Km yapo baadhi ya mambo jamii yetu inapaswa kuyaishi kwa sasa ni kuambizana ukweli pasina kujali muda, hadhi, umri nk..hii ni dawa nzuri kwa sasa, baada ya kujaribu dawa nyingi muda mrefu ikiwemo hiyo unayosema kuangalia mazingira..kweli inatibu mambo mengi sana tuliyo nayo kwenye jamii.Ni sawa lakini sio mahala pake hapo.
Unajua thamani ya nyumba inabebwa na hadhi ya kiwanja kwanza, sasa unaweza kuzungumza point sana ila inategemea umeizungumza wapi na kwenye tukio gani, hapo ndipo utaisoma hekima ya mtu.