Xiaomi 14 na Xiaomi 14 Pro: Mchina anaendelea kuleta competition

Xiaomi 14 na Xiaomi 14 Pro: Mchina anaendelea kuleta competition

Hii simu haitumii Adroid OS
Inatumia Android 14, ila wameweka Android skin yao wenyewe juu ya Android 14 inayoitwa Xiaomi HyperOS.

Lengo la Xiaomi HyperOS ni kuweka ile feeling ya Xiaomi kwenye simu zake na kuunganisha simu yako na vifaa vya nyumbani vya Xiaomi kama TV, laptop, Air conditioners, dryers, electric scooters, mafriji na electronics nyingine za Xiaomi.
Pia inalenga kuunganisha simu za Xiaomi na magari yao ya umeme ambayo yataachiliwa siku za usoni mwakani 2024
 
Very interesting
 
View attachment 2847909
Mwaka huu zimetoka simu nyingi sana ila Mchina kanifurahisha zaidi.
Kampuni ya Xiaomi imetoa flagship zao mpya October mwaka huu ambazo ni Xiaomi 14 na Xiaomi 14 Pro.View attachment 2847911
Nadhani zinastahili kuwa flagship bora zaidi kwa mwaka huu.
Xiaomi 14 Pro imefikia level ambayo inaweza kushindanishwa na iPhone 15 Pro Max na kuizidi Samsung Galaxy S23 Ultra.View attachment 2847913
Xiaomi 14 Pro inakuja na Qualcomm Snapdragon 8 Gen 3, na inafikia hadi 16GB RAM 1TB ROM, Inakuja na 1440p display, kamera ya mbele sasa inaweza kurekodi video za 4K@60fps na pia inakuja na USB Type C 3.2View attachment 2847916
Kitu kingine chema ni kwamba Xiaomi 14 na 14 Pro sasahivi hazijaja na software ya MIUI, Sasahivi ziatumia software mpya ya Xiaomi inayoitwa "Xiaomi HyperOS"View attachment 2847917
Xiaomi HyperOS inafanana na MIUI kimwonekano ila wamebadilisha mwonekano kidogo sana. Xiaomi HyperOS iko more optimised kushinda MIUI 14 na imekuwa very stable kuliko MIUI ilivyokuwa hapo awali mpaka baadhi ya phone reviewers wameshangaaView attachment 2847915
View attachment 2847920
Kwenye upande wa kamera Xiaomi anaendelea kushirikiana na Mjerumani "LEICA" na kamera ya Xiaomi 14 Pro imekuwa very improved, kama ulifuatilia vizuri kamera ya nyuma ya Xiaomi 13 Ultra ilikuwa ni nzuri kushinda iPhone 14 Pro Max. Sasahivi kamera ya nyuma ya Xiaomi 14 Pro iko vizuri kiasi cha kushindana na iPhone 15 Pro Max View attachment 2847921
Kwa sasa hii simu ipo official kwa China tu ila Global version inaweza kuachiwa February 2024. Nadhani na Samsung Galaxy S24 Ultra itaachiwa kipindi hichohichoView attachment 2847922
Nchini China, Xiaomi 14 na 14 Pro zilipoachiwa tu, waliuza takribani simu milioni 1.45 (Xiaomi 14 series) ndani ya siku 10 tu na kufanya Xiaomi 14 series kuongoza kwa mauzo nchini China katika wiki ya 44 ya mauzo ya simu huku Huawei na Honor ndio wanafuatia.View attachment 2847929
Xiaomi 14 Pro version ya 16GB RAM 1TB ROM imetengenezwa na titanium kwa nje kama tu iPhone 15 Pro Max. Mfano angalia hii picha, hiyo ya kushoto ni Xiaomi 14 Pro (titanium) na kulia ni iPhone 15 Pro Max. Zote ni titaniumView attachment 2847930
Kadri siku zinavyoenda Mchina anazidi kuionesha dunia kuwa na yeye anaweza
Mbona huzungumzii Huawei 60 Pro? Je, baba lao duniani kwa sasa Huawei Mate 60 Pro una la kusema?
 
Reuben Challe naomba ushauri Kati ya Redmi note 11 pro vs Redmi 12 C ipi bora

Bei ya 11 pro kwa sasa sokoni ikoje maana nakosaga majibu sahihi
Redmi Note 11 Pro ni bora kwenye kila kitu kuliko Redmi 12C, kuanzia kamera, display, performance, software, design, call quality na kila kitu tena kwa gap kubwa sana kwa sababu Redmi Note 11 Pro ni midrange na Redmi 12C ni low end phone
Kwa Tanzania naona Redmi Note 11 Pro inauzwa kwa 600,000/= halafu Redmi 12C inauzwa kwa 240,000/=. Hata bei zinaonesha utofauti uliopo baina ya hizi simu mbili

Redmi Note 11 Pro ni simu ya muda, sasa hivi Note 12 series zimeshatoka na Note 13 series zimetoka pia kwa hiyo kama unataka Redmi Note series ni heri ununue Redmi Note 12 series au Note 13 series au baadhi ya midrange za Poco na A-series za Samsung

Ni vyema kutaja bei ya simu unayoitaka ili tuangalie ipi itafaa zaidi kwa bei hiyo
 
Mbona huzungumzii Huawei 60 Pro? Je, baba lao duniani kwa sasa Huawei Mate 60 Pro una la kusema?
Niliacha kufuatilia Huawei mazima ndio maana niliposikia kuhusu Huawei Mate 60 Pro nilikuwa naichukulia kawaida mpaka nilipozifuatilia juu juu

Huawei Mate 60 Pro imenikosha kwanza kwa kutumia chipset yake mwenyewe "Kirin 9000S" ambayo manufacturing process yake ni 7nm
Pili katumia GPU yake ya "Maleoon 910 MP4", kwenye display protection hajategemea Gorilla glass ila kaamua kutumia "Huawei Kunlun Glass 2" pia inatumia HarmonyOS 4.0 badala ya Android kwa China

Ila kwa upande wangu naona Xiaomi 14 Pro ni bora zaidi kwa sababu
*Xiaomi inatumia Android 14 ambayo nadhani ni better kuliko HarmonyOS. Android ina watumiaji wengi na pia developers wengi wametengeneza apps nyingi kwa ajili ya Android. Xiaomi 14 Pro inategemea Google PlayStore kama main app store ya simu ambayo ni bora kuliko Huawei App Gallery
*Xiaomi 14 Pro inatumia chipset ya Qualcomm Snapdragon 8 Gen 3 (4nm) ambayo ina nguvu kuliko "Kirin 9000S (7nm)" ya Huawei Mate 60 Pro.
Kwa kuangalia benchmark naona Mate 60 Pro inapata total of 700000 AnTuTu score ambayo hii ni ndogo sana, level moja na Google Tensor G2 ya kwenye Google Pixel 7A. Ina maana hata midrange ya Xiaomi (Xiaomi Redmi Note 12 Turbo/ Poco F5) inaishinda Huawei Mate 60 Pro kwenye performance
*Xiaomi 14 Pro ina access ya Google services ambazo ni popular kuliko za Huawei
*Xiaomi 14 Pro ina hadi 16GB RAM na UFS 4 ukilinganisha na UFS 3.1 kwenye Mate 60 Pro
*Pia kwenye kamera chance kubwa inaonesha Xiaomi 14 Pro ipo mbali kuliko Huawei kupitia LEICA collaboration

Huawei Mate 60 Pro ni simu nzuri ila sio bora kuliko Xiaomi 14 Pro.
Hata Google Pixel 8 Pro iko vizuri kuliko hii flagship mpya ya Huawei
 
Sijaona siku ya kupambana na S23 hapo.
Samsung Galaxy S23 inafananishwa na Xiaomi 13, sio hata 13 Pro.
Unless uwe unaongelea S23 Ultra ambayo kwenye performance haiifikii hata Xiaomi 13 Ultra ambayo ilitoka kabla ya Xiaomi 14 series

Samsung Galaxy S23 Ultra ni simu tu iliyotimia kila kona na kufaa watu wengi. Ila Xiaomi 14 Pro iko vyema kuliko S23 Ultra
 
Xiaomi 14 na 14 Pro kwa sasa zipo China tu na bei zake ni

Xiaomi 14 kwa 520Euros (About TSh 1,445,000/=)
Xiaomi 14 Pro kwa 650Euros (About TSh 1,800,000/=)

Zikiachiwa globally bei itakuwa kubwa zaidi
Thanks
 
Xiaomi 14 na 14 Pro kwa sasa zipo China tu na bei zake ni

Xiaomi 14 kwa 520Euros (About TSh 1,445,000/=)
Xiaomi 14 Pro kwa 650Euros (About TSh 1,800,000/=)

Zikiachiwa globally bei itakuwa kubwa zaidi
Haya mambo ndiyo yanayonikera, wachina, wakitoa simu zao utasikia zinatumika china tu kwanza Wengine baadaye. Mbona apple au sumsung mambo hayo hawana?
 
Haya mambo ndiyo yanayonikera, wachina, wakitoa simu zao utasikia zinatumika china tu kwanza Wengine baadaye. Mbona apple au sumsung mambo hayo hawana?
Ukiona hvyo ujue wana soko kubwa sana la ndani, kumbuka population ya China ni 1.4 Billion
 
Haya mambo ndiyo yanayonikera, wachina, wakitoa simu zao utasikia zinatumika china tu kwanza Wengine baadaye. Mbona apple au sumsung mambo hayo hawana?
Hata hivyo Samsung anachelewa kutumia chipset mpya.

Bora hiyo Xiaomi 14 Pro inaexist na inatumia Snapdragon 8 Gen 3.
Samsung itakayotumia Snapdragon 8 Gen 3 ni Samsung Galaxy S24 Ultra ambayo itatoka February 2024
Mpaka kufikia muda huo Xiaomi 14 Pro Global version itakuwa imeshatoka.

Acha wauze nyumbani kwao kwanza maana ndio soko lao kubwa la flagship liliko.
 
Redmi Note 11 Pro ni bora kwenye kila kitu kuliko Redmi 12C, kuanzia kamera, display, performance, software, design, call quality na kila kitu tena kwa gap kubwa sana kwa sababu Redmi Note 11 Pro ni midrange na Redmi 12C ni low end phone
Kwa Tanzania naona Redmi Note 11 Pro inauzwa kwa 600,000/= halafu Redmi 12C inauzwa kwa 240,000/=. Hata bei zinaonesha utofauti uliopo baina ya hizi simu mbili

Redmi Note 11 Pro ni simu ya muda, sasa hivi Note 12 series zimeshatoka na Note 13 series zimetoka pia kwa hiyo kama unataka Redmi Note series ni heri ununue Redmi Note 12 series au Note 13 series au baadhi ya midrange za Poco na A-series za Samsung

Ni vyema kutaja bei ya simu unayoitaka ili tuangalie ipi itafaa zaidi kwa bei hiyo
Hii Redmi 13c pro ni mediatek, vp hii processor ipo poa?
 
Apple wako nyuma inapokuja suala la features mpya kwenye simu. Kila mwaka wakiongeza features tatu au nne imeisha hiyo
Mkuu naomba uongelee na laptop zisizo na majini huku kwetu, eg za Xiaomi, tumechoka na hizi zilizozoeleka huku.
 
Back
Top Bottom