Ya Adani na Wachina: Hii ndiyo sababu kuu inayofanya Wanasiasa wetu wawachukie Wazungu

Ya Adani na Wachina: Hii ndiyo sababu kuu inayofanya Wanasiasa wetu wawachukie Wazungu

Kama Elon Musk katoa Rushwa lazima utakuja kuona anachunguzwa na kufikishwa Mahakamani. Huyo Trump tu ameshachunguzwa mara kadhaa na kufikishwa Mahakamani.

Mtoto wa Joe Biden, Rais wa sasa wa Marekani amechunguzwa na kufikishwa Mahakamani kwa tuhuma kadhaa tena Baba yake akiwa Rais.

Huu ndo utofauti wa wazungu na sisi waafrika.
Uko sahihi, ila in deep wazungu hawana nia kumthamini Mwafrica. Angalia Congo, Msumbiji, na kote kwenye vurugu za mauaji mabaya ya waafrica, ni makampuni ya kizungu kupora mali za weusi ili kutengeneza bidhaa zitakazouzwa tena kwa waafrika kwa bei kubwa kama simu, silaha nk
 
Ushushaji na Upakiaji wa makontena kasi yake imeongezeka, muda wa kuhudumia meli moja umepungua.

Malalamiko ya wateja kuhamia bandari za nchi jirani yamepungua sana, mapato ya TRA yameongezeka sana.

Sio mimi niliyesema kuwa ubora wa kazi umeongezeka, ni gazeti mojawapo maarufu la kingereza linalotoka jijini Dar lilikuja na hiyo habari.
Hilo gazeti ndio wamesema tunaongoza afrika mashariki?? Ungeiweka hiyo taarifa

Kuhusu mizigo ushushaji na upakiaji, ufanisi, mapato na mengine haya yote mbona yalikua yanaongezeka sana kabla hata ya Dp world? Je serikali ilikua inatuongopea?
Soma chini taarifa za ufanisi, mizigo na mapato kuongezeka wakati huo kabla ya dp world

Hapana huu ni ukweli. Mimi ni mdau wa Bandari nimeliona hilo
Sio kweli. Hayo yote yamekua yakiongezeka kabla ya ujio ya dp world.
Taarifa hizi walizileta wenyewe, ikafikia TPA kupewa tuzo ya ufanisi bora
 
Najua huu uzi hautapata wachangiaji wengi kwa sababu Watanzania wengi ni mazuzu. Hawaelewi unyeti wa kodi zao na wanawaona wanasiasa kama miungu ambao wanaweza fanya chochote na hela zao bila kuhojiwa au kufanywa chochote.
🙏 👍
 
Uko sahihi, ila in deep wazungu hawana nia kumthamini Mwafrica. Angalia Congo, Msumbiji, na kote kwenye vurugu za mauaji mabaya ya waafrica, ni makampuni ya kizungu kupora mali za weusi ili kutengeneza bidhaa zitakazouzwa tena kwa waafrika kwa bei kubwa kama simu, silaha nk
Siku mtakapo tambua kuwa shida zenu zinawahusu nyie zaidi(Waafrika)na sio wazungu,ndipo mtakapo acha huu uzuzu wa kutupa lawama kwa wazungu.

Ufisadi mfanye wenyewe,mikataba ya kimangungo msaini nyie, matumizi ya pesa ya umma mnatumia kwenye anasa na sio maendeleo,bunduki mnunue nyie muuane wenyewe,alafu lawama muwape wazungu kweli ?

Katika kitabu chake Mwl.Nyerere Cha "Tujisahihishe" anasema kwamba pale tunapo shindwa kutatua matatizo au changamoto zetu mara nyingi tumekuwa tunatoa lawama kwa wakoloni(wazungu),waarabu na wahindi,jambo ambalo sio sahihi kabisa ,tufike hitimisho baada ya kufanya tafiti(Research).
 
Kwa huu uzi wako tayari huyo adani ameshakuwa na hatia, kwa ushahidi upi usiotiliwa shaka kwamba habari yako ina ukweli mtupu ndani yake?.

Tatizo la taasisi nyingi za afrika tija inakuwa ni ndogo na sababu zipo nyingi sana. Ukiona wanasiasa wanakimbilia nje kutafuta taasisi za kigeni ujue hizi za kwetu zina matatizo mengi.

Wizi mwingi, nidhamu ndogo kazini, urasimu mwingi, badala ya taasisi kurahisisha maisha ya kijamii inakuwa ni sehemu ya kero zinazokwamisha kupiga hatua.

DPW kaleta tofauti pale TPA hivi sasa bandari yetu inaongoza kwa tija katika ukanda huu wa afrika, tulipokuwa sisi wenyewe tunaiendesha kila siku tulizoea kusoma habari za wateja kuelekea Kenya na Msumbiji wakiikimbia bandari iliyojaa upigaji wa kila aina.

Tambua kwamba wanasiasa na udhaifu wao wa miaka na miaka, wanalo lengo jema kutafuta wawekezaji wa kigeni.
Sasa kwanini msijenge taasisi simamizi imara??
Kwa maana hiyo hata hizo taasisi za nje zikianza kuwaibia hamtajua ama lah hamtokua na la kuwafanya maana ndizo tabia zenu.
 
Siku mtakapo tambua kuwa shida zenu zinawahusu nyie zaidi(Waafrika)na sio wazungu,ndipo mtakapo acha huu uzuzu wa kutupa lawama kwa wazungu.

Ufisadi mfanye wenyewe,mikataba ya kimangungo msaini nyie, matumizi ya pesa ya umma mnatumia kwenye anasa na sio maendeleo,bunduki mnunue nyie muuane wenyewe,alafu lawama muwape wazungu kweli ?

Katika kitabu chake Mwl.Nyerere Cha "Tujisahihishe" anasema kwamba pale tunapo shindwa kutatua matatizo au changamoto zetu mara nyingi tumekuwa tunatoa lawama kwa wakoloni(wazungu),waarabu na wahindi,jambo ambalo sio sahihi kabisa ,tufike hitimisho baada ya kufanya tafiti(Research).
Weupe wote wanatumia hila kupata mali za Mwafrica, baada ya kutambua sisi kweli hamnazo kichwani. Ninachokataa ni kumuona mzungu ana afadhali kuliko yeyote.
 
Weupe wote wanatumia hila kupata mali za Mwafrica, baada ya kutambua sisi kweli hamnazo kichwani. Ninachokataa ni kumuona mzungu ana afadhali kuliko yeyote.
Endelea kuishi kwa kuraririshwa!

Mzungu angekuwa hana afadhali angekurudishia chenji yako ya Rada?
 
Hilo gazeti ndio wamesema tunaongoza afrika mashariki?? Ungeiweka hiyo taarifa

Kuhusu mizigo ushushaji na upakiaji, ufanisi, mapato na mengine haya yote mbona yalikua yanaongezeka sana kabla hata ya Dp world? Je serikali ilikua inatuongopea?
Soma chini taarifa za ufanisi, mizigo na mapato kuongezeka wakati huo kabla ya dp world

Kumbuka kuwa volume inategemewa kuwa kubwa sana itakapofika wakati SGR ikawa na uwezo wa kuutoa mzigo Rwanda ilipo yard ya DPW na kuuleta bandarini.

Anahitajika mwekezaji mwenye uwezo wa kwenda na kasi ya wakati huo ambaye pia yupo vizuri kiteknolojia kuliko hali ilivyokuwa. Kumbuka kuwa DPW ni mmiliki wa mzigo unaotoka Rwanda, Burundi na DRC hautakuwa mzigo wa kitoto.

Logistic supply chain kwa maana ya mzigo kutoka huko bara ukaja kwa treni na kisha ukapanda melini ni shughuli nzima anayokwenda kuifanya DPW hivyo tunapoiongelea bandari huo ndio mtazamo wa kutakiwa kueleweka.

Inawezekana uboreshaji ulifanyika lakini tuendapo lengo ni uchumi wa nchi kuwa unaitegemea TPA kwa asilimia kubwa kuliko ilivyo hivi sasa.
 
Sasa kwanini msijenge taasisi simamizi imara??
Kwa maana hiyo hata hizo taasisi za nje zikianza kuwaibia hamtajua ama lah hamtokua na la kuwafanya maana ndizo tabia zenu.
Taasisi za nje zinawekeza hata kwenye mataifa ya huko huko nje. DPW aliyewekeza TPA pia kawekeza kule India, ina maana India hawana uwezo wa kukagua mahesabu yao ya kifedha ili kujua biashara ya ubia inakwenda vipi?.
 
Endelea kuishi kwa kuraririshwa!

Mzungu angekuwa hana afadhali angekurudishia chenji yako ya Rada?
Mimi nakubaliana na wewe kabisa ila, bado tambua linapokuja swala la maslahi, weupe wote lao moja. Wazungu walipiga vita biashara ya utumwa sio kwa kutupenda weusi ila kwa sababu ya mapinduzi ya viwanda kwao.
 
Uko sawa pia. Ila bora wazungu kuliko hawa wachina na wahindi wanaokumbatiwa na Viongozi wetu
 
Kumbuka kuwa volume inategemewa kuwa kubwa sana itakapofika wakati SGR ikawa na uwezo wa kuutoa mzigo Rwanda ilipo yard ya DPW na kuuleta bandarini.

Anahitajika mwekezaji mwenye uwezo wa kwenda na kasi ya wakati huo ambaye pia yupo vizuri kiteknolojia kuliko hali ilivyokuwa. Kumbuka kuwa DPW ni mmiliki wa mzigo unaotoka Rwanda, Burundi na DRC hautakuwa mzigo wa kitoto.

Logistic supply chain kwa maana ya mzigo kutoka huko bara ukaja kwa treni na kisha ukapanda melini ni shughuli nzima anayokwenda kuifanya DPW hivyo tunapoiongelea bandari huo ndio mtazamo wa kutakiwa kueleweka.

Inawezekana uboreshaji ulifanyika lakini tuendapo lengo ni uchumi wa nchi kuwa unaitegemea TPA kwa asilimia kubwa kuliko ilivyo hivi sasa.
Umeandika vitu visivyoeleweka. Dpw ni mmiliki wa mzigo unaotka drc, Burundi na Rwanda kivipi? Wanamiliki hiyo mizigo kivipi?

Pili hoja yako ilikua kwa sasa kuna ufanisi na ongezeko la mapato, wakati tupo sisi wenyewe kulikua hakuna ufanisi Wala ongezeko la mapato. Hapo ndio tulianza huu mjadala. Haya ya sgr, Mara drc, mara Rwanda yanakuja wapi?
 
Uko sawa pia. Ila bora wazungu kuliko hawa wachina na wahindi wanaokumbatiwa na Viongozi wetu
Soma HISTORIA ya wazungu,, wafaransa na uporaji wa mali Africa na jinsi walivyoanzisha vikundi vya kigaidi kote west Africa kulinda mali zao. Juzi juzi tu hao mabedui wamemuua Gadafi na kupora mafuta. Waupe wote hila kwenda mbele. Na maafrica majinga jinga tu.
 
Taasisi za nje zinawekeza hata kwenye mataifa ya huko huko nje. DPW aliyewekeza TPA pia kawekeza kule India, ina maana India hawana uwezo wa kukagua mahesabu yao ya kifedha ili kujua biashara ya ubia inakwenda vipi?.
Unaniuliza as if mimi ni kanjibai!!

Kwahiyo kisa fulani kafanya basi na ninyi mnaiga??
 
Pamoja na yote Mzungu ni mtu aliyenyooka sana!

Mzungu kawekeza sana kwenye suala la utawala bora ambapo kupitia utawala bora amejenga Taasisi na mifumo imara sana zinazosimamia mambo na kuhakikisha yanaenda bila shida.

Kunyooka huku kwa Mzungu ndiko kumefanya sasa aanze kupoteza sana Africa. Hii ni kwa sababu Viongozi wa Afrika wanapenda sana Rushwa. Kupenda Rushwa kwa Viongozi wa Afrika ndiko kumefanya kwa sasa bara la Africa kuongoza kwa uwekezaji wa Wachina na Wahindi.

Mchina na Mhindi ni watu wanaoamini kuwa ili jambo lake liende lazima atoe Rushwa. Endapo siku ikitokea ukafanyika uchunguzi huru wa namna kandarasi za Wachina na Wahindi zinavyopatikana hapa Tanzania na Afrika nawaambia wananchi wetu wanaweza choma nyumba zote za Viongozi wetu sio tu Tanzania bali Afrika nzima.

Waendesha Mashtaka wa Marekani kufungua Mashtaka dhidi ya tajiri wa kihindi Adani ni funzo kubwa kwetu kuwekeza kwenye katiba bora inayojenga na inayosimamia mifumo imara. Mifumo isiyotoa nafasi kwa rushwa na kuhakikisha fedha zote za walipakodi zinatumika kwa maendeleo ya wananchi tu na sio kuwanufaisha wachache.

Hapa Tanzania Adani kapewa sehemu ya Bandari yetu. Huwezi sikia hata siku moja PCCB wakifanya uchunguzi. Na kamwe hatutosikia. Hii ni kwa sababu Adani ameingia Tanzania kupitia Ofisi namba moja.

Sio mara ya kwanza kwa mzungu kuonyesha umuhimu wa Mifumo na Taasisi imara kwenye utawala bora. Tanzania tulishawahi rudishiwa chenji yetu ya Rada baada ya Wazungu kugundua kuwa kampuni zao zilitupiga na wakazibana zikarudisha kweli.

Kuna kipindi Bandarini Wazungu waligundua kuna kampuni zao zilitoa Rushwa kupata tenda za kufunga mifumo ya tehama kwenye Bandari yetu. Ila pamoja na Ile kampuni kubanwa nchini mwao hapa kwetu hatujasikia hadi leo wahusika wakifikishwa Mahakamani.

Kusema kweli ili tuendelee tunawahitaji sana Wazungu kuliko hawa wachina na wahindi wanaojenga miradi ya hovyo iliyo chini ya kiwango tena kwa pesa nyingi ambazo zinaenda kutumika kama Rushwa kuwanufaisha wachache.

Najua huu uzi hautapata wachangiaji wengi kwa sababu Watanzania wengi ni mazuzu. Hawaelewi unyeti wa kodi zao na wanawaona wanasiasa kama miungu ambao wanaweza fanya chochote na hela zao bila kuhojiwa au kufanywa chochote.
View attachment 3158628

Ipo siku

Lord denning
Qatar
Sisiemu watakuelewa ..
 
Adani hakuna.sehemu.aliyowekeza hajatuhumiwa kwa dhuluma na rushwa ni muhuni kama.wahuni.wa.kichina hawa.waliojaa hapa.

Huwa najiuliza kwanini nchi zingine.zinapata.investor kutoka continental.europe ila sisi tunapata.wachina hawana.utu. adabu. Hawalipi wafanyalazi hela.nzuri wapo wapo tuu na bado tunawakumbatia.

Huwezi kwenda Rwanda ukasikia mchina ana kiwanda cha misumari itasikia mspain. Mtaliani au mfaransa
 
Wazungu hatuwataki. Kwanza wabishi na wengi wana mkono mfupi. Wachina huwa wanatoa bakshishi na wahindi halafu hawatupangii siasa zetu.
Hawatupangii siasa zetu,manake haya wahusu muauane,muchinjane,muibiane wao wanachojua wamepiga dili lao.

Wazungu ni race inayo jitambua na wataka woye tujitambue jambo ambalo viongozi wa afrika hawapendezwi nalo.
 
Kweli kabisa
 
Back
Top Bottom