Tetesi: Wydad Casablanca wamrudia Clement Mzize, Ofa ya zaidi ya Tsh. Bilioni 2, na Masharti Magumu

Kama ni serious.

Wamwache aende.

Maisha popote.
 
Elewa neno kwa faida ya mchezaji.. Unadhani mzize kati ya yanga na wydad wapi anatengeneza cv nzuri zaidi,
Wydad ni timu kubwa kwa yanga, mchezaji anapaswa kwenda kujikuza zaidi.
Kama ni swala la CV basi akiwa Yanga ndio atatengeneza CV nzuri zaidi kwasababu kwanza ana uhakika wa kupata namba kwasababu tayari kaishaingia kwenye mfumo wa Gamondi.
Pili ni kwamba Yanga inacheza klabu bingwa ni mashindano yanayoangaliwa na wengi.
Tatu akiwa Yanga, Mzize anacheza bila presha kwavile alipo anavumiliwa
 
🤣😂🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Inatosha mkuu, utanivunja mbavu. 😂🤣🤣🤣🤣🤣
 
propaganda tu ,hakuna mchezaji wa kuuzwa bilioni pale uto, acheni utani uto.
 
Hii kamba kwa mpira alionao juzi ilikuwa anaruka ruka tu.
 
Kwahiyo Mzize akacheze timu anbayo aishiriki mashindano ya CAF kama timu za Mashujaa, Tabora United!

Alafu huyo kocha wao hana muda mrefu watamtimua
 
Kama ni kweli. Yanga tusimbanie dogo maisha mazuri.

Familia yake isonge mbele.

Tumuache dogo akacheze FIFA Club world cup na kina Man city marekani akiwa na Wydad.

Kuna muda inabidi utu uwepo. Naona yanga tunamuharibia maisha mzize. Fursa kubwa sana hiyo ya kucheza club world cup
Naunga mkono hoja iwe kama Simon msuva alivyouzwa Morocco na Yanga akaleta mchango kwa timu ya taifa .
Mokwena alimtaja sana mzize wakati wa mechi za yanga v mamelodi Kumbe alimaanisha .
 
Unaambiwa, vigogo wa soka la Morocco, Wydad Casablanca, hawajakata tamaa. Wakifukuzia saini ya mshambuliaji wa Taifa Stars na Yanga SC, Clement Mzize. Hii ni baada ya klabu yake kuweka wazi kuwa hajupo sokoni. Lakini Wydad hawajali, hawasikii wala hawaogopi—wanaendelea kushindilia mlango ambao unaonekana kufungwa.

Kwa mujibu wa taarifa ya, Micky mwandishi wa Ghana, amefichua kuwa ofa ya hivi karibuni ya Wydad ni kama wameamua kurudi tena, wakiwa na begi zima la fedha ofa ikifikia—USD 500,000, sawa na takriban Tsh. bilioni 1.4, na masharti maalum ya kuongeza USD 300,000 (Tsh. milioni 815.4) zaidi endapo Mzize atatimiza malengo fulani, kama kushinda tuzo ya mfungaji bora na kuchangia ushindi wa mataji ya ligi na Kombe la Dunia la Vilabu.
Ni kama mchezo wa bahati nasibu—kila mmoja anasubiri kuona kama Yanga watasalimu amri au kama Wydad watavunja ngome hiyo ya Yanga.
Klabu hiyo yenye mamilioni ya mashabiki maarufu "Ultras Winners", wamekuwa wakikatiza kwenye page ya instagram ya Mzize na kumkaribisha kwenye klabu yao.
Je, Yanga wataruhusu ajiunge na Wydad AC?

Soma zaidi:
Clement Mzize huyu hapa kwenye rada ya Wydad Casablanca
Yanga imekataa ofa ya pili ya klabu ya Wydad ya Tsh Bilioni 1.7
Waongeze mzigo ufike $1 mil
 
Dogo aende kula pesa huku akiozea benchi!! Baada ya mwaka mmoja kwishney!! Chezea waarabu weye!!
 
Shida ya Waydad wao wanaangalia umri wa Mzize wa kwenye makaratasi wanaamini bado mdogo na atafundishika. Subiri sasa wamchukue halafu wakampime umri kwa kutumia "carbon 14" hapo ndio watagundua kuwa huyo Mzize kapishana umri kidogo sana na Zinjathropus. Na ikitokea kapata injury hata ya kawaida tu kupona kwake sio chini ya miezi sita maana viungo na mifupa yote ya mwilini imeshakomaa.

Hovi kweli Wydad wangekuwa werevu si bora wangepambana kumpata mmojawapo kati ya Aziz Ki au Max au ikishindikana kabisa si bora hata wangemchukua mzee Chama akawasaidia kwenye "moment" muhimu kuliko kuhangaika na huyo Mzize ambaye hana mwendelezo mzuri wa moja kwa moja.
 
Back
Top Bottom