Yaani tumewahonga Mtibwa Sugar FC tushinde nyingi ili Mashabiki wajae Mechi na Horoya FC tupige Pesa?

Yaani tumewahonga Mtibwa Sugar FC tushinde nyingi ili Mashabiki wajae Mechi na Horoya FC tupige Pesa?

Hovyo kabisa mbona huu Mpira wa leo Wachezaji wetu hawakuucheza Mechi kama Nne zilizopita na tukawa tunashinda kwa Taabu huku Sisi Mashabiki wenu GENTAMYCINE nikiwepo tukiwa tunajituliza kwa Dawa za Maumivu za Panadol?

Nitarudi hapa baadae Saa 4 Kamili na mengineyo.
Yaani wewe ni kunguru asiyefugika. Simba wakifungwa au wakishinda kwa goli moja kelele, wakishinda goli nyingi kelele pia. Hebu acheni kuwapa stress zisizifaa wachezaji na benchi la ufundi.
 
Wachambuzi na wapenzi wa yanga wengi ni vilaza wa mpira.

Huyu mhuni aliyeleta uzi ni kati ya watanzania wasiofikiri hata kidogo. Saikolojia ya mtibwa tu pekee ilitosha kuwafunga hata goli 8.Ila kwa vile tuna aina ya watu wajinga wajinga wanaojua kuandika mitandaoni na kupata airtime kwenye media zetu,kusikia ujinga kama huu tutegemee tu
Wewe ni zaidi ya kilaza Sasa maana Kila Yanga akishinda unakuja na Uzi wa malalamiko ya bahasha, Sasa genta Huwa Hana unafiki na anajua hii Michezo ya bahasha vizuri kuliko wew mbwiga na saa 4 anakuja na ushahidi. Kaa kwa kutulia
 
Mtibwa kapigwa kwa haki. Magoli yote ya kupambania.

Sema mengi kwa Simba, sema kuna wachezaji wazee, sema kuna wakati wanacheza kifaza, sema kuna wachezaji wa chini ya kiwango yote hayo naweza kukubaliana nawe kwa kiwango fulani ila ambacho siamini ni Simba kununua games za NBC. Mpaka sasa msimu huu sijaona dalili zozote za hilo kufanyika.

Cha nyongeza, kongore kwa Mtibwa. Uwanja wao nimependa nyasi zake. Wajitahidi wajenge hata vibenchi vya watazamaji kukaa. Si haki mtu kulipia kuangalia mechi halafu hauna hata siti ya kukaa.
 
We nae maandazi tu. Timu gani huwa inacheza kwa kiwango sawa kila mechi?
Nilipoandika huu Uzi nilijua tu kuwa kuna Majuha na Wapuuzi watakurupuka na Kutonielewa na ningeshangaa kama wasingejitokeza.

Jamani GENTAMYCINE sijawa Mshindi wa Jukwaa hili la Michezo ( Sports ) kwa Mwaka jana ( 2022 ) kwa Kubahatisha bali ni kwa Uwezo wangu wa Kitaarifa, Uchambuzi na Uibuaji wa Hoja Tunduizi zenye Mvuto na Ushawishi kwa Wasomaji.

Na leo narudia tena ( na hii itakuwa ni mara ya mwisho ) kuwaambieni kuwa GENTAMYCINE najuana na nipo karibu kwa 95% na Wachezaji wa Simba na Yanga na pia kwa 75% na Viongozi na Watendaji wa hivi Vilabu Vikubwa hivyo nikija na Taarifa hapa jueni kuwa nimepenyezewa na hao hao na bahati nzuri niliyonayo ni kwamba Wote nipo nao ila hawajui na hawatokuja kujua kuwa Mimi ndiyo GENTAMYCINE wa JamiiForums.

Kingine nikisema kuwa katika Soka la Tanzania ( Bongo ) kuna Michezo michafu mingi ( hasa utoaji wa Rushwa kwa Waamuzi, Wachezaji na Timu ) muwe mnanielewa kwani hata Mimi GENTAMYCINE mwaka 2012 Yanga SC ilipofungwa Goli / Bao zile 5 kwa 0 nilishiriki kwa 100% katika Umafia kwa Kushirikiana na Wachezaji Waandamizi wa Yanga SC na Kufanikiwa.

Na hapa isionekane labda GENTAMYCINE naisema tu Simba SC ( ambayo naishabikia ) ila ukweli ni kwamba hata Yanga SC nao kwa 100% wanafanya hivyo hivyo isipokuwa kwa sasa Maovu ya Yanga SC yanafichwa na Kikosi chake Imara, Mahiri na Bora tofauti na chetu Simba SC ambacho ni cha Kujitafuta ( Kibovu ) na hakitoi Matumaini yoyote yale kwa hii Misimu / Miaka miwili mfululizo.

Kilichofanyika leo ni Wachezaji wa Mtibwa Sugar FC Kupoozwa ( Kulainishwa ) na Mafia wa Simba SC ili Wasikaze na Simba SC icheze Mpira mwingi na ishinde Bao / Goli nyingi ili Kurejesha matumaini kwa Mashabiki wa Simba SC ambao 97% wameshakata Tamaa na Kuchukizwa na Soka Bovu na Ushindi wa Mungu Nisaidie ( wa Kubahatisha ) na wajitokeze kwa wingi tarehe 18 Machi, 2023 Uwanja wa Mkapa Simba SC ikicheza Mechi muhimu ( ya Kimaamuzi ) kwa CAFCL na Watu wapige Pesa kwa Nyomi litakalokuwepo.

GENTAMYCINE nawajua hadi Wachezaji waliopewa Mzigo mpaka Waratibu wa Zoezi hilo ( ambao Watatu walishawahi kuwa Wachezaji wakubwa hadi Manahodha ) na Viongozi Wawili wa Klabu hiyo ambao wamefanikisha Kimafia Simba SC kushinda leo.

Namalizia kwa kusema kuwa sikulazimishi na sijakulazimisha Uamini nilichokisema hapa ila Siku zote Silaha Kuu ya GENTAMYCINE ni Kujiamini kwa Mambo yangu na Taarifa na huwa sibahatishi / sizibahatishi kwani huwa ni za uhakika na zinatoka Jikoni kwenyewe na siyo Sebuleni au Kibarazani.

Na ukiona Umekwazika / Umechukizwa nami GENTAMYCINE kwa nilichokiandika au basi tu hunipendi kutokana na Umaarufu wangu mkubwa hapa JamiiForums au kwa Uwasilishaji wangu wa Kipekee wa Masuala Mtambuka nakurahisishia Kazi tafuta popote pale Sumu ya Panya changanya na Dawa ya Mbu katika Kikombe cha Maji kisha ukinywe ili Ufe na ukatuandalie Makazi mema Ahera.

Imeisha hiyo...........................Kudadadeki

Mimi ndiyo GENTAMYCINE The King!!!!

Cc: KANYIMBI, Tui, Cashman, Kalpana, mganda og, Vontec
 
Wewe ni zaidi ya kilaza Sasa maana Kila Yanga akishinda unakuja na Uzi wa malalamiko ya bahasha, Sasa genta Huwa Hana unafiki na anajua hii Michezo ya bahasha vizuri kuliko wew mbwiga na saa 4 anakuja na ushahidi. Kaa kwa kutulia
Nimeshawapa Taarifa Kamili kuhusu Tukio hilo kama nilivyoahidi kuwa Saa 4 Kamili nitarejea hapa JamiiForums na kila Kitu.

Mimi ndiyo GENTAMYCINE The King!!!!
 
Back
Top Bottom