Kabla hata sherehe za kufurahia Gekul kufutiwa kesi iliyomkabili , ile ya kumtumbukiza Chupa makalioni kijana mmoja huko Manyara haijaanza , Tayari Mawakili wa Mlalamikaji huyo wametangaza kukata rufaa kupinga Uamuzi wa DPP wa kuifuta kesi hiyo.
Tayari nyaraka zimeanza kukusanywa ili kulianzisha upya jambo hilo.
---
Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka nchini imeondoa Kesi ya namba 179 ya mwaka 2023 ya shumbulio la mwili iliyokuwa ikimkabili aliyekuwa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria ambaye ni Mbunge wa Babati Mjini Pauline Gekul ambapo upande wa Mbunge huyo ilikuwa ikiwakilishwa na wakili Ephraim Kisanga huku upande wa mlalamikaji Hashimu Ally ikiwakilishwa na mawakili watatu ambao ni Thadei Lista,Peter Madeleka na Joseph Masanja.
Kesi hii kwa mara ya kwanza imesikilizwa hii Leo katika mahakama ya wilaya ya Babati Mkoani Manyara na Hakimu wa mahakama hiyo Victor Kimario ambapo amesema kesi hiyo imeondolewa kwa mujibu wa sheria namba 91 kifungu kidogo cha( 1) cha sheria ya mwenendo wa mashauri ya jinai sura namba 20 Kama ilivyorekebishwa mwaka 2022, ambayo inampa mkurugenzi wa mashitka mamlaka ya kuondoa kesi yeyote ya jinai mahakamani kabla haijafikia hukumu.
Kwa upande wa Mawakili wa mlalamikaji wameelezwa kutokuridhishwa na kitendo kilicho endelea mahakamani hususani kufutwa kwa kesi hiyo na wameeleza kukata rufaa.