Yajue maisha ya Mbinguni, yana raha isiyo na kifani

Yajue maisha ya Mbinguni, yana raha isiyo na kifani

Huyo ni roho mtakatifu anawaka kila mahali 😂😂
da!! ila huyu mwamba aliyepiga picha mbinguni kiboko!!!....alifikaje huko bila kukamatwa na mwamba malaika MICHAEL???,,,,mwanangu jamaa noma,,ananyatia hadi MBINGU na anaipiga picha?????,,,,sasa huyu si hatari sana??,,,kama ameweza kuingia mbinguni na kupiga picha si anaweza kuingia IKULU huku anapiga ULUZI?
 
Hao walishakufa, kwa tuliopo duniani wote tunafuata tuliyoyakuta walioleta hawawezi kuamka maana walishakuwa mavumbi miaka mingi sana.
Tatizo mambo mengi ya historia huathiriwa

Dini zinazid kuathiriwa Kwa kasi sana had sisi tumefikia kudanganyana waziwazi had kizazii kingine mambo yattaazid kuharibika
 
Watu wengi wanahangaika usiku na mchana kutafuta raha na starehe za dunia hii, ambazo ni za muda mfupi, lakini hawajishughulishi kuhakikisha wanayo “tiketi” ya kuingia mbinguni kwenye raha na furaha ya milele. Labda ni kwa sababu hawajui maisha ya mbinguni yatakuwa ya namna gani. Nakutajia hapa mambo mazuri ya mbinguni. Mbinguni...
  • Maisha ni matamu mno. Utamu huo unafanya miaka 1000 ionekane kama siku moja tu.(2 Petro 3:8)
  • Hakuna kilio wala maombolezo – Ufunuo 21:4
  • Hakuna kuzeeka. Tutakuwa na miili mipya ya utukufu – Wafilipi 3:21
  • Hakuna njaa wala kiu – Ufunuo 7:16
  • Hakuna magonjwa wala ulemavu – Isaya 35:5-6
  • Hakuna dhambi wala majaribu –Ufunuo 21:27
  • Kuna furaha isiyo na mwisho – Zaburi 16:11
  • Tutaishi milele. Hakutakuwa na kifo kabisa – 1 Yohana 2:25; Ufunuo 20:6; Ufunuo 21:4
  • Tutaishi na Mungu na kumuona uso kwa uso – Ufunuo 22:4; Ufunuo 21:3
  • Tutakuwa kama malaika, hakuna kuoa wala kuolewa – Mathayo 22:30
    Kwa sababu hiyo hakuna matatizo ya ndoa!
  • Hakutakuwa na giza wala usiku – Ufunuo 22:5
  • Hatutakula kwa jasho. Tutakula matunda, bure – Ufunuo 2:7
  • Hakuna vita wala maadui – Isaya 11:9
  • Tutaimba nyimbo tamu kwa lugha moja – Ezra 3:11
  • Tutapokea taji za thawabu – 2 Timotheo 4:8
  • Tutashiriki karamu(sherehe kubwa) ya arusi ya Mwana-Kondoo(Ufunuo 22:4). Karamu hiyo inapita mara elfu elfu karamu zote zinazofanyika hapa duniani.
Yesu kabla ya kupaa mbinguni aliahidi kwamba anaenda kutuandalia makao yenye raha hizo(Yohana 14:2-3). Dalili zinaonesha karibu atarudi kuwachukua wote waliokata “tiketi” ya kuingia kwenye makao hayo mapya ya mbinguni(Mathayo 24:3-33). Kama umeokoka, tiketi hiyo tayari unayo. Kama hujaokoka fanya haya yafuatayo, nawe utakuwa miongoni mwa watakaoingia mbinguni Yesu atakaporudi, au ukiondoka duniani kabla ya ujio wa Yesu:
  • Kubali kuwa wewe ni mwenye dhambi – Warumi 3:23 – “Kwa maana wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.”
  • Amini kwamba Yesu alikufa kwa ajili ya dhambi zako na akafufuka –Warumi 10:9 – “Kwa sababu ukikiri kwa kinywa chako ya kuwa Yesu ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.”
  • Tubu dhambi zako kwa moyo wa dhati na usitende dhambi tena – Matendo 3:19 – “Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe.”
  • Mpokee Yesu moyoni mwako kwa imani awe Bwana na Mwokozi wa maisha yako – Yohana 1:12 – “Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndiyo wale waliaminio jina lake.”
Kama uko tayari kuyafanya hayo, fuatisha sala hii ya toba, utaokoka sasa hivi. Omba hivi:
Ee Mungu wa mbinguni, nakiri kuwa mimi ni mwenye dhambi, lakini leo natubu kwa moyo wangu wote. Naamini kuwa Yesu Kristo alikufa msalabani kwa ajili ya dhambi zangu, akafufuka ili nipate uzima wa milele. Bwana Yesu, naomba unisafishe kwa damu yako. Ninakukaribisha moyoni mwangu uwe Bwana na Mwokozi wa maisha yangu. Nisaidie kuishi maisha mapya ya utakatifu. Kuanzia leo namkataa shetani na kazi zake zote. Asante Yesu kwa kuniokoa na kunipa “tiketi” ya kuingia mbinguni. Katika Jina la Yesu Kristo, ninaomba na kushukuru. Amina.”

Kama umeomba sala hiyo kwa moyo wako wote, tayari umeokoka na umepata “tiketi” ya kuingia mbinguni.

Ili uendelee vizuri na maisha ya wokovu, hakikisha unasoma Biblia na kuomba kila siku. Lakini pia ungana na waumini wengine katika Kanisa lolote linalohubiri wokovu na kufundisha maisha ya utakatifu, watakuelekeza mambo mengine yakupasayo kufanya. Ubarikiwe sana.
Mkuu Setfree naomba dadavua hapa panapo nitatiza Mimi binafsi
  • Hakuna njaa wala kiu – Ufunuo 7:16
  • Hatutakula kwa jasho. Tutakula matunda, bure – Ufunuo 2:7
Asiyekuwa na njaa hahitaji kula eventually hatoenda chooni mana hajala chochote.

Kama mbinguni hakutakuwa na njaa kwanini tule matunda? Kwanini tushiriki karamu kubwa pamoja na Yesu kristo?
 
Hakuna mbinguni au motoni, ni mchongo tu. Kama kweli mbingu ipo ni kwa nini mtu usikubali kufa ili uende huko? Ndugu zangu, hakuna maisha mazuri zaidi ya haya, jaribu tu kuboresha maisha yako kabla ya kuyeyuka.
 
Waliotuketea dini sikumoja waamke watuambie ukweli Jamani
Hasa hawa,wanayumba sana.

Yohana 9:2
Wanafunzi wake wakamuuliza, “Mwalimu, ni nani aliyetenda dhambi; ni huyu mtu au wazazi wake hata azaliwe kipofu?”
 
Mbingu ipo hapahapa duniani
Mkuu, epuka huo mtazamo wa Atheists. Biblia inatufundisha waziwazi kuwa mbingu ipo; ni makao ya Mungu na ni mahali ambapo waaminio watakwenda kuishi.

Biblia inataja mbingu mara nyingi kuwa ni mahali halisi tofauti na dunia.

Mwanzo 1:1 – “Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.” Mstari huo unaonyesha kuwa mbingu sio sehemu ya dunia, bali ni mahali tofauti.

Yesu pia alisema, "Katika nyumba ya Baba yangu mna makao mengi...nakwenda kuwaandalia mahali... ili nilipo, nanyi muwepo." (Yohana 14:2-3). Hapo Yesu anaelezea mbingu kuwa ni mahali halisi ambako waaminio watakwenda.

Mbingu sio sehemu ya dunia. Kama mbingu ingekuwa hapa hapa duniani, Yesu asingesema kuwa "Nakwenda kuwaandalia mahali."(Yohana 14:2). Maandiko yanaonyesha wazi kuwa Yesu alipaa kwenda mbinguni(Matendo 1:9-11). Na pia Yesu asingesema atarejea tena duniani, kama mbingu ingekuwa hapa hapa.

Biblia inatupa ufunuo wa watu walioiona Mbingu.
Paulo anasema alipelekwa hadi "mbingu ya tatu" (2 Wakorintho 12:2), akionyesha kuwa kuna viwango vya mbingu na kwamba ipo sehemu iliyo tofauti na dunia.
Stefano alipopigwa kwa kutupiwa mawe, aliona "mbingu zimefunguka" na Yesu akiwa mkono wa kuume wa Mungu (Matendo 7:55-56).

Usidanganywe na raha za kitambo za hapa duniani ukafikiri ndiyo mbingu yenyewe. Mbinguni hakuna raha ya kitambo. Ni raha tupu milele yote.
 
Raha ikwapi hapo wakati hakutakuwa na wali maharage
Kama unafurahia wali maharage, basi mbinguni kuna zaidi ya wali maharage kwakuwa aliyeumba wali na maharage Mbinguni ndiyo makao yake. Anatuandalia vyakula vitamu zaidi.
 
Tatizo wanaosimulia mbinguni pazuri, wanaogopa kufa😆😆😆 hampendi kwenda kula raha!?
Mtu wa rohoni haogopi kufa. Kufa ni faida na kuishi ni Kristo. Kumbuka habari za Stefano. Alishtakiwa kwa uongo. Wakati anajitetea mbele ya wazee wa baraza, walimsagia meno kwa hasira. Hakuogopa vitisho vyao kuwa watamuua, badala yake alifurahi na kuwaambia anaona mbingu zimefunuliwa(Matendo 7:55-56).
 
Mkuu, epuka huo mtazamo wa Atheists. Biblia inatufundisha waziwazi kuwa mbingu ipo; ni makao ya Mungu na ni mahali ambapo waaminio watakwenda kuishi.

Biblia inataja mbingu mara nyingi kuwa ni mahali halisi tofauti na dunia.

Mwanzo 1:1 – “Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi.” Mstari huo unaonyesha kuwa mbingu sio sehemu ya dunia, bali ni mahali tofauti.

Yesu pia alisema, "Katika nyumba ya Baba yangu mna makao mengi...nakwenda kuwaandalia mahali... ili nilipo, nanyi muwepo." (Yohana 14:2-3). Hapo Yesu anaelezea mbingu kuwa ni mahali halisi ambako waaminio watakwenda.

Mbingu sio sehemu ya dunia. Kama mbingu ingekuwa hapa hapa duniani, Yesu asingesema kuwa "Nakwenda kuwaandalia mahali."(Yohana 14:2). Maandiko yanaonyesha wazi kuwa Yesu alipaa kwenda mbinguni(Matendo 1:9-11). Na pia Yesu asingesema atarejea tena duniani, kama mbingu ingekuwa hapa hapa.

Biblia inatupa ufunuo wa watu walioiona Mbingu.
Paulo anasema alipelekwa hadi "mbingu ya tatu" (2 Wakorintho 12:2), akionyesha kuwa kuna viwango vya mbingu na kwamba ipo sehemu iliyo tofauti na dunia.
Stefano alipopigwa kwa kutupiwa mawe, aliona "mbingu zimefunguka" na Yesu akiwa mkono wa kuume wa Mungu (Matendo 7:55-56).

Usidanganywe na raha za kitambo za hapa duniani ukafikiri ndiyo mbingu yenyewe. Mbinguni hakuna raha ya kitambo. Ni raha tupu milele yote.
Nani kakuambia huo mtazamo ni wa Atheists? Je wana hati miliki ya hayo maneno?
 
Back
Top Bottom