Xiaomi wamekua wakitoa models za Xiaomi (zamani Mi) flagship tokea 2011 walivyotoa Mi 1 hadi 2021 wakaona waziite tu Xiaomi 12 na kuachana Mi.
Sasa mwaka jana walitoa Xiaomi 15 ikiwa na simu nne. Xiaomi 15 base, 15 Pro, 15 Ultra na 15S Pro. Kwahiyo tukajua mwaka huu watatoa Xiaomi 16.
Wametangaza jana Xiaomi 17 base, Xiaomi 17 Pro na 17 Pro Max.
Najua ni naming tu kama Samsung alivyoskip Note 6, au walivyotoka S10 wakaruka hadi S20 ila wao kidogo walikua na reasons. Ila hawa Wachina ni kama wanataka wapambane na iPhone 17 series hivi?
Okay, simu zenyewe ni kali na zina design unique.
Xiaomi 17
Kioo 6.3 inch OLED , SoC mpya Snapdragon 8 Elite Gen 5, RAM 12 au 16 GB, Storage 256GB au 512GB, Battery 7,000 mAh, nyuma camera tatu (main, ultrawide, na telephoto) kila moja 50MP na ya mbele pia 50MP.
Bei kuanzia Mil 1.6 hadi 1.8 kutegemea RAM na storage.
Xiaomi 17 Pro na Xiaomi 17 Pro Max
Kwa mbele kama mdogo wao 17 ila kwa nyuma kuna screen imeongezeka kwaajili ya wapenzi wa selfie na kusaidia notification.
Bei zake za moto zinatoka Mil 1.7 hadi 2.6 hivi.
Wapenzi wa Xiaomi mzigo huo. Ngoja tuone baba yao Samsung ataleta nini kwenye Galaxy S26 February.