Rebeca 83
JF-Expert Member
- Jun 4, 2016
- 15,136
- 32,268
Ni hivi Rebecca,
Nadhani unaamini mwanaume ndiye kichwa cha familia.Sasa kuna nyakati ngumu ambapo labda hela hamna halafu linatokea jambo ambalo linahitaji hela nyingi halafu ukifika tuu nyumbani unaambiwa mtoto alirudishwa ada na mama anakukumbushia hitaji lake.Inabidi ubehave as if everything is under control hata kama hujui utafanyaje.Na sio kujifungia chumbani na kuanza kulia mbele ya mkeo eti hauna hela.
Mmepata shida kama familia, hata kama imekuumiza, inabidi wewe ndiwe uanze kuwatia wenzio moyo.
Bahati mbaya mtoto wenu wa pekee mliyekua mkimsubiria kwa hamu bahati mbaya mama akajifungua mtoto akiwa amefariki, hapa inabidi uwe mstari wa mbele kumtia moyo mkeo n.k
Sasa kwenye mazingira kama haya(na yanayofanania hayo) ukianza kulia huo ndio udhaifu tunaozungumzia hapa.Baba ukianza kulia, mkeo afanyeje sasa?
Unawatia moyo wanaokuzunguka halafu baadae unatafuta faragha ya kujituliza kwa kinywaji, marafiki n.k
Sent using Jamii Forums mobile app
Kulia hakukuzuii kufanya mambo mengine,Kama kwenye hio scenario hapo kwani MC Pili pili si eventually alimvisha hio pete??au alilia akarudi na Pete yake??kukosa Ada ya Mtoto kunaweza kumfanya mke au mume alie Ndio,lakini baada ya kulia si unatafuta Ada?? Kwanza kulia baada ya kukosa Ada kuna release tension mapema hivyo inakupa muda zaidi wa ku focus......,