Yaani mwaka 2023, mwezi uandame Rwanda, Kenya na Uganda halafu usiandame Tanzania! Hapa kuna utapeli kwa 100%

Yaani mwaka 2023, mwezi uandame Rwanda, Kenya na Uganda halafu usiandame Tanzania! Hapa kuna utapeli kwa 100%

inaonekana South Africa nako Eid ni leo, Saudia, UAE, Kenya, Uganda, Rwanda nk kote Eid ni leo... Tanzania Eid Kesho kwa niaba ya Mufti..

Kuna usemi unasema, yasiyowezekana duniani kote huwa Tanzania yanawezekana.

Wanazuoni Watanzania wanapaswa kulijadili hili kwa pamoja maana dhima hii iko kwao na kulitolea ufanunuzi pamoja na msimamo ili waislamu wa Tanzania wasiendelee kuyumba.
 
...Mimi nilishangaa kwamba SAA TATU Usiku Mufti Zanzibar kutangaza Redioni na kwenye TiiVii kuwa Mwezi haujaonekana Kwa Hiyo Ijumaa Watu wanaendeles na Mfungo na Sikukuu ni Jumamosi! SAA TATU USIKU !

Nikashangaa Sana! Walikuwa na haraka Gani ya kusema Mwezi haujaonekana hivyo Mfungo unaendelea?

SI Kuna Eid Mwaka wa Nyuma kidogo walitutangazia SAA NNE USIKU kuwa Mwezi umeonekana Huko Congo na Uarabuni...na Kesho ikawa Eid?

SI Kuna siku Miaka ya Nyuma Enzi za Baba wa Taifa kuonekana Mwezi kulitangazwa Alfajiri wakati Watu wanajiandaa kwenda Makazini...na ikawa Eid?

Hii ya kutangaza SAA TATU USIKU kuwa Mwezi haujaonekana na Kesho Ijumaa Watu waendelee kufunga, na maelezo mengine Kibao, ya Nini???
Walijuaje kwamba hawataletewa taarifa za kuonekana Mwezi SAA NNE USIKU ???
Kuna Neno !....[emoji35]
 
Sababu kesho msipoenda kazini serikali inapoteza mapato makubwa
Bakwata =serikali so kachepi kazi.
 
Bila kuzingatia kwa mwaka huu 2023 nani yuko sahihi kati ya wale waliosema mwezi umeandama Kenya, Uganda na Rwanda (hivyo ijumaa ni sikukuu) dhidi ya wale waliosema mwezi haujaandama Tanzania (hivyo Ijumaa watu waendelee kufunga), hapo kuna harufu ya Uongo na utapeli kwa 100%.

Sote tunajua mwezi ni mmoja dunia nzima, na jiografia ya Rwanda, Kenya, Uganda na Tanzania inashahabiana sana huku nchi zote hizo zikiwa na jirani. Sasa inakuwaje suala la muandamo wa mwezi likatofautiana hivyo?

Hapa kuna utapeli kwa 100%
Wewe una akili Sana. Huu ni utapeli mkubwa Sana! Hawa BAKWATA??? Wajitafakari Sana!
 
Bila kuzingatia kwa mwaka huu 2023 nani yuko sahihi kati ya wale waliosema mwezi umeandama Kenya, Uganda na Rwanda (hivyo ijumaa ni sikukuu) dhidi ya wale waliosema mwezi haujaandama Tanzania (hivyo Ijumaa watu waendelee kufunga), hapo kuna harufu ya Uongo na utapeli kwa 100%.

Sote tunajua mwezi ni mmoja dunia nzima, na jiografia ya Rwanda, Kenya, Uganda na Tanzania inashahabiana sana huku nchi zote hizo zikiwa na jirani. Sasa inakuwaje suala la muandamo wa mwezi likatofautiana hivyo?

Hapa kuna utapeli kwa 100%

Kila nchi na mipango yake
Kwani wewe uliuona mwezi😂😂😂
 
Mufti wa Tanganyika na wa Zanzibar na wa Kenya wanapeana taarifa za mwezi wakati wa Idd. Sasa wote kwa pamoja wametamka mwezi haujaonekana. Sasa kuleta hoja kuwa Kenya kesho ni Idd kuna lengo gani? Kwa Uganda na Rwanda sidhani kama kuna mashirikiano hayo. Ila tuache kupotosha
Acha unaa wewe!
 
Back
Top Bottom