WW1, WW2 na kinachoendelea sasa Middle east vilipangwa mwaka 1871 kama barua hii ni kweli

WW1, WW2 na kinachoendelea sasa Middle east vilipangwa mwaka 1871 kama barua hii ni kweli

Hao sio binadam

Kuna sehemu walikula kiapo Cha damu zao ,Ili siku Moja watu waje kutambua kuwa wao sio watu wa Ulimwengu huu,walikuja kama Roho zilizo Toka juu Ulimwengu mwinginw ni Roho za Giza zilizo Vaa mwili,


Kwenye Agenda Yao ya mwisho kama sikosei


Tafakari2010@yahoo.com
Jamaa anaitwa Gideon ,alikuwa akichambua Kila kinachoendelea Kila siku kina maana Gani,

Yaani jamaa kama ana macho ya ziada na anaufahamu mwingi na hio ndio email yake ya garazeti Hilo la tazama tz,

Huyo jamaa ni mchambuzi wa kinachoendelea duniani ,freemason wanahusikaje,
Hivi huyu jamaa alipotelea wapi, sijawahi kuona mtu anayejua maswala ya freemason kama huyu ,sijawahi kuona
 
Unaweza kunieleza ni kwa namna ipi vinachanganya watu na ku distort dhana nzima ya hukumu halisi?

Maana kwangu mimi hilo silioni na badala yake inafunua kwa uhalisia jambo hilo...

MOJA; Sijasema popote Nuhu aliandika kitabu bali Enock,kama umekosea kuandika kwa kuandika Nuhu badala ya Enoch,ni kwamba kiukweli sijaona sababu ya wewe kutoona sababu ya Enoch kuandika kitabu kile...

Vilivyoandikwa viliandikwa kwaajili ya wanadamu wajao,Enoch ni miongoni mwa wanadamu wa kwanza kabisa kuwepo hapa duniani ambapo walifuatiwa na wanadamu wengi baadaye,bado huoni sababu ya yeye kuandika kitabu hicho?

Unazungumzia historia ipi mkuu?

Binadamu hawakujua kuandika kabla ya Misri? Unaamini hili? kama unaamini basi naona una safari ndefu ya kujifunza historia sahihi kabisa ya binadamu na jambo hili....

Realy?

Kama unazungumzia suala la kujifunza kuandika hapo sawa lakini siyo nje ya hapo...

Ni kweli....

Tunatofautiana tu kujua malengo....

Wamecomplicate maandiko ya kitabu kipi?

Wanawezaje kuyafanya maandiko yafanane na Biblia ambayo ndiyo adui yao mkuu?

Wakati wa vita ya pili ya dunia kuna mmoja alipatikana wakati ule kwenye moja ya mapango ya maeneo ambayo vita ilikuwa inapiganwa,Mnefili mmoja wa karibuni kabisa kuonekana na watu wa kawaida ni yule aliyepatikana kwenye vita ya kule Afghanistan na akasafirishwa hadi Marekani na jeshi la nchi hiyo.....

Ngoja nikiikumbuka hiyo documenary nitaiweka hapa ukaangalie....
Mkuu, hicho kitabu cha Enock kinatumiwa sana na waganga na Masonic. Una uhakika kwamba Enok alijua kusoma na kuandika? Elimu hiyo ilikiwepo?
Ninavyofahamu elimu ya kusoma ilianzia Misri, Musa alilelewa na binti Farao alipewa elimu yote ya kimisri, huyo ndie alieandika torati na historia yote ya kuanzia Adam hadi wakati wake (Musa).
Yeye ndie aliyewafundisha walawi na Wana wa Israel kuandika (nafikiri Sina hakika) wakiwa kangwani ili kutunza torati na matukio ya historia yao, huyo Enok habari zake ziliandikwa na Musa.
Kabla ya Musa hakuna ushahidi wa yeyote aliyeandika chochote.
Huoni kwamba hicho kitabu cha Henoko alichoandika Henoko mwenyewe ni uzushi, ni mafrimason wamekitunga?
 
Matatizo yote ya hii dunia kimsingi yameletwa na kiumbe mwenye "busara" unaweza kumuita nyoka au Lucifer ukitaka,hapa panahitajika somo refu lenye kuweza kukuelewesha ni kwa maana ipi ambayo mimi namaanisha kinyume na unayoona wewe.Mtu yoyote ukimueleza kuwa tatizo ni Shetani ataelewa na mawazo yake yatakwenda kwenye kile alichoeleweshwa kumhusu ambacho naona kama kinapungua,hatujui ipaswavyo,nitakueleza kwa ufupi na kwa namna fulani ambayo utaweza kupata picha angalau kidogo....

Kama ujuavyo ni kwamba Lucifer alikuwa ni malaika kule mbinguni na alianzisha harakati za kudai "haki" kutoka kwa Mungu.Yeye kwa tafsiri yake aliona hakuna haki hivyo alianzisha kampeni ambayo ilipelekea kufanikiwa kuwadanganya robo ya malaika wa mbinguni ambapo inakadiriwa ni malaika zaidi ya 300.......

Harakati hizi za Shetani zilisababisha kutokea kwa mvurugano huko mbinguni na kulazimika Shetani kuondolewa huko na kutupwa hapa duniani ambapo nako alidhamiria kuendeleza kampeni ya "kukomboa" viumbe wengine kutoka kwenye "udikteta" wa Mungu.Shetani hakuwa akikubaliana na Mungu namna ambayo aliamua kuwahudumia viumbe wote pamoja na kanuni zote alizoweka hivyo akaamua kuanzisha movement yake ambayo mwanzo alidhani angeweza kushinda....

Ukweli ni kwamba alishindwa,baada ya kushindwa na kujua kuwa hataweza kutimiza malengo yake aliamua kuendeleza harakati zile kwenye viumbe wengine lakini akitaka kumtumia kiumbe mmoja maalum...

Aliamua kumtumia kiumbe ambaye Mungu alimuumba kwa unadhifu na kwa malengo maalum kutimiza malengo yake.Malengo ya Shetani ni kutaka kuzuia malengo ya Mungu kutimia kwa kiumbe huyu na kwa kufanya hivyo atakuwa ametimiza angalau lengo moja ambalo ni kuvuruga mipango ya Mungu kwa kiumbe huyu aliyempenda kabisa.....

Kiumbe huyu ni binadamu.Shetani anajua kabisa kuwa kiumbe huyu ndiye kiumbe pekee ambaye Mungu alimpenda na kuchagua yeye [Mungu] kuwa sehemu yake,hivyo akaamua kufanya harakati zote ili amdhalilishe Mungu kupitia kiumbe huyu....

Aliamua kuanzisha harakati nyingi sana ili aweze kutimiza lengo lake hili.Harakati ya kwanza kabisa ni tukio la pale Eden ambapo alimtumia mwanamke kumuangusha mwanadamu huyu na alifanikiwa.Tool kubwa sana anayotumia Shetani ni uongo maana akisema ukweli hataweza kufanikiwa kabisa....

Baada ya kufanikiwa kwenye tukio hili Shetani aliamua au niseme alipanga kuvuruga kabisa uumbaji wa Mungu kwa kiumbe huyu,kwakuwa Mungu alimfukuza Shetani kule mbunguni na huyo huyo Mungu akaamua kuwa sehemu ya kuimbe ambaye Shetani anamuona kama dhaifu,aliamua na yeye kutengeneza harakati za yeye naye kuingia ndani ya binadamu na kuwa sehemu yake....

Aliamua kutengeneza mahusiano ya karibu na binadamu na hatimaye alifanikiwa kuanza kuvuruga DNA ya binadamu kwa kumuingilia kingono na kufanikiwa kutengeneza kizazi au blood line ambayo haikuwa pure human,blood line hii inafahamika kama hybrid leo lakini miongoni mwa matokeo ya jambo hili ni kuzaliwa Wanefili [Nephilims]....

Hawa hybrid ndiyo binadamu wanaojulikana kuwa na akili sana na hapa ndipo tunakuja kwenye yote tunayojifunza duniani na historia kwa ujumla wake.

Mungu alijua hili kuwa Shetani naye ataanzisha race yake na ndiyo maana Mungu alimuambia pale Eden kuwa "nitaweka uadui kati ya kizazi chako na cha mwanamke",hapa alikuwa anazungumzia kizazi hiki kiovu kabisa cha Shetani au "the brothherhood of the snake"....

Shetani alitaka ku wipe out kabisa mwanadamu wa asili ili zweze kutengeneza ufalme wake hapa duniani lakini Mungu hakuruhusu hili na ndiyo maana unaona matukio kama gharika.....

Pamoja na lengo hili la Shetani la kutaka kuvuruga kizazi cha mwanadamu ili kuvuruga lengo la Mungu kumuumba mwanadamu,pia alifanikiwa kuingia ndani ya mwanadamu kama alivyo Mungu kwa namna niliyoielezea hapo juu.Hakuishia hapo,aliendelea na harakati zake za kutaka kumdhalilisha Mungu kupitia kiumbe huyu ambaye Mungu alimuumba kwa gharama kubwa kabisa.....

Alitengeneza mbinu za kumfanya binadamu huyu amuabudu kama vile ambavypo Mungu anaabudiwa na mwanadamu,ikumbukwe kwamba ni binadamu pekee anayemuabudu Mungu katika viumbe vyote.Kwa kutimiza hilo,kwa udanganyifu mkubwa na kwa kubadili majina yake alifanikiwa kutengeneza dini tofauti tofauti ambazo kwa binadamu kutokuelewa wanazifuata wakidhani wanamuabudu Mungu kumbe wanamuabudu Shetani,hapa akawa amefanikiwa kumrubuni tena kumbe huyu ambaye Mungu alimuumba kwa gharama kubwa kabisa.....

Hakuishia hapo,aliendelea na harakati zake za kuhakikisha anavuruga kabisa malengo ya Mungu kwa kiumbe huyu kwa namna yoyote ile na kuhakikisha anamuweka kiumbe huyu mbali kabisa na Mungu.Harakati yake nyingine aliyoileta ni elimu na falsafa.Shetani ni kiumbe ambaye ameumbwa kwa ubora zaidi ya binadamu kwa maana ya mwili na uwezo wake,ana uwezo mkubwa sana wa kiakili.Lakini kikubwa na cha hatari kabisa ni kwamba wakati Mungu anaiumba dunia hii kiumbe huyu alikuwepo,hivyo ni kiumbe anayeielewa physics kwa kiwango cha kutisha....

Ni kiumbe ambaye wakati Mungu anamuumba binadamu alikuwepo na alijua Mungu anafanya nini au alifanya nini,anajua namna mwili wako unafanya kazi kwa kiwango cha kutisha kabisa.Shetani,kama siyo Mungu kuingilia kati leo binadamu tungekuwa hatupo kabisa.....

Shetani akaamua kuleta elimu na falsafa ambazo zitamfanya binadamu kuwa mbali kabisa na Mungu.Mambo kama uwezo wa kutoka nje ya mwili [Ashtral projection] matukio ya NDE [Near death experiance] masuala ya tahajudi [Meditation] ambayo yanakufanya unakutana na viumbe wa anga za mbali huko,sayansi na maendeleo yake yote ambayo yanamfanya binadamu kujua asiyostahili kujua,elimu za anga na nyota ambapo malaika waliowafundisha wanadamu yote haya wanajulikana majina, waliwafanya binadamu kuwa na access na mambo ambayo hakupaswa kuyajua na kumfanya binadamu kumuona Mungu kama ni hadithi,hayupo....

Kitendo cha binadamu kujua mambo mengi ya ulimwengu kukamfanya akawa mbali kabisa na Mungu wake.Shetani na jeshi lake wakawafundisha wanadamu kufanya abortion na uchafu mwingine mwingi kabisa,taratibu mwanadamu akaanza kuona Mungu ni jambo la kijinga kabisa,Shetani akawa amefanikiwa tena....

Kwakuwa yote haya Shetani aliyafanya ili amdanganye mwanadamu na amuache Mungu wake,Shetani hakuwa mkweli kwa binadamu huyu kuwa alitaka amdhalilishe yeye [mwanadamu] na muumba wake.Shetani akaendelea na harakati zake za kutimiza hili.Akawaagiza wale binadamu ambao ni kizazi chake kuanza kuwafundisha wanadamu kufanya mapenzi kinyume na maumbile,wakaendesha harakati kuwa ni haki yao kufanya hivyo kwakuwa wanaweza kujiamulia watakayo....

To cut the story maana matukio ya mfululizo ni mengi ni kwamba,katika harakati hizi hadi kufikia kutengeneza kizazi kiovu cha Shetani kutokana na wao kuingilia wanadamu na kuzaa,wamekuwa ndiyo wanaoiendesha dunia hii na wanapanga vita ili kuua wanadamu kwasababu nyingi sana lakini kubwa ni hiyo hizo nilizozieleza hapo juu....

Wanatengeneza vyakula ambavyo vitamfanya binadamu ashindwe kabisa kufikiri.Wanatengeneza madawa ya kumdhoofisha mwanadamu huyu ashindwe kabisa kuwa na mwili imara ili aweze kumtawala atakavyo na kutimiza malengo yake....

Vita na yote unayoona yanaendelea ni vita kati ya Mungu na huyu kumbe muovu.Nimeelezea kiduchu kwa upande huu mdogo sana lakini yapo mengi sana tena sana na ya kutisha kabisa.Binadamu anayeonekana juu ya uso wa dunia leo ni binadamu dhaifu kabisa kuliko ambavyo tunaelezwa kuwa anaendelea kupanuka kifikra....

Hili limetokea kwasababu hizo nilizozieleza hapo juu na nyingine nyingi kabisa ambazo kuziangika zote zinahitaji kitabu....

Nadhani nimejibu swali lako kuwa "ni akina nani hao" angalau kwa sehemu mkuu....
Duh!
 
Back
Top Bottom