Wajinga hawataona Impact ya hii miradi inayowekezwa na Serikali ya Chama cha Mapinduzi.
Ila nikwambie. Miradi hii PESA zitakazopatikana zitakwenda moja kwa moja kuhudumia wananchi.
Huwezi kusema ndege hainisaidii wakati kuna Utalii unaotegemea Usafiri wa Anga. Hao wageni watakuja na Bodaboda? Utapataje PESA za kigeni kama huwekezi?
Huwezi kubeza SGR kwamba huta panda Tren hivyo haina Msaada kwako una sahau kwamba Kuna wakulima wanategema usafirishaji wa mazao na mizigo wakipata usafiri wa uhakika na nafuu utapunguza Mfumuko wa bei na kusaidia kupunguza Gharama za maisha.
Huwezi kubeza Mradi wa Bwawa la Nyerere kwamba Hauna tija wakati Viwanda vina hitaji Umeme wa uhakika na wagharama nafuu ili kuongeza uzalishaji na Ajira.
Ndio maana nasema wafuasi wengi wa upinzani Akili zenu ni ndogo sana. Mnawaza kuwa na PESA Mfukoni kuliko kuangalia Vitu vya msingi ambavyo ndio vitakua mkombozi wa watu wengi wa taifa hili.
Hivi umeshajiuliza ukawa na fedha mfukoni Alafu hakuna Miundo mbinu mizuri ikapelekea Mfumuko mkubwa wa bei hivi hiyo hela itakusaidia nini?
Umeshajiuliza Congo ya Mobutu ilikua unaenda kununua mkate na sanduku la Pesa Kutokana na serikali kutokuwekeza kwenye Miundombinu ila iliruhusu watu wawe na PESA Ambazo mwisho wa siku hazikuwasaidia wakamtoa madarakani.
Hivyo wanadamu hawana jema. Hiyo Ndio nature yao. Mimi naipongeza CCM kwa misimamo YAKE chini ya Rais Magufuli. Nchi haiendeshwi kwa kusikiliza watu nchi inaendeshwa kwa kufuata vipaumbele vya msingi na sio kuwanufaisha wachache Bali kwa manufaa ya wengi.