Yafichuka: Jinsi Tanzania ilivyotia saini mkataba kichaa na kampuni ya siri kuendesha uwanja mkuu wa watalii nchini (KIA)

Tatizo letu sisi lipo wazi, Mlalamishi sio kwamba anakuwa ana uchungu ni kwamba hicho anacholalamikia hana mgao ila akipewa nafasi ya kuwa sehemu ya mgao na yeye anakula na kukaa kimya, na usiombe awe mlamba miguu, atasifia usiamini.
Ukweli wote ndio huu mkuu.
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Ndiyo maana umasikini ni Mkubwa kwenye hii Nchi maana Viongozi wamekosa maono pamoja na kuendekeza upigaji.
Hii nchi ina kundi kubwa la watu masikini ila sio nchi masikini. Ndani ya hii nchi kuna watu wana uhakika wa usafiri, matibabu, mavazi, malazi, chakula, uwekezaji, usafiri na mambo yote ambayo masikini hawezi kuwa nayo wala kuyaota. Kuna mtu akikohoa tu ni airport chap hadi paris kwa chekup.
 
Umesema kweli Mkuu

Yaani mtu akishapata nafasi badala ya kuitumikia Nchi basi atataka aanze kujinufaisha yeye kwanza.

Badala yake mnakuta mna mipango ya maendeleo ya miaka 10 kumi ambayo haitekelezeki kutokana na kukosa fedha ambazo unakuta tayari Viongozi walishazichukua zao mapema 🙌
 
Serikali imetangaza leo kuwa hatimaye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) utakabidhiwa kwa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) inayomilikiwa na Serikali (TAA) kesho, lakini walengwa halisi wa KADCO, kampuni iliyoendesha uwanja huo kwa miaka 25 na kukusanya mabilioni ya mapato, kubaki kufunikwa na siri

*KIA ni uwanja wa ndege wa tatu kwa shughuli nyingi zaidi nchini Tanzania na ndio lango la maeneo makuu ya utalii ya nchi hiyo katika mzunguko wa kaskazini.

CHRONOLOJIA YA MATUKIO:

✅ Tarehe 11 Machi 1998, Kilimanjaro Airports Development Company Limited (KADCO) imesajiliwa BRELA, ikiwa na wanahisa wa ajabu Mott MacDonald International Ltd (99%) na Inter Consult Ltd (1%).

✅ Miezi 3 tu baada ya KADCO kusajiliwa (17 Julai 1998), inaingia mkataba mpya wa umiliki wa hisa, ambapo serikali ya Tanzania ilipata 24% ya hisa za kampuni ya Mott MacDonald International Ltd (41.4%), South Africa Infrastructure Fund ( 30%) na Inter Consult (T) Ltd (4.6%)

✅ Tarehe 10 Novemba 1998, miezi 8 tu baada ya KADCO kuanzishwa, kampuni hiyo ilitia saini makubaliano ya mkataba wa miaka 25 na serikali ya Tanzania, kuipa haki ya kipekee ya kuendeleza na kuendesha KIA, licha ya kutokuwa na rekodi wala uzoefu wa awali katika kuendesha uwanja wa ndege.

✅ Mwaka 2006, serikali ilipitia utendakazi wa KIA na kugundua hitilafu zifuatazo:

* Wanahisa walishindwa kuwekeza katika uboreshaji wa miundombinu katika KIA, na kusababisha utendakazi duni wa uwanja wa ndege

* KADCO ilikuwa hailipi ada yoyote ya makubakiano kwa serikali kwa uendeshaji wa uwanja wa ndege licha ya kukusanya mapato. Hakukuwa na kifungu cha ada ya makubaliano katika makubaliano

* Pia hakuna kifungu cha kuvunja makubaliano katika mkataba. Mkataba huo una kifungu cha kusasisha/kuhuisha ukodishaji tu baada ya kila miaka 15 wakati mkataba wa miaka 25 unaisha.

* Mkataba wa makubaliano UNAZUIA ujenzi wa uwanja wa ndege wowote wa kimataifa ndani ya eneo la kilomita 240 kutoka upande wowote wa KIA, hivyo basi kuipa KADCO haki za kipekee za kuendesha uwanja wa ndege pekee wa kimataifa katika eneo hilo.

✅ Wakati serikali ilipotaka mapitio ya masharti yasiyokubalika ya mkataba wa makubaliano, wanahisa WALIKATAA marekebisho yoyote. Mnamo 2009, serikali iliamua kuwanunua wanahisa wa kampuni na kupata umiliki wa 100% wa KADCO. Bado haijabainika ni kiasi gani serikali ILILIPA wenyehisa ili kuwanyima umiliki.

✅ KADCO iliendelea na uendeshaji wa KIA, licha ya serikali kuchukua umiliki wa kampuni kwa asilimia 100 huku kukiwa na maswali ya ukaguzi kutoka kwa CAG na Bunge kuhusu mapato yanayokusanywa na KADCO kama mwendeshaji wa uwanja wa ndege.

✅ Tarehe 9 Novemba 2023, Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, alitangaza Bungeni kuwa KIA sasa itakabidhiwa rasmi kwa TAA tarehe 10 Novemba 2023.

View attachment 2808725
WAlioongezewa mafao Juzi ndio wenye maslahi na KADCO, sitegemei lolote jipya.Washaambiwa wale lakini wasijisahau.
 
Nchi ya ajabu sana hii unaona jinsi kwa miaka yote tangu 1998 kia imekua inamilikiwa na kuendeshwa na wahuni ambapo hawakuwekeza hata senti moja. Ni mambo ya ufisadi kama hayo ndio yanajirudia hadi leo dubai walitaka lupewa bandari zetu zote wamiliki. Haya makubaliano ya DP na serikali kuhusu bandari ya dsm hatuwezi kuamini hadi mkataba uwekwe wazi. Vigogo nchini ni fisadi kiasi cha kutisha.
 
  1. nani aliondoa vitabu katika literature vilivyokuwa vinawafundisha ujasiri wanafunzi? the river between ,things fall apart na vingine vingi watu wa lugha mnajua vzuri.
  2. nani aliruhusu watu wazima wengi (nikiwemo mimi) kuingia chuo kikukuu cha Dar es salaam na equivalent qualification badala ya kuendelea na mzumbe au IFM kwa michepuo yetu halali ya advance diploma. kwa kufanya hivyo alisababisha woga kuongezeka katika chuo kikukuu kwa kuwa kulikuwa na ongezeko kubwa ya watu wanaotumia busara na hekima kuliko akili na kusababisha migomo kuondoka na kupunguza uwezo wa kuwajengea ujasiri vijana
  3. nani alishinikiza au alishawishi ajira za kupendeleana na wizi ukawa sehemu ya ushujaa?
  4. katika yote madereva kwanini mliwaleta waganga mjini?
 
Nchi ngumu hana hii. Tungekuwa na sheria za kueleweka, basi mpaka muda huu kuna kundi kubwa la mchwa lingekuwa kifungoni. 😡
 
Nchi inakosa mapato kwa ujanja ujanja wa vikampuni uchwara hadi tunapata aibu ya kushindwa kusomesha vijana elimu ya chuo kikuu.
Halafu Unaambiwa Kuna Vyombo Makini Pale Hata Sindano Haipiti Bila Ukaguzu
Utagundua Tanzania Tunachezewa Sana Ndugu Zangu
Tumeliwa Mno
Tumelaliwa Mno
Tumechezewa Sana
 
Kama watu wasingehoji watu wasingejua ,chukulia mfano hapo KIA kuna KADCO na TAA wanaoperate ila nyuma ya pazia wte ni serikali moja 😅😅kila mmoja ana management yake hata mishahara wanatofautiana.
Duh...hatari sana
 
Halafu Unaambiwa Kuna Vyombo Makini Pale Hata Sindano Haipiti Bila Ukaguzu
Utagundua Tanzania Tunachezewa Sana Ndugu Zangu
Tumeliwa Mno
Tumelaliwa Mno
Tumechezewa Sana
Inawezekana kabisa..
 
Back
Top Bottom