Huwa sipotezi muda na ngonjera hizi, lakini hata sijui nimefungua vipi hii sanaa leo.Ifahamike, huyo Makamu si Hayati baba wa Taifa kwamba eti aendelee kubembelezwa kama mtoto. Yeye si lolote kwamba Chama na Taifa ki/litapungukiwa na kitu pasipo yeye.
Nafuu na jambo jema ni kuwa hata boss wake ameamua kumfungia vioo na hataki tena kujishughulisha naye kwa namna yeyote ile. Uamuzi ni wake!
Nanyi ambao kutwa na kila uchwao mnamshauri Sponsor eti aone namna bora ya kuzungumza na huyo zilipendwa wenu, komeni! Hivi, hamjiulizi kwa nini boss lady anawapiga dana dana kwalo?! Jibu ni moja, ameshaamua kama mbwai na iwe.
Ya safari hii, dogo kawaweza kweli kweli na mbaya zaidi hamkutarajia hata chaguo lake!
Habembelezwi mtu! Na chaguo la boss lady ndilo hilo. Sasa mpende, ama, lau msipende, uamuzi wenu wa ima mu resign ama muendelee kuwamo kundini huku mkiugulia kwa uchungu maamuzi ya Sponsor.
Huyo unayemlilia kichizi ndiye 'master mind' wa chama hicho kilichooza; pasipo yeye mnayo hali ngumu sana.
Kwetu sisi wengine wote tunao tizama ukombozi wa taifa letu, hali haijawahi kuwa ya matumaini makubwa wakati mwingine wowote kuliko ilivyo sasa.
Kwa hiyo ni furaha kwetu mkisambaratishana wenyewe kwa wenyewe.