Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kama ndo huyu alicheza juzi match ya stars na Ethopia wamtoe tu hata bure ikiwezekana.Kama ni kweli. Yanga tusimbanie dogo maisha mazuri.
Familia yake isonge mbele.
Tumuache dogo akacheze FIFA Club world cup na kina Man city marekani akiwa na Wydad.
Kuna muda inabidi utu uwepo. Naona yanga tunamuharibia maisha mzize. Fursa kubwa sana hiyo ya kucheza club world cup
Akili za yanga wanazijua wenyewe. Juzi nilimuona akicheza na Ethiopia aibu nilikuwa naona mmWydad ipo kwenye ratiba ya kushiriki michuano mikubwa ya world cup.
Inatazamiwa kukutana na vilabu bikubwa zaidi duniani kama Madrid, Barcelona, Chelsea, Man U nk.
Mamelody, Al Ahly wao wanafikia hatua ya kwenda hadi huko huko Ulaya kuchukua wachezaji wakubwa ili kupata Quality ya ku-challenge hizo Clubs.
Then Wydad wenye ambitions hizo hizi za kuonesha challenge dhidi ya hao vigogo aje amsajili Mzize??
Huyu huyu Mzize ambaye kacheza msimu mzima lakini kafunga goli 3 kazidiwa na Fredy aliyekuja dirisha dogo?
Sio Mtanzania tu pia ni KINDA🤣Kumbe jamaa ni Mtanzania
Ally Kamwe bana.Unaambiwa, vigogo wa soka la Morocco, Wydad Casablanca, hawajakata tamaa. Wakifukuzia saini ya mshambuliaji wa Taifa Stars na Yanga SC, Clement Mzize. Hii ni baada ya klabu yake kuweka wazi kuwa hajupo sokoni. Lakini Wydad hawajali, hawasikii wala hawaogopi—wanaendelea kushindilia mlango ambao unaonekana kufungwa.
Kwa mujibu wa taarifa ya, Micky mwandishi wa Ghana, amefichua kuwa ofa ya hivi karibuni ya Wydad ni kama wameamua kurudi tena, wakiwa na begi zima la fedha ofa ikifikia—USD 500,000, sawa na takriban Tsh. bilioni 1.4, na masharti maalum ya kuongeza USD 300,000 (Tsh. milioni 815.4) zaidi endapo Mzize atatimiza malengo fulani, kama kushinda tuzo ya mfungaji bora na kuchangia ushindi wa mataji ya ligi na Kombe la Dunia la
Vilabu.
View attachment 3088174
Ni kama mchezo wa bahati nasibu—kila mmoja anasubiri kuona kama Yanga watasalimu amri au kama Wydad watavunja ngome hiyo ya Yanga.
Klabu hiyo yenye mamilioni ya mashabiki maarufu "Ultras Winners", wamekuwa wakikatiza kwenye page ya instagram ya Mzize na kumkaribisha kwenye klabu yao.
Je, Yanga wataruhusu ajiunge na Wydad AC?
Soma zaidi:
• Clement Mzize huyu hapa kwenye rada ya Wydad Casablanca ✅
• Yanga imekataa ofa ya pili ya klabu ya Wydad ya Tsh Bilioni 1.7
Kwahiyo Yanga ndio wanao report kuwa Wydad wanamuhitaji Mzize? Mbona akili za kufikiria hamna?Akili za yanga wanazijua wenyewe. Juzi nilimuona akicheza na Ethiopia aibu nilikuwa naona mm
Hivi wewe unajidanganya kuwa Wydad wanaweza kumlilia Mzize kiasi hicho? Hizo ni Propaganda za kumkuza Mzize na hazina ukwel wowote.Kwahiyo Yanga ndio wanao report kuwa Wydad wanamuhitaji Mzize? Mbona akili za kufikiria hamna?
Umempa pigo mujarabuYanga wana mipango yao na Wydad wana mpango yao katika dunia ya kibepari hakuna kitu kuoneana huruma kama unadhani ni rahisi nenda kwao ukanunue key player wao uone kama watakuuzia
Mzize awekewe propaganda za kukuzwa ili iweje?Hivi wewe unajidanganya kuwa Wydad wanaweza kumlilia Mzize kiasi hicho? Hizo ni Propaganda za kumkuza Mzize na hazina ukwel wowote.
Kwa uchawi uliopo Yanga huyo Mzize anaweza kupotea ghafla akaja kujitokeza Wydad wakiwa wameghairi.
Case Study: Mrisho Ngasa na club kutoka Sudan.
Maskini roho mbaya ya viongoz watamnyima na hio itamvunja sana moyo, ndio mana jana hakucheza vyema ana mawazo tele
Tetesi kidogo watu mmeshavaa khanga na kuanza kusuta kwa maneno kama yoteYanga SC club ya vibwengo mdundiko watafanya wivu
Hilo tukio ni upumbavu wa Manara na likamng'oa mazima. Swala la Azizi Ki kutakiwa na vilabu vya nje mbona lilikuwa wazi hasa hasa Belouizdad walionesha wapo serious naye. Mchezaji kutakiwa ni swala moja na mchezaji mwenyewe au klabu kukubali kufanya dili ni swala lingine.Tangu Azizi na Hamisa wavalishane jezi Mambo ya tetesi za wachezaji wa Yanga si ya kutilia maanani sana unless ni official statement kutoka Club husika. Kuna maigizo mno na waigizaji wapo hadi wa kimataifa. Club ikizungumza kuhusu hilo sawa.
Kutakiwa kupo. Ila kuna tetesi ambazo zina ukweli na zisizo za ukweli.Hilo tukio ni upumbavu wa Manara na likamng'oa mazima. Swala la Azizi Ki kutakiwa na vilabu vya nje mbona lilikuwa wazi hasa hasa Belouizdad walionesha wapo serious naye. Mchezaji kutakiwa ni swala moja na mchezaji mwenyewe au klabu kukubali kufanya dili ni swala lingine.
Kwahiyo ya Aziz Ki ilikuwa ni tetesi za ukweli au uongo?Kutakiwa kupo. Ila kuna tetesi ambazo zina ukweli na zisizo za ukweli.
Aziz K alimvalisha mobeto jezi, hii ndo suala halisi mengine ni tetesi.Kwahiyo ya Aziz Ki ilikuwa ni tetesi za ukweli au uongo?
Hii kitu ilikuuma sanaAziz K alimvalisha mobeto jezi, hii ndo suala halisi mengine ni tetesi.