Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mimi sitaki faida nataka ufafanue majibu uliyotoa juu ya hoja yangu.Hautapa faida nikikueleza walisema nini. Heri nikueleze habari za Yesu kuliko kukueleza habari za wafuasi wa shetani.
Mkuu hapa duniani unasubiria nini!Watu wengi wanahangaika usiku na mchana kutafuta raha na starehe za dunia hii, ambazo ni za muda mfupi, lakini hawajishughulishi kuhakikisha wanayo “tiketi” ya kuingia mbinguni kwenye raha na furaha ya milele. Labda ni kwa sababu hawajui maisha ya mbinguni yatakuwa ya namna gani. Nakutajia hapa mambo mazuri ya mbinguni. Mbinguni...
Yesu kabla ya kupaa mbinguni aliahidi kwamba anaenda kutuandalia makao yenye raha hizo(Yohana 14:2-3). Dalili zinaonesha karibu atarudi kuwachukua wote waliokata “tiketi” ya kuingia kwenye makao hayo mapya ya mbinguni(Mathayo 24:3-33). Kama umeokoka, tiketi hiyo tayari unayo. Kama hujaokoka fanya haya yafuatayo, nawe utakuwa miongoni mwa watakaoingia mbinguni Yesu atakaporudi, au ukiondoka duniani kabla ya ujio wa Yesu:
- Maisha ni matamu mno. Utamu huo unafanya miaka 1000 ionekane kama siku moja tu.(2 Petro 3:8)
- Hakuna kilio wala maombolezo – Ufunuo 21:4
- Hakuna kuzeeka. Tutakuwa na miili mipya ya utukufu – Wafilipi 3:21
- Hakuna njaa wala kiu – Ufunuo 7:16
- Hakuna magonjwa wala ulemavu – Isaya 35:5-6
- Hakuna dhambi wala majaribu –Ufunuo 21:27
- Kuna furaha isiyo na mwisho – Zaburi 16:11
- Tutaishi milele. Hakutakuwa na kifo kabisa – 1 Yohana 2:25; Ufunuo 20:6; Ufunuo 21:4
- Tutaishi na Mungu na kumuona uso kwa uso – Ufunuo 22:4; Ufunuo 21:3
- Tutakuwa kama malaika, hakuna kuoa wala kuolewa – Mathayo 22:30
Kwa sababu hiyo hakuna matatizo ya ndoa!- Hakutakuwa na giza wala usiku – Ufunuo 22:5
- Hatutakula kwa jasho. Tutakula matunda, bure – Ufunuo 2:7
- Hakuna vita wala maadui – Isaya 11:9
- Tutaimba nyimbo tamu kwa lugha moja – Ezra 3:11
- Tutapokea taji za thawabu – 2 Timotheo 4:8
- Tutashiriki karamu(sherehe kubwa) ya arusi ya Mwana-Kondoo(Ufunuo 22:4). Karamu hiyo inapita mara elfu elfu karamu zote zinazofanyika hapa duniani.
Kama uko tayari kuyafanya hayo, fuatisha sala hii ya toba, utaokoka sasa hivi. Omba hivi:
- Kubali kuwa wewe ni mwenye dhambi – Warumi 3:23 – “Kwa maana wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.”
- Amini kwamba Yesu alikufa kwa ajili ya dhambi zako na akafufuka –Warumi 10:9 – “Kwa sababu ukikiri kwa kinywa chako ya kuwa Yesu ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.”
- Tubu dhambi zako kwa moyo wa dhati na usitende dhambi tena – Matendo 3:19 – “Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe.”
- Mpokee Yesu moyoni mwako kwa imani awe Bwana na Mwokozi wa maisha yako – Yohana 1:12 – “Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndiyo wale waliaminio jina lake.”
“Ee Mungu wa mbinguni, nakiri kuwa mimi ni mwenye dhambi, lakini leo natubu kwa moyo wangu wote. Naamini kuwa Yesu Kristo alikufa msalabani kwa ajili ya dhambi zangu, akafufuka ili nipate uzima wa milele. Bwana Yesu, naomba unisafishe kwa damu yako. Ninakukaribisha moyoni mwangu uwe Bwana na Mwokozi wa maisha yangu. Nisaidie kuishi maisha mapya ya utakatifu. Kuanzia leo namkataa shetani na kazi zake zote. Asante Yesu kwa kuniokoa na kunipa “tiketi” ya kuingia mbinguni. Katika Jina la Yesu Kristo, ninaomba na kushukuru. Amina.”
Kama umeomba sala hiyo kwa moyo wako wote, tayari umeokoka na umepata “tiketi” ya kuingia mbinguni.
Ili uendelee vizuri na maisha ya wokovu, hakikisha unasoma Biblia na kuomba kila siku. Lakini pia ungana na waumini wengine katika Kanisa lolote linalohubiri wokovu na kufundisha maisha ya utakatifu, watakuelekeza mambo mengine yakupasayo kufanya. Ubarikiwe sana.
We Kbobori hutaiona mbingu 😀😀Hakuna mbinguni, wazungu walitunga tu ili kumdanganya hasa mwafrika. Amri ya usiibe sio kumuibia Mungu, ila usimuibie mzungu ili uende mbinguni. Dini inashusha kiwango cha kufikiria. Usikubali bila kuhoji? Je ulihoji kama kweli Yesu alifufuka? Wengi wa wayahudi ambao ni asili ya maandiko matakatifu wanamkataa Yesu, inakuwaje mwafrika unampokea? Hoji na wewe! Come out from the cave!!
Wahi, watakukuta mkuuUchoyo wa nini? Waswahili wanasema: kizuri kula na mwenzio.
Nasubiri niwajulishe watu wengi habari hizo njema; watakaokubali tutaenda nao kula hiyo raha ya milele.
Duh hiyo kali sn, vp idara ya maji na yenyewe pia wasisahau kuweka na betting huko, ukishamaliza kupiga story na isaka, yakobo na ibrahimu mnampitia daudi na goliath mnaenda zenu kusuka mikekanaona pia TANESCO wameunganisha umeme,,,,,
Umka utajikojleaMkuu, epuka huo mtazamo wa Atheists. Biblia inatufundisha waziwazi kuwa mbingu ipo; ni makao ya Mungu na ni mahali ambapo waaminio watakwenda kuishi.
Biblia inataja mbingu mara nyingi kuwa ni mahali halisi tofauti na dunia.
Mwanzo 1:1 – “Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.” Mstari huo unaonyesha kuwa mbingu sio sehemu ya dunia, bali ni mahali tofauti.
Yesu pia alisema, "Katika nyumba ya Baba yangu mna makao mengi...nakwenda kuwaandalia mahali... ili nilipo, nanyi muwepo." (Yohana 14:2-3). Hapo Yesu anaelezea mbingu kuwa ni mahali halisi ambako waaminio watakwenda.
Mbingu sio sehemu ya dunia. Kama mbingu ingekuwa hapa hapa duniani, Yesu asingesema kuwa "Nakwenda kuwaandalia mahali."(Yohana 14:2). Maandiko yanaonyesha wazi kuwa Yesu alipaa kwenda mbinguni(Matendo 1:9-11). Na pia Yesu asingesema atarejea tena duniani, kama mbingu ingekuwa hapa hapa.
Biblia inatupa ufunuo wa watu walioiona Mbingu.
Paulo anasema alipelekwa hadi "mbingu ya tatu" (2 Wakorintho 12:2), akionyesha kuwa kuna viwango vya mbingu na kwamba ipo sehemu iliyo tofauti na dunia.
Stefano alipopigwa kwa kutupiwa mawe, aliona "mbingu zimefunguka" na Yesu akiwa mkono wa kuume wa Mungu (Matendo 7:55-56).
Usidanganywe na raha za kitambo za hapa duniani ukafikiri ndiyo mbingu yenyewe. Mbinguni hakuna raha ya kitambo. Ni raha tupu milele yote.
Utasikia kwenye bibliaMmekutana naye wapi wewe!!?
Wahi, watakukuta mkuu
Ulikutana nae wapiNimeambiwa na aliyeumba mbingu.
Umeme utawaka milele bila kukatika mgaonaona pia TANESCO wameunganisha umeme,,,,,
Mbona hilo swali rahisi? Bila miili hii tungewezaje kukuhabarisha raha ya mbinguni? Yesu alituagiza tuwajulishe mataifa yote habari njema, then the end will come. Hapo ndipo tutakapovikwa miili mipyaKama mtapewa miili mipya, sasa hii mnatunza ya nini? kwo Watu wale gambe waue figo na ini?
Hao wataofufuliwa siku ya mwisho, sindio wataamka na miili yao?Mbona hilo swali rahisi? Bila miili hii tungewezaje kukuhabarisha raha ya mbinguni? Yesu alituagiza tuwajulishe mataifa yote habari njema, then the end will come. Hapo ndipo tutakapovikwa miili mipya