Mkuu.. ujue nimejaribu kufikiria juu ya hoja ya kukosa hofu ya Mungu. Hivi unadhani mtu akiwa na hofu ya Mungu kweli anaweza kufanya hivi? Ujue inahitaji roho ya kikatili sana? Ujue sisi ni wadhambi, siyo malaika. Lakini kuna matukio yanaogopesha sana. Mtu ukiwa na hofu ya Mungu sidhani kama unaweza fanya dhuluma hivi. Jamani... mume wangu hata awe bilionea vipi, yaan kama ni jasho lake wallah sitokaa niwahi jifikirisha ni sehemu ya mali zangu. Sitaki kabisa. Awape watoto wake. Nitahesabu kitu ni chetu endapo tu tutafanya mradi pamoja. Hilo tuu. Lakini hata tuwemo kwenye ndoa sishtuki haataaa... one day nilimweleza mama yangu, akiona anakaribia kufa awagawie wanaye wawili mali zake ama auze[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] au nitakua si mchagga ndugu yangu. Hapa tu ndo naposhushuliwa. Mali za watu ambazo sijazitolea jasho hazilegezi kabisa mshipa wangu wa wowowo... naamini hofu ya Mungu ndo kila kitu