Yafichuka: Jinsi Tanzania ilivyotia saini mkataba kichaa na kampuni ya siri kuendesha uwanja mkuu wa watalii nchini (KIA)

Tatizo letu sisi lipo wazi, Mlalamishi sio kwamba anakuwa ana uchungu ni kwamba hicho anacholalamikia hana mgao ila akipewa nafasi ya kuwa sehemu ya mgao na yeye anakula na kukaa kimya, na usiombe awe mlamba miguu, atasifia usiamini.
Ukweli wote ndio huu mkuu.
 
Reactions: Tsh
Ndiyo maana umasikini ni Mkubwa kwenye hii Nchi maana Viongozi wamekosa maono pamoja na kuendekeza upigaji.
Hii nchi ina kundi kubwa la watu masikini ila sio nchi masikini. Ndani ya hii nchi kuna watu wana uhakika wa usafiri, matibabu, mavazi, malazi, chakula, uwekezaji, usafiri na mambo yote ambayo masikini hawezi kuwa nayo wala kuyaota. Kuna mtu akikohoa tu ni airport chap hadi paris kwa chekup.
 
Umesema kweli Mkuu

Yaani mtu akishapata nafasi badala ya kuitumikia Nchi basi atataka aanze kujinufaisha yeye kwanza.

Badala yake mnakuta mna mipango ya maendeleo ya miaka 10 kumi ambayo haitekelezeki kutokana na kukosa fedha ambazo unakuta tayari Viongozi walishazichukua zao mapema 🙌
 
WAlioongezewa mafao Juzi ndio wenye maslahi na KADCO, sitegemei lolote jipya.Washaambiwa wale lakini wasijisahau.
 
Nchi ya ajabu sana hii unaona jinsi kwa miaka yote tangu 1998 kia imekua inamilikiwa na kuendeshwa na wahuni ambapo hawakuwekeza hata senti moja. Ni mambo ya ufisadi kama hayo ndio yanajirudia hadi leo dubai walitaka lupewa bandari zetu zote wamiliki. Haya makubaliano ya DP na serikali kuhusu bandari ya dsm hatuwezi kuamini hadi mkataba uwekwe wazi. Vigogo nchini ni fisadi kiasi cha kutisha.
 
  1. nani aliondoa vitabu katika literature vilivyokuwa vinawafundisha ujasiri wanafunzi? the river between ,things fall apart na vingine vingi watu wa lugha mnajua vzuri.
  2. nani aliruhusu watu wazima wengi (nikiwemo mimi) kuingia chuo kikukuu cha Dar es salaam na equivalent qualification badala ya kuendelea na mzumbe au IFM kwa michepuo yetu halali ya advance diploma. kwa kufanya hivyo alisababisha woga kuongezeka katika chuo kikukuu kwa kuwa kulikuwa na ongezeko kubwa ya watu wanaotumia busara na hekima kuliko akili na kusababisha migomo kuondoka na kupunguza uwezo wa kuwajengea ujasiri vijana
  3. nani alishinikiza au alishawishi ajira za kupendeleana na wizi ukawa sehemu ya ushujaa?
  4. katika yote madereva kwanini mliwaleta waganga mjini?
 
Nchi ngumu hana hii. Tungekuwa na sheria za kueleweka, basi mpaka muda huu kuna kundi kubwa la mchwa lingekuwa kifungoni. 😡
 
Nchi inakosa mapato kwa ujanja ujanja wa vikampuni uchwara hadi tunapata aibu ya kushindwa kusomesha vijana elimu ya chuo kikuu.
Halafu Unaambiwa Kuna Vyombo Makini Pale Hata Sindano Haipiti Bila Ukaguzu
Utagundua Tanzania Tunachezewa Sana Ndugu Zangu
Tumeliwa Mno
Tumelaliwa Mno
Tumechezewa Sana
 
Kama watu wasingehoji watu wasingejua ,chukulia mfano hapo KIA kuna KADCO na TAA wanaoperate ila nyuma ya pazia wte ni serikali moja 😅😅kila mmoja ana management yake hata mishahara wanatofautiana.
Duh...hatari sana
 
Halafu Unaambiwa Kuna Vyombo Makini Pale Hata Sindano Haipiti Bila Ukaguzu
Utagundua Tanzania Tunachezewa Sana Ndugu Zangu
Tumeliwa Mno
Tumelaliwa Mno
Tumechezewa Sana
Inawezekana kabisa..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…