Wydad wanacheza ligi kwao leo usiku, sisi huku Bongo tunazipa muda wa kurelax Simba na Yanga

Wydad wanacheza ligi kwao leo usiku, sisi huku Bongo tunazipa muda wa kurelax Simba na Yanga

Wydad anacheza na Simba jmoc saa 4 usiku lakn leo jumatano ana kibarua cha ligi kuu, nimejiuliza sana kwann haya mambo hayafanyiki hapa bongo, wiki nzima Simba na Yanga zimekaa bila kucheza, Shall we make it?

Kwa hiyo wacheze mechi ya ligi Bongo halafu wasafiri lini kwenda Morocco kuwahi hiyo mechi ya j'mosi?
 
Kwa upeo mdogo tu ungeweza kujua kuwa Simba inasafiri wakati Wydad haisafiri. Hata hilo ulishindwa kuliona?
Al ahly alicheza kwao ligi ndo akaja kucheza na yanga mbona haujashangaa?

Yaan hauoni hata aibu? Haya mambo ni ya kijinga wala sio ya kutetea, huko ulaya wanacheza uefa j5 na jmos wancheza tena ligi. Tena team zina safari.
 
Kakimbilia kupost tu
Ww ndo haujielewi unatetea ujinga coz hao wydad wiki iliyoisha kacheza far rabat kati kati ya wiki akafungwa na akasafiri mpka ivory Coast kucheza champion ligi dhidi ya asec.

Na pia sio wydad tu hata Al ahly, esperance na mamelod wanacheza ligi kati kati na champion ligi ndani ya wiki moja moja hiyo hiyo.

Hizi simba na yanga zinalelewa vibaya na zina haribu tu mpira
 
Kwa hiyo wqcheze mechi ya ligi Bongo halafu wasafiri lini kwenda Morocco kuwahi hiyo mechi ya j'mosi?
Kwani wydad,mamelod ,Al ahly na esperance wanavocheza mechi za ligi na kusafiri kwenda kucheza champion league huwa wanasafiri vp? Mnatetea vitu vya kipumbavu sana.

Mamelod anacheza lig saiv na ana mechi weekend kama simba
 
Hata wiki iliyopita jumatano kama ya Leo walicheza mechi ya Ligi(Botola pro) Tena mechi ngumu kwelii kwelii dhidi ya ASFAR Rabat na wakati huo jumamosi walikuwa wanaenda kukutana na Asec mimosas ugenini huko Ivory coast...
Na mwisho wa siku Mamelod na Wydad wakapoteza mechi, je haiwezi kuwa uchovu wa safari na kucheza mechi back to back kumesababishia?
 
Ww ndo haujielewi unatetea ujinga coz hao wydad wiki iliyoisha kacheza far rabat kati kati ya wiki akafungwa na akasafiri mpka ivory Coast kucheza champion ligi dhidi ya asec.

Na pia sio wydad tu hata Al ahly, esperance na mamelod wanacheza ligi kati kati na champion ligi ndani ya wiki moja moja hiyo hiyo.

Hizi simba na yanga zinalelewa vibaya na zina haribu tu mpira
Simba na yanga kabla ya kucheza mechi zao za pili walipaswa wacheze mechi moja moja ta ligi hii ingewasaidia kuwa na match fitness
 
simba wana game na kagera sugar trehe 15 ;tarehe 19 wanarudiana na wydad.

yanga wana game trhe 16 na mtibwa ;tarehe 20 wanarudiana na medeama.

izo game za kagera na mtibwa kama zitakuwa postponed.. nitaamini kweli kuna shida pahala.
 
Ww ndo haujielewi unatetea ujinga coz hao wydad wiki iliyoisha kacheza far rabat kati kati ya wiki akafungwa na akasafiri mpka ivory Coast kucheza champion ligi dhidi ya asec.

Na pia sio wydad tu hata Al ahly, esperance na mamelod wanacheza ligi kati kati na champion ligi ndani ya wiki moja moja hiyo hiyo.

Hizi simba na yanga zinalelewa vibaya na zina haribu tu mpira
Ila ukicheki hizi ligi za Africa almost hamna tofauti, angalia table za ligi hizo umezitaja👇
 
Attachments

  • Screenshot_20231206-230053_Carbon Super Fast Browser.jpg
    Screenshot_20231206-230053_Carbon Super Fast Browser.jpg
    110.6 KB · Views: 2
  • Screenshot_20231206-230119_Carbon Super Fast Browser.jpg
    Screenshot_20231206-230119_Carbon Super Fast Browser.jpg
    121.6 KB · Views: 1
  • Screenshot_20231206-230224_Carbon Super Fast Browser.jpg
    Screenshot_20231206-230224_Carbon Super Fast Browser.jpg
    146 KB · Views: 1
  • Screenshot_20231206-230304_Carbon Super Fast Browser.jpg
    Screenshot_20231206-230304_Carbon Super Fast Browser.jpg
    119.4 KB · Views: 2
  • Screenshot_20231206-230944_Carbon Super Fast Browser.jpg
    Screenshot_20231206-230944_Carbon Super Fast Browser.jpg
    114.7 KB · Views: 2
  • Screenshot_20231206-231016_Carbon Super Fast Browser.jpg
    Screenshot_20231206-231016_Carbon Super Fast Browser.jpg
    127.4 KB · Views: 1
  • Screenshot_20231206-231055_Carbon Super Fast Browser.jpg
    Screenshot_20231206-231055_Carbon Super Fast Browser.jpg
    122.8 KB · Views: 1
Kwa upeo mdogo tu ungeweza kujua kuwa Simba inasafiri wakati Wydad haisafiri. Hata hilo ulishindwa kuliona?
Shida ujinga umekujaa, mara ngap Simba anabaki nchini anakaa wiki nzima kusubiri mechi, Simba wamekaa wiki nzima wakisubiri kucheza na yanga, hili nalo huoni, yaan timu inaakaa wiki ndio inacheza
 
Izo timu kubwa barani Afrika faatilieni zinapo safiri uwa Zinafanya ma koneksheni kama izi timu zetu?
Mara zote izo timu Zina Kodi ndege au Zina ndege zao kwaiyo inakua rahisi kufika na kuondoka kwenye kituo.

Ni kweli timu kukaa wiki bila mechi haijakaa vizuri ila Kuna muda ni kwakua zinasafiri kwa kupitia kituo zaidi ya kimoja.
Bara la Afrika usafiri wa Anga Bado una shida.

Timu inatoka Dar mpaka Adis au Dubai pale unakuta Ina Kaa on transit massa 6 ikisubiri connection, wachezji wanakaa lounge baadae wanaunga safari unakuta Wana connect Tena .
Mpaka wafike wako hoi.

Ikiwa Ahly wanasafiri na ndege ya kukodi na Bado wanatembea na mapipa ya Recovery ili kuondoa fatigue, Nyie msipo zipa muda timu zenu zitaweza kushindana na vibajeti vyenu vya kuunga unga!!
 
Wydad anacheza na Simba jmoc saa 4 usiku lakn leo jumatano ana kibarua cha ligi kuu, nimejiuliza sana kwann haya mambo hayafanyiki hapa bongo, wiki nzima Simba na Yanga zimekaa bila kucheza, Shall we make it?
Uharoooo
 
Na mwisho wa siku Mamelod na Wydad wakapoteza mechi, je haiwezi kuwa uchovu wa safari na kucheza mechi back to back kumesababishia?
Kupoteza mechi Kuna sababu nyingi sana na sababu kuu hasa Huwa ni ubora na maandalizi aliyoyafanya mpinzani wako dhidi yako wewe, nje na hapo ni sababu ambazo hazina kichwa Wala miguu.

Unasema kwamba waydad alifungwa na Asec mimosas sababu ya uchovu haya vipi na mechi ya kwanza ambayo alifungwa na Janengwe galaxy ambapo alikuwa nyumbani na Tena alipumzika wiki nzima kabla ya mechi? Vipi na Yanga yetu hii ambayo ilipunzika kwa zaidi ya siku 10 Kisha ndio ikasafiri kwenda Algeria ikakutana na kichapo cha 0-3?

Sundowns na Waydad kufungwa sababu ni za kiufundi zaidi na Wala sio uchovu wa safari au kucheza mechi back to back, kwanza kama hata uliangalia mechi zao Sundowns alitawala Ile mechi mwanzo mwisho.

Hizi mambo za kupoteza mechi Kisha unato excuses za sijui uchovu wa safari Morinho anasema ni sababu za kipuuzi na hazistahili kabisa kusemwa na mtu wa mpira. Hili jibu aliwaambia Barcelona baada ya kuwafunga 3-1 kwenye mechi ya nusu fainali ya CL mwaka 2010 ambapo Barcelona ilikuwa imesafiri kwa treni kutoka Spain mpaka Milan.
 
Al ahly alicheza kwao ligi ndo akaja kucheza na yanga mbona haujashangaa?

Yaan hauoni hata aibu? Haya mambo ni ya kijinga wala sio ya kutetea, huko ulaya wanacheza uefa j5 na jmos wancheza tena ligi. Tena team zina safari.
Watu wanatetea tu sababu ya mahaba waliyonayo kwa hivi vilabu vyao mapacha. Lakini wanachokifanya TFF na hizi timu zenyewe ni mambo yaliyopitwa na wakati, yaani Leo hii 2023 timu Bado Zina rundika viporo kwa sababu ya mambo ya logistics na hapo tunaambiwa eti bajeti zao kwa msimu Huwa ni mabilion..!!??!!!

Mimi nasubiri tu itakapofika mwezi march watakapoanza kucheza kila baada ya siku moja kutokana na mrundikano wa viporo.... sipati picha mapacha hawa watakavyokuwa wanashindana kununua mechi kwa hivi vilabu vidogo vinavyoelekea kushuka daraja, maana timu zitakuwa hazina Tena morali wa kupambana, wachezaji wanawaza Ligi iishe waendelee likizo.

Poor TFF, poor Tanzanian football
 
Unajua kutoka Tanganyika mpaka Morroco kwa ndege ya kibiashara ni siku 3?

Unatoka Dar mpaka Doha, pale Doha unachukua ndege mpaka Algeria, Algeria ndio siku inayofuata unapata connection ya Morroco?

Na ukifika Casablanca mechi inachzwa mkoani huko Marakesh- yaani kilometa 200 lazma upate connection ya local flights ama basi ni masaa 4, , natumai sasa akili zako kama si za maandazi umeelewa.

Unajua hata hapo Angola ukitaka kwenda kucheza unakwenda Dubai, Dubai ndio unapata ndege ya kwenda hapo angola?
Wiki ilopita wote yanga simba mlikua dar nako wiki nzima kulikua hakuna mechi leta utetezi. Sema tu league yetu kivyetuvyetu
 
Back
Top Bottom