Wote walioteuliwa aidha wanakaa ama wanatoka Dar es Salaam

Kwahiyo wanaoishi mikoani ni mambumbumbu?

Mkuu hilo neno linakera lakini ndio ukweli wenyewe. Na sio kuwa viongozi wanatokea na kuishi hapa Dar tu,bali hata sheria zote za nchi zinatungwa hapa hapa Dar, deal zote kubwa zinaanzia hapa Dar na kwenda kutekelezwa tu huko mikoani, na hata wasimamizi wa hizo deals ni watu wa hapa Dar.
 
Hii inafikirisha sana. Hivi inawezekanaje jambo hili.

Kwamba nchi nzima watu wenye uwezo kuongoza wanatoka au kukaa Dar pekee.

Pia uteuzi umeshindwa kubalance makundi ya kijamii. Tunajua haiwezi kuwa balanced 100% lakini je haya makundi yatawakilishwa na nani maana ndio proportion kubwa ya wananchi mathalani:

1. Walimu
2. Wakulima
3. Wafugaji
4. Wafanyabishara
Makundi yanayodharaulika hapa kwetu Ni hao.
1. Walimu. Angalia maslahi yao, mazingira ya kazi . Wanafunzi zaidi ya Mia kwa drs. Nyumba zao vijijini hata hapo Dar.
2. Wakulima. Angalia asilimia ya kilimo kwenye bajeti. Angalia Bei ya bidhaa zao. Ulisha wahi kuona fungu la mihogo au viazi vitamu la elfu moja Dar lilivyo kubwa. Huko mikoani si ni balaa
3. Tanzania Kuna wafugaji?
4. Wafanyabiashara .
Tanzania wanaoheshimika Ni watangazaji wa fm radios na tiivii, wasanii, watu wa ofisini walimbwende na mapolisi.
Wastaafu ndio kabisa hatujulikani
 
Tatizo kubwa mfumo wa vetting Sio mzuri, watu wanafanyiwa vetting ikiwa majina na connections tayari. Kujuana Ni kwingi zaidi kuliko uwezo wa mteuliwa..
 
Hakuna uteuzi ni mwiba wa moto kwa bavicha kama huu
 
Mkuu hilo neno linakera lakini ndio ukweli wenyewe. Na sio kuwa viongozi wanatokea na kuishi hapa Dar tu,bali hata sheria zote za nchi zinatungwa hapa hapa Dar, deal zote kubwa zinaanzia hapa Dar na kwenda kutekelezwa tu huko mikoani, na hata wasimamizi wa hizo deals ni watu wa hapa Dar.
Mbunge hata kama ni wa katavi lakini anaishi Dar.
 
Nafasi za uteuzi zina ushawishi wa kisiasa,na uzoefu wa mifumo ya kiserikali.

Aidha anayeteua yupo Serikalini,kwenye chama muhimu "Unayeteuliwa uwe umejihusisha na mambo mawili(Serikali au Chama),kama utapata uteuzi kutokea nyanja nyingine,basi itakuwa ni utashi wa anayeteua viongozi.

Mambo ya Serikali ni "Siri kali",yaone hivyo hivyo!,kama haujabahatika kupata uteuzi,jitahidi kupigania mlo wa familia yako hilo ndio muhimu.
Watanzania tunakadiriwa kufikia milioni 60,inabidi wapate wachache,watuwakilishe kwa niaba ya wengi tunaokosa nafasi.

Kama una watoto wadogo waandae kisaikolojia kuwa viongozi na watawala,maana walioongoza taifa hili siku za nyuma bado wanaendelea kupeana nafasi kwa watoto wao.(Tutatawaliwa hadi kizazi cha 3,ndipo tutaondoa hiyo staili ya wastaafu kurithisha watoto wao madaraka kwenye nafasi kubwa za madaraka).
85% mapato ya nchi yapo Dar sasa uende mbali channel ya mzunguko pesa? Shauri yako utapishana gari mshahara
 
Hii inafikirisha sana. Hivi inawezekanaje jambo hili.

Kwamba nchi nzima watu wenye uwezo kuongoza wanatoka au kukaa Dar pekee.

Pia uteuzi umeshindwa kubalance makundi ya kijamii. Tunajua haiwezi kuwa balanced 100% lakini je haya makundi yatawakilishwa na nani maana ndio proportion kubwa ya wananchi mathalani:

1. Walimu
2. Wakulima
3. Wafugaji
4. Wafanyabishara
Anaandika Diwani wa Kata ya Kongolo- Magu na Mwanafalsafa Ndugu Herbet Faustine
__________________________

RAIS SAMIA ALITEGEMEA KUKUTANA NA NDOTO ZA MABILIONEA NYAMAGANA, KAKUTANA NA WAGOMBEA MIRATHI.

Rais Samia Suluhu Hassan kamaliza ziara yake mkoani Mwanza kwa kuzungumza na vijana wa taifa hili kupitia vijana wa mkoa wa Mwanza na Kanda ya ziwa kwa ujumla. Namshukuru Mungu kuna michuano ya soka huko Ulaya inaendelea ikatufanya tusahau yaliyojiri Nyamagana.

Tusidanganyane, tulichokiona Nyamagana ndiyo taswira ya vijana wa taifa hili walio wengi, wasomi kwa wasio soma tofauti kwenye ujenzi wako sawa. James Mbatia alipolalamikia mitaala ya elimu kipindi chote alipokuwa Bungeni alionekana hana maana! Katuumbua.

Rais Samia Suluhu Hassan alitoa fursa za vijana kuongea nae, waseme changamoto zao, nchi hii ni kubwa, nchi ina mambo mengi, Rais si nabii wa kujua kwenye mifugo kuna shida gani, kwenye uvuvi kuna matatizo gani, kwenye madini kuna nini, Rais akataka kujua kwenye kilimo kipi kinawapa taabu vijana kuwa mabilionea kupitia kilimo.! Je ni mbegu za GMO? Uhaba wa masoko? Rais aliwaza mbali kuliko vijana wenyewe.

Kwanini vijana? Nguvu ya uchumi wa nchi iko kwa vijana! Kama kuna fursa za kiuchumi zinahitajika kulisukuma taifa mbele basi fursa hizo zinawalenga vijana. Mama akatenga penalti wapige, vijana si tu wamepaisha ila kwa uwakilishi ule penalti imepigwa ikawa mpira wa kurusha.

Tatizo ni nini? Vijana walio wengi maono yao ni namna gani wapate hela ya kula na kunywa. Hela hii haihitaji sana uwekezaji wa muda mrefu bali maono ya muda mfupi. Akili hizi zimewekezwa kwenye teuzi. Vijana wateuliwe u DC, U RC, u DAS. Aibu🙈

Rais alitegemea kukutana na hoja za vijana zinazoonesha namna gani vijana wapatiwe fursa za mitaji, misamaha ya kodi kwenye baadhi ya vitu kama matrekta ya kilimo, mikopo isiyo na masharti magumu kwenye taasisi za kifedha.

Nyamagana Rais Samia alitegemea kukutana na hoja zenye kuonesha miaka hamsini ijayo taifa liwe la aina gani, mama akakutana na hoja za namna gani walioteuliwa wanaendelea kuaminiwa nae kwenye nafasi zao, na wale wasioteuliwa wanaingiaje kwenye nafasi za kuteuliwa mana wanajua kuna nafasi hizo😳🙈.

Ukisikiliza hoja za pale Nyamagana mbele ya Rais unaona kabisa Rais alikuja kusikiliza hoja za mabilionea watarajiwa ila ajabu akakutana na hoja za wagombea mirathi. Mama akafa moyo, kwenye hotuba akaanza kufafanua mpaka dhana nzima ya ujana! Ukimsikiliza Rais kwenye maana ya ujana utaona kuwa badala ya kuongea na vijana, alianza kutoa semina elekezi. Mwisho akakidhi matarajio yao ya muda mfupi, akawambia kuna mkeka wa wakuu wa wilaya unakuja. Wakashangilia.

Pale Kenya wiki hii wamempoteza bilionea Christopher Kirubi kwa saratani. Watanzania tarehe 15 June 2021 tumepoteza mabilionea Nyamagana kwa uwezo wa kufikiri. Christopher Kirubi alitaka kuwa bilionea akawekeza kwa kutumia fursa za nchini kwake, vijana wa Watanzania wanataka kuitwa mheshimiwa mkuu wa wilaya wamewekeza kwenye kujipendekeza.

Angalia jumuia za vyama vya siasa za makundi ya vijana. Hazina maono. Wakipata fursa ya kuongelea jambo mwisho wa hotuba lazima uulize ana elimu gani huyu mtu. Ukiambiwa elimu yake bado unahoji alipataje hii nafasi.

Nchi nzima inakusikiliza unapewa kisemeo unaanza kusema Mheshimiwa Rais sisi vijana tunakuunga mkono. Baada ya kumuunga mkono kinafuata nini? Aliyekuuliza nani? Mama kasema anawateua kutegemea na bidii yenu ya kusifu na uimbaji pambio?

Kundi hili la vijana ndilo lenye watu wasomi, lakini, nasema tena lakini, ikitokea mheshimiwa Rais akakutana na kundi la Mama Ntilie, ndiyo utaona tofauti ya elimu maisha na elimu teuzi.
 
Hii inafikirisha sana. Hivi inawezekanaje jambo hili.

Kwamba nchi nzima watu wenye uwezo kuongoza wanatoka au kukaa Dar pekee.

Pia uteuzi umeshindwa kubalance makundi ya kijamii. Tunajua haiwezi kuwa balanced 100% lakini je haya makundi yatawakilishwa na nani maana ndio proportion kubwa ya wananchi mathalani:

1. Walimu
2. Wakulima
3. Wafugaji
4. Wafanyabishara
Hili swala liangaliwe aisee kwenye teuzi zijazo kusiwe na double standard Kama Ni chama kinapiganiwa na makundi mbali mbali kwaio kigezo ukiwa Ni kada wa chama wanaofanya vetting waangalie maeneo mbali mbali ya hii nchi ya hii nchi sio hao celebrity na waandishi tu wanaokidhi dar es salaam.
 
Watu wenye huitaji maalum naona kwenye teuz nyingi wanasahaulika
Kuna mmoja aliwahi kupewa nafasi alikuwa na ulemavu wa ngozi( albumino) yeye kila kukicha na kuchwa ni mapambio tu hadi akasahau kuwa amepewa nafasi kuwakilisha walemavu. Nilikua namshangaa michango yake bungeni. Hawana hata maana.
 
Anaandika Diwani wa Kata ya Kongolo- Magu na Mwanafalsafa Ndugu Herbet Faustine
__________________________

RAIS SAMIA ALITEGEMEA KUKUTANA NA NDOTO ZA MABILIONEA NYAMAGANA, KAKUTANA NA WAGOMBEA MIRATHI.

Rais Samia Suluhu Hassan kamaliza ziara yake mkoani Mwanza kwa kuzungumza na vijana wa taifa hili kupitia vijana wa mkoa wa Mwanza na Kanda ya ziwa kwa ujumla. Namshukuru Mungu kuna michuano ya soka huko Ulaya inaendelea ikatufanya tusahau yaliyojiri Nyamagana.

Tusidanganyane, tulichokiona Nyamagana ndiyo taswira ya vijana wa taifa hili walio wengi, wasomi kwa wasio soma tofauti kwenye ujenzi wako sawa. James Mbatia alipolalamikia mitaala ya elimu kipindi chote alipokuwa Bungeni alionekana hana maana! Katuumbua.

Rais Samia Suluhu Hassan alitoa fursa za vijana kuongea nae, waseme changamoto zao, nchi hii ni kubwa, nchi ina mambo mengi, Rais si nabii wa kujua kwenye mifugo kuna shida gani, kwenye uvuvi kuna matatizo gani, kwenye madini kuna nini, Rais akataka kujua kwenye kilimo kipi kinawapa taabu vijana kuwa mabilionea kupitia kilimo.! Je ni mbegu za GMO? Uhaba wa masoko? Rais aliwaza mbali kuliko vijana wenyewe.

Kwanini vijana? Nguvu ya uchumi wa nchi iko kwa vijana! Kama kuna fursa za kiuchumi zinahitajika kulisukuma taifa mbele basi fursa hizo zinawalenga vijana. Mama akatenga penalti wapige, vijana si tu wamepaisha ila kwa uwakilishi ule penalti imepigwa ikawa mpira wa kurusha.

Tatizo ni nini? Vijana walio wengi maono yao ni namna gani wapate hela ya kula na kunywa.
Hela hii haihitaji sana uwekezaji wa muda mrefu bali maono ya muda mfupi. Akili hizi zimewekezwa kwenye teuzi. Vijana wateuliwe u DC, U RC, u DAS. Aibu🙈

Rais alitegemea kukutana na hoja za vijana zinazoonesha namna gani vijana wapatiwe fursa za mitaji, misamaha ya kodi kwenye baadhi ya vitu kama matrekta ya kilimo, mikopo isiyo na masharti magumu kwenye taasisi za kifedha.

Nyamagana Rais Samia alitegemea kukutana na hoja zenye kuonesha miaka hamsini ijayo taifa liwe la aina gani, mama akakutana na hoja za namna gani walioteuliwa wanaendelea kuaminiwa nae kwenye nafasi zao, na wale wasioteuliwa wanaingiaje kwenye nafasi za kuteuliwa mana wanajua kuna nafasi hizo😳🙈.

Ukisikiliza hoja za pale Nyamagana mbele ya Rais unaona kabisa Rais alikuja kusikiliza hoja za mabilionea watarajiwa ila ajabu akakutana na hoja za wagombea mirathi.
Mama akafa moyo, kwenye hotuba akaanza kufafanua mpaka dhana nzima ya ujana! Ukimsikiliza Rais kwenye maana ya ujana utaona kuwa badala ya kuongea na vijana, alianza kutoa semina elekezi. Mwisho akakidhi matarajio yao ya muda mfupi, akawambia kuna mkeka wa wakuu wa wilaya unakuja. Wakashangilia.

Pale Kenya wiki hii wamempoteza bilionea Christopher Kirubi kwa saratani. Watanzania tarehe 15 June 2021 tumepoteza mabilionea Nyamagana kwa uwezo wa kufikiri. Christopher Kirubi alitaka kuwa bilionea akawekeza kwa kutumia fursa za nchini kwake, vijana wa Watanzania wanataka kuitwa mheshimiwa mkuu wa wilaya wamewekeza kwenye kujipendekeza.

Angalia jumuia za vyama vya siasa za makundi ya vijana. Hazina maono. Wakipata fursa ya kuongelea jambo mwisho wa hotuba lazima uulize ana elimu gani huyu mtu. Ukiambiwa elimu yake bado unahoji alipataje hii nafasi.

Nchi nzima inakusikiliza unapewa kisemeo unaanza kusema Mheshimiwa Rais sisi vijana tunakuunga mkono. Baada ya kumuunga mkono kinafuata nini? Aliyekuuliza nani? Mama kasema anawateua kutegemea na bidii yenu ya kusifu na uimbaji pambio?

Kundi hili la vijana ndilo lenye watu wasomi, lakini, nasema tena lakini, ikitokea mheshimiwa Rais akakutana na kundi la Mama Ntilie, ndiyo utaona tofauti ya elimu maisha na elimu teuzi.
pointi
 
Back
Top Bottom