Ya CCM tumeyasikia, yamepita. Turudi kwenye habari ya mjini yaani Mifumo kusomana.

Ya CCM tumeyasikia, yamepita. Turudi kwenye habari ya mjini yaani Mifumo kusomana.

jindundu

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2025
Posts
679
Reaction score
581
CCM wanajua kucheza karata zao vizuri. Wana magwiji wa Mikakati mizuri na ya hovyo pia.

Siyo siri Kombora la mwisho alilotoa Humphrey Polepole kwamba mifumo ya INEC, NIDA na Lumumba inasomana hivyo kupora maamuzi ya watu katika kupiga kura, limewashtua na kukitikisa Chama hicho.

Mabadiriko ya ghafla ya uongozi wa juu wa CCM katika kipindi hiki yaweza kuwa ni njia ya kuwatoa watanzania kwenye mjadala wa hoja hiyo nzito aliyoitoa Polepole.

Watu badala ya kuzidi kushinikiza ufanyike uchunguzi katika mifumo hiyo inayodaiwa kusomana, Sasa tunaimba wimbo wa CCM na mabadiriko yao ya kiuongozi waliyofanya. Hayo yanawasaidia wao, mikakati na malengo yao.

Kadri siku zitakavyoenda, baada ya hili, CCM wataibua jambo jingine Tena, haoo tutaanza kuimba kama kasuku na kubishana humu. mwisho mambo ya msingi aliyosanua Polepole yataishia hapo na kusahaulika.

Tutakuja Tena humu humu kuanza kusema mbona Polepole kakaa kimya? Mbona hatuambii aliyemuua Magufuli na ujinga mwingine mwingi.
 
Back
Top Bottom