Nimekuuliza swali hujajibu ila unauliza swali lingine..
Inawekwa kwenye kundi la maskini Kwa sababu Tzn imejaa wajinga kama wewe wasio na akili za kukuza Uchumi wao badala yake wanalaumu serikalini.
Tulipopata uhuru tulikuwa na matatizo makuu 4 tuliyokuwa tukipambania kama Nchi,
1. UJINGA 2. MARADHI.
3. UMASKINI 4. RUSHWA. 5. VIONGOZI DHAIFU.
Kama Nchi Kwa kiasi Gani tumeondoa matatizo hayo ktk Nchi Kwa Chama kile kile?
RUSHWA ktk Nchi imepungua au imeongezeka Kwa kiasi gn tangu Awamu ya kwanza hd sasa? Usilinganishe na majirani, ongelea takwimu zetu ndani.
Je UJINGA umeondoka Kwa kiasi Gani ktk Nchi ukilinganisha alipokuwapo Nyerere na sasa, watoto walikuwa wanapata chakula Bure shuleni, mwalimu alikuwa anaheshimika nk.
Darasa la nane enzi zile alikuwa na uwezo kuliko kidato Cha Sita Cha sasa, why tumerudi nyuma Badala ya kusonga mbele?
MARADHI je tumefanikiwa? Pamoja na jitihada zilizofanyika, hatua zetu zinarudi nyuma Badala ya kusonga mbele?
VIONGOZI.
Kwann hakuna maadili ya viongozi? Aliteuliwa tu Leo anaenda tafuta namna ya kuiba? Kwann wanaingia wafanyabiashara bungeni kutafuta fursa za biashara na wanakumbatiwa na chama?
Ni sawa kama Nchi tujivunie bodaboda kufanyika ajira?
Kwann kilimo hakiwekewi nguvu?
Kwann maskini wanaporwa ardhi walorithishwa na mababu Kwa nguvu?
Kwann Nchi yetu, urithi wetu unafanyikaj shamba la bibi?