Yajue maisha ya Mbinguni, yana raha isiyo na kifani

Yajue maisha ya Mbinguni, yana raha isiyo na kifani

Waliotuketea dini sikumoja waamke watuambie ukweli Jamani
Kama una kiu ya kuujua ukweli, isome kwa makini Biblia. Anza na kitabu cha Mathayo sura moja moja kila siku mpaka Ufunuo wa Yohana. Soma huku ukimuomba Mungu akufunulie ukweli. Wakati unasoma, ukikutana na mistari yenye amri au maagizo yatekeleze. Ukikutana na maonyo, yazingatie. Nakuambia ndani ya muda mfupi, utaamini Biblia ni kitabu cha kweli na wala hutahitaji tena walioleta dini waje wakuambie ukweli.
 
Unaweza kuta yeye ndiye yule mchungaji Zumaridi anayeishi Mwanza.

Anasema yeye Mbinguni huwa anakwenda na kurudi, anaongea na Mungu kwa kiswahili na Kisukuma.
da!!!,,,dunia inaenda kasi sana,,,sasa ndo nimeelewa kwa nini fisi wanafungwa plate number!!
 
Mbinguni hakuna njaa wala kiu

Mbinguni tutakula matunda.

Unakula ili iweje wakati hakuna njaa
 
Mbinguni hakuna njaa wala kiu

Mbinguni tutakula matunda.

Unakula ili iweje wakati hakuna njaa
Mbinguni tutakula si kwa sababu ya njaa, bali kwa furaha na uzuri wa uzima wa milele. Kama vile Adamu na Hawa walivyokula matunda katika Bustani ya Edeni kabla ya dhambi kuingia, vivyo hivyo mbinguni tutafurahia matunda ya uzima bila njaa wala kiu. Ni sehemu ya baraka na utimilifu wa maisha ya milele tuliyoahidiwa na Mungu.
 
Kuna nyama?
 
Kuna nyama?
Mbinguni ni mahali pazuri sana, penye utimilifu wa furaha. Mungu atatupatia mahitaji yetu kwa njia bora zaidi kuliko tunavyofikiria. Mambo mazuri unayoyaona duniani yameumbwa na Mungu. Sasa aliyeyaumba hayo unayoona mazuri, atashindwa kutupatia chakula kizuri zaidi kuliko nyama?

Biblia inasema tutakula matunda ya uzima (Ufunuo 22:2), haielezi kuhusu kula nyama mbinguni. Hata hivyo wewe elewa tu kwamba Mungu atatupatia kila kitu kinachotuhakikisha furaha na utoshelevu wa milele.
 
Kuna nyama, hakuna au hujui?
 
kama hamna ugomvi wala chuki ilikuwaje kukawa na vita mbinguni?...kati ya jeshi la mbinguni likiongozwa na malaika michail na shetani na malika wake????...naomba jibu?
Hiyo ilitokea mara moja tu na haitatokea tena. Shetani alifukuzwa mbinguni na hawezi kurudi tena huko anasubiri tu kutupwa katika moto wa milele.
 
Hiyo ilitokea mara moja tu na haitatokea tena. Shetani alifukuzwa mbinguni na hawezi kurudi tena huko anasubiri tu kutupwa katika moto wa milele.
usitoke nje ya mada hapa tunazungumzia vita,na kwa taarifa yako mpaka leo shetani na mawakala wake bado wako kwenye vita vikali kati ya MUNGU na mawakala wake plus malaika,,,,yaani vita iliyopiganwa mbinguni kwa sasa imehamia duniani,mawakala wa MUNGU ni mapadre,mashehe, na wachungaji,mawakala wa shetani ni malaika wachafu,waganga[wapiga ramli],wachawi,vinyamkera n.k,nadhani umeona wiki ilopita fisi kauwawa lakini mzoga wake umekutwa umefungwa plate namba kama gari,,,na kuna mganga wa kienyeji wamemkuta na fisi[polisi]huko simiyu,,alipoulizwa akasema anamtumia kama pikipiki,na pia usiku anamtumia kama helikopta[[unaona vita hiyo],,,so ndo manake unaona tunafundishwa kusali kwa hisia kali sana kwani vita ni vikalimno,,,so USIJE UKASEMA ILIKUWA YA MARA MOJA TU!!!!...vita ya MUNGU na SHETANI haitoisha mpaka siku ya kiama,,,na baada ufufuo,shetani atatupwa kenye ziwa lamoto!!!!!!.............MAPAMBANO BADO YANAENDELEA!!
 
Wewe hio unayoita furaha kwa mwingine ni kero na majonzi.., nilishakuuliza siku moja kama kuna wadau zangu niliokuwa nikiendana nao huku wao wakiwa wanapata shida (mtu kama mimi takuwa vipi na furaha kuwaona hao wanapata shida) ?

Nakama takuwa sina masikitiko sababu nitakuwa nimebadilika (sina feelings za kusikitika) hio ina tofauti gani na hata hapa nikibwia madawa ya kulevya na kuwa teja yaani out of touch of what is happening to my surroundings....

Na maisha ya kuimba na kusifu to infinity kwa mwingine ni kero yaani wengine hata partying tu ikiboa unaanza kuangalia saa (ije kuwa kuimba na kusifu kama kasuku wakati kuna wadau wanapigwa na shida hapo karibu)..., That is not the living for me and I had rather remain dead (which thankfully is known to be)
 
Kama una kiu ya kuujua ukweli, isome kwa makini Biblia. Anza na kitabu cha Mathayo sura moja moja kila siku mpaka Ufunuo wa Yohana. Soma huku ukimuomba Mungu akufunulie ukweli. Wakati unasoma, ukikutana na mistari yenye amri au maagizo yatekeleze. Ukikutana na maonyo, yazingatie. Nakuambia ndani ya muda mfupi, utaamini Biblia ni kitabu cha kweli na wala hutahitaji tena walioleta dini waje wakuambie ukweli.
Shida ukiisoma sana biblia huwez kuiamini Raha uisome juu juu hivohivo kwakweli km mnavoisoma
 
Back
Top Bottom