Jana usiku nilifuatilia mjadala wa Hoja yenye kichwa cha habari kinachohusu Mtaala Mpya katika Shule za Sekondari ambayo inasisitiza "Elimu Ujuzi". Nia ya mpango huu ni nzuri kabisa na nimponngezee Mhe. Rais na viongozi wote walioliona wazo hili. Wanafunzi wanatakiwa wawe na elimu ya ujuzi ili anapomaliza masomo yake akirudi huku mitaani awe na kitu cha kufanya kama useremala, ushonaji, fundi umeme, fundi magari, kilimo, ufugaji nk. Kwa mawazo yangu kwa sasa mpango huu hautafanikiwa kwa asilimia mia moja kutokana na sababu zifuatazo:-
(1) Hatuna vyuo vilivyoanzishwa kutoa watalaam wa kufundisha masomo hayo.
(2) Hatuna walimu wa kutosheleza kufundisha masomo hayo.
(3) Serikali haijajipanga kupeleka nyenzo za kujifunzia katika shule za sekondari mfano vifaa vya useremala, ushonaji nk. Kwa kifupi mtaala huu unahitaji maandalizi makubwa na inaweza kuchukua nusu nzima ya bajeti ya Serikali. Nia ni nzuri lakini mpango huu hautatekelezeka.