bigmind
JF-Expert Member
- Oct 28, 2015
- 12,457
- 12,689
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yaani kitu bado ni tetesi ila ulivowaka utasema una ugomvi binafsi na watu.. Hivi kwa hizi pressure si ikibainika kweli upo kuna mtakao kufa kabla hata hamjaambukizwa ugonjwa wenyewe.. Nyie liombeni tu hili janga iko siku dua zenu zitasikika
Imyuni system yetu iko juuuuuuuuuuuHuu uogonjwa kwann watu weusi hawafiii wakiupataa [emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]
unachokisema kina uhalisia fulani hivi juzi nimezunguka kkoo kama masaa 4 leo sijielewi kabisa kichwa kinauma mafua kwa mbali koo limekauka inshort ninajihisi sipo sawa nimechokachoka dalili za mafua naziona kabisa naomba yawe mafua ya kawaida tu.
Kweli bongo kila mtu ni daktari.. We tayari umejipima na umethibitisha unao! Angalia unachokitamani utakipata, maneno yanaumba
Upo nchi gani kwani?Mtakufa kama kuku wenye mdondo haki ya baba mlivyojazana kwenye hako kamji kama nguruwe mtajuuuta!
Nitashukuru mno maana Rais Magufuli ndio itakuwa tiketi yake rasmi kuhamia Dodoma
Ni hivi.. huu si muda wakuacha mipaka wazi.Huu sio muda wa kusafiri safiri kwenda nchi za mbali hasa ulaya lakini bado watu ni viburi. Diamond na timu yake anafanya tour ya europe hivi sasa hii ni hatari hasa ukizingatia kushikana mikono na mashabiki wakati wa show. Huyu angepata ushauri a postpone hizo show zake kipindi hiki wasije kuchuma janga huko wakaja kula na wabongo huku. Huu ugonjwa ni nyoko unakimbia kama moto kwenye majani makavu
ni kweli si muda wa kuacha mipaka wazi,ila na watanzania kusafiri safiri hovyo wapunguze kama hakuna ulazima sana kama safari ya matibabu.nchi nyingi corona imeingizwa na raia wa nchi husika waliokwenda kutalii nchi nyingine zenye maambukizi.Nchi nyingi za ulaya corona imeingizwa na raia wa nchi husika.nchi za ulaya zilibana zaidi kwa wachina huku raia wao wakiendelea kuzurula tu,matokeo yake umeingizwa na raia wao wenyewe.
Asubuhi hii Kenya imesharipoti kesi.. mtu kutoka usani kweli si muda wa kuacha mipaka wazi,ila na watanzania kusafiri safiri hovyo wapunguze kama hakuna ulazima sana kama safari ya matibabu.nchi nyingi corona imeingizwa na raia wa nchi husika waliokwenda kutalii nchi nyingine zenye maambukizi.Nchi nyingi za ulaya corona imeingizwa na raia wa nchi husika.nchi za ulaya zilibana zaidi kwa wachina huku raia wao wakiendelea kuzurula tu,matokeo yake umeingizwa na raia wao wenyewe.
Huwezi kuzuia spectators bana wee.. haya mambo yapo duniani kote sio hapa tu... kama ikitokea hivyo vyombo husika sasa ndio vichukue hatua kuprove wrong na sio kusema raia wajuaji..Nashangaa watu wanavyolazimisha kuwa tayari Tz Kuna Corona, sijui watapata faida gani kwa uwepo wa hiyo Corona??
Hivi kwanini tumekuwa wajuaji Sana kiasi hiki?? Yaani hapa kwetu likija suala la ugonjwa Kama huu basi kila mtu ni doctor tena wa viwango vya juu, likija suala ujenzi kila mtu ni engineer tena mbobezi haswa.
Likija suala la kiusalama basi kila mtu ni jasusi hatari.
Ukigusa sheria ndio kabisaa wote humu wanakuwa na shahada zao.
Nakumbuka kipindi cha ununuzi wa ndege, daah!! Kulikuwa na wataalamu wa ndege humu hujawahi kuona.
Nakumbuka watu walivyokuwa wanalazimisha kuwepo kwa Ebora hapa daah palikuwa hapatoshi hapa jukwaani kila mtu alikuja na taaluma yake mpya ya udaktari akitoa uthibitisho wa uwepo wa Ebora, leo tena tumehamia kwenye Corona.
Jambo la kushangaza wengine wanasema Corona imetokana na laana ya JK aliyofanya 2015 kuwa katuletea janga. Alafu bila aibu anajiita GT.
Ujinga huu sijui utaisha lini, inashangaza sema.
Mwingine anadiliki kusema et mtakufa nyumba kwa nyumba kana kwamba yeye anamkataba na Mungu hatokufa.
Unajua matatizo tunayo siku zote kila kitu kwetu ni majanga na matatizo sasa ya nn kuogopa tatizo lingine tena la mafua tu ? Piriton zipo tutatumia dawa zetu tulizozoeaComment yako nimecheka, ili hali hili suala ni serious halipaswi mtu kucheka. hahahahah