakae jaribu kuweka pingamizi kwenye maamuzi aliyoyatoa marehemu mzee mengi iwapo atashinda kesi apatiwe Buku. Ndio nilijua wanawake wa kuokoteza uzeeni sio wazuri
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]

Sent from my Nokia 3.2 using JamiiForums mobile app
 
Hata Jaq anatambuliwa, mgao bado hawajagawana. Hata ukae na mwanamke miaka 20 bila kufunga ndoa huyo sio mke wako, hilo unalosema ni stori za mtaani tu.

Mkuu mtafute mwanasheria akupe updates kuhusu kukaa na mwanamke miezi 6 hata kama mjafunga ndoa.
 
Case Ya Mirathi ya ya Dr. Reginald Mengi: Former Miss Tanzania Jackline Ntuyabaliwe adondokea pua kwa Mara Ya nane tena katika Rufaa

View attachment 1791249
View attachment 1790872

Mahakama Kuu ya Tanzania Masijala ya Dar es Salaam imetoa uamuzi kuwa mtoto wa Marehemu Reginald Mengi;-Abdiel na kaka wa marehemu, Bw. Benjamin Mengi kuwa wasimamizi wa mirathi ya mali alizoacha marehemu (Reginald Mengi). Katika uamuzi huo, mahakama imeagiza usimamizi na mgawanyo wa mirathi uanze mara moja.

Akisoma hukumu hiyo yenye kurasa 72 mnamo Mei 18/2021 Jaji Mlyambina alisema kuwa wosia wa mwisho wa Marehemu Dkt. Mengi ulioandikwa Agosti 17,2017 haukuzingatia misingi ya kisheria ya uandishi wa wosia.

Katika shauri hilo watoto wa marehemu Dkt. Mengi walikuwa wakipinga wosia uliodaiwa kuachwa na Marehemu baba yao kwa madai kwamba wosia huo haukufungwa ‘sealed’ na saini iliyopo kwenye wosia huo ni tofauti na sahihi zingine za Marehemu na pia kwa wakati huo baba yao hakuwa na uwezo wa kuandika kutokana na matatizo makubwa ya kiafya aliyokuwa nayo tangu mwaka 2016.

Aidha watoto hao walidai kuwa wosia uliwabagua na urithi wote aliachiwa mkewe mpya na watoto mapacha na hivyo wosia huo ulikuwa kinyume na sheria sababu uliwabagua watoto bila sababu za msingi na za kisheria.

=====

Dar es Salaam. Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imeukataa wosia uliokuwa ukidaiwa kuandikwa na aliyekuwa mfanyabiashara maarufu nchini marehemu Reginald Mengi pamoja na mambo mengine ikieleza kuwa haukidhi matakwa ya kisheria ili kuwa wosia halali.

Uamuzi huo ulitolewa jana na Jaji Yose Mlyambina kufuatia shauri la mirathi lililokuwa limefunguliwa na watu wanne wakiwemo ndugu wa marehemu, wakiomba kuteuliwa kuwa wasimamizi wa mirathi hiyo.

Jaji Mlyambina amefikia uamuzi huo baada ya kukubaliana na hoja za pingamizi lililowekwa na mmoja wa watoto wakubwa wa marehemu Mengi pamoja na ndugu yake marehemu Mengi, waliokuwa wakipinga uhalali wa wosia huo.

Shauri hilo la mirathi namba 39 la mwaka 2019 lilifunguliwa na Benson Benjamin Mengi, William Onesmo Mushi, Zoebu Hassuji na Sylvia Novatus Mushi wakiomba kuteuliwa kuwa wasimamizi mirathi hiyo kwa mujibu wa wosia huo.

Hata hivyo, mtoto wa Marehemu Mengi, Abdiel Reginald Mengi na ndugu wa marehemu Mengi, Benjamin Abraham Mengi, waliweka pingamizi dhidi ya wosia huo, wakipinga uhalali wake huku wakiwasilisha jumla ya sababu nne za kuupinga.

Sababu hizo ni pamoja na kwamba haukwa umepigwa mhuri na saini iliyokuwepo ilikuwa ni tofauti na saini ya kawaida ya marehemu Mengi na kwamba haukushuhudiwa na ndugu au mke wa marehemu.

Pia walikuwa wakidai kuwa marehemu hakuwa na uwezo wa kuandaa wosia kwa kuwa alikuwa na matatizo ya kiafya tangu mwaka 2016 na kwamba unaondoa katika urithi, watoto bila kuzingatia mila za Kichaga au kuhusisha ndugu.

Mahakama Kuu baada ya kusikiliza hoja za pande zote katika hukumu yake iliyosomwa juzi na Jaji Mlyambina na nakala yake kupatikana jana kwa matumizi ya umma, alikubaliana na hoja za pingamizi hilo dhidi ya wosia huo na kuikataa kuwa ni batili.

Jaji Mlyambina alikubaliana na sababu hizo za pingamizi na pamoja na mambo mengine, amesema kuwa inawanyima urithi wanaye bila kutoa sababu, na kwamba ziliiingizwa mali za mke wake mkubwa.

Kwa uamuzi huo, Jaji Mlyambina hakuwateua waombaji hao kuwa wasimamizi wa mirathi na badala yake aliwateua Abdiel na Benjamini kuwa wasimamizi wa mirathi na akaelekeza mali za marehemu zigawiwe warithi wanaostahili kwa utaratibu wa kawaida kama wa mtu ambaye hakuacha wosia.

Awali mjane wa marehemu Mengi, Jacquiline alijaribu kuingia katika shauri hilo bila mafanikio baada ya mahakama hiyo kutupilia mbali maombi yake mara tatu.

Credit: Mwananchi

Zaidi soma;

1). Thread 'Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi: Nimezuiwa kuingia kwenye kaburi la mume wangu. Nimechoka na sitakubali' Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi: Nimezuiwa kuingia kwenye kaburi la mume wangu. Nimechoka na sitakubali

2). Thread 'Hatimaye K Lyn (Jacqueline Ntuyabaliwe) achumbiwa na Reginald Mengi' Hatimaye K Lyn (Jacqueline Ntuyabaliwe) achumbiwa na Reginald Mengi

3). Thread 'Watoto wa Mengi wamburuza mahakamani Jacqueline Mengi "Klynn"' Watoto wa Mengi wamburuza mahakamani Jacqueline Mengi "Klynn"

4). Thread 'Unaodaiwa kuwa wosia wa Reginald Mengi huu hapa, mali zote ni za Jacqueline na watoto wake mapacha' Unaodaiwa kuwa wosia wa Reginald Mengi huu hapa, mali zote ni za Jacqueline na watoto wake mapacha

5). Thread 'Miaka 5 ya Anniversary ya Reginald Mengi na Jackline Mengi wote wafunguka' Miaka 5 ya Anniversary ya Reginald Mengi na Jackline Mengi wote wafunguka

6). Thread 'TANZIA: Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Abraham Mengi afariki dunia akiwa Dubai, UAE' TANZIA: Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Abraham Mengi afariki dunia akiwa Dubai, UAE
Rasmi sasa JAQ MENGI kuungana na genge la kina SEPENGA, UWOYA na AMBER RUTTY kutumia reslimali yake kupata kipato maana alizoeshwa na yule mchagga maisha ya juu sana.
 
Huyu dada kashindwa kutafuta hela zake mwenyewe, anataka kutumbua za huyu Mzee wa watu aliyechuma miaka nenda rudi tena kwa shida kubwa.
1621486177949.png

Halafu anamwita baby
Dunia imepinda kwakweli
 
Back
Top Bottom