Yajue mambo mazito yatakayotokea wakati Yesu atakapokuja

Yajue mambo mazito yatakayotokea wakati Yesu atakapokuja

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
6,238
Reaction score
8,194
Heshima zenu wakuu.
Leo nawaletea mpangilio(timeline) au mtiririko wa mambo mazito sana yatakayotokea Yesu atakapokuja. Maandalizi yanayofanyika nchini Israeli, ya kujenga hekalu la tatu, ni ushahidi wa wazi kuwa Yesu amekaribia kuja.

Nakusihi usome kwa makini uzi huu usije ukasema hukujua au hukuambiwa, mambo haya yatakapoanza kutokea:

1. Kunyakuliwa kwa Kanisa
Tukio hili litafanyika wakati Yesu atakapokuja mawinguni kulichukua Kanisa, yaani wote wanaomwamini (1 Thes 4:16-17). Waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza na kuungana na watakatifu walio hai duniani – kisha Yesu atawanyakua na kuwapeleka mbinguni na kukaa nao kwa miaka 7.

2. Kiti cha Hukumu cha Kristo na Arusi ya Mwanakondoo
Baada ya kunyakuliwa, waaminio watasimama mbele ya Kristo kupokea thawabu ya kazi waliyoitenda duniani. (2 Korns 5:10) – Kazi ya kila mtu itapimwa (1 Kor 3:12-15). Baada ya hapo Watakatifu watasherehekea pamoja na Kristo arusi ya Mwanakondoo. Hii ndiyo arusi(wedding banquet) niliyoizungumzia katika Mwaliko niliowapa members wote wa JF!

3. Miaka 7 ya Dhiki Kuu
Wakati Wateule wakisherehekea Arusi ya Mwanakondoo mbinguni, watakaobaki duniani watapata dhiki kuu ambayo haijawahi kutokea tangu kuumbwa kwa ulimwengu. Wanaomlalamikia sasa Mungu eti kama ana upendo kwanini anaruhusu vita, njaa na mateso, kipindi hiki cha dhiki kuu ndio watatoa maneno ya kufuru kabisa kutokana na mateso mazito watakayopata chini ya utawala wa Mpinga Kristo(Mt 24:21; Dan 9:27; Ufu 13:16-17 Mpinga Kristo atamlazimisha kila mtu apokee chapa ya mnyama(666). Atakayekataa kuipokea hataweza kuuza wala kununua chochote.

4. Yesu Atarudi Tena Duniani na Kutawala Miaka 1000
Baada ya miaka hiyo 7 ya Dhiki Kuu, Yesu atakuja duniani kwa utukufu mwingi na kila jicho litamuona (Ufu 19:11-16; Zek 14:4; Mt 24:30). Yesu atamshinda Mpinga Kristo na Nabii wa uongo na kuwatupa katika ziwa la moto na shetani atafungwa kwa miaka 1000 (Ufu 19:19-20; Ufu 20:1-3) ndipo Yesu Kristo atakapoanza kutawala kwa miaka 1000. Miaka hii itakuwa ya haki na amani kabisa duniani (Ufu 20:4-6). Kipindi hiki hata wanyama wa mwituni hawatakuwa na madhara(Isa 11:6-9). Mwishoni mwa kipindi hiki shetani ataachiliwa kwa muda mfupi, atawadanganya watu lakini Mungu atamshinda na kumtupa katika ziwa la moto milele(Ufu 20:7-10).

5. Kiti Kikubwa Cheupe cha Hukumu
Waliokufa katika dhambi watafufuliwa na kuhukumiwa kwenda katika ziwa liwakalo moto.
(Ufu 20:11-15)

6. Mbingu Mpya na Nchi Mpya
Mungu ataumba mbingu mpya na nchi mpya. Watakatifu wataishi milele pamoja na Bwana(Ufu 21:1-4; 2 Pet 3:13)

7. Ni nini kitakachotokea kwa Waisraeli?
  • Wakati wa Dhiki Kuu (Juma la 70 la Danieli) Waisraeli watateseka sana.
  • Mpinga Kristo atafanya na Waisraeli mkataba wa uongo wa kuleta amani mwanzoni mwa miaka saba ya dhiki kuu(Dan 9:27). Katikati ya miaka hiyo (yaani baada ya miaka 3 na nusu), Mpinga Kristo atawasaliti Waisraeli, ataingia hekaluni na kudai yeye ndiye Mungu. Hapa unaweza ukaelewa sasa kwanini Waisraeli wanaandaa hekalu la tatu. Mpinga Kristo ndiye chukizo la uharibifu linalotajwa katika Mt 24:15-16 litakalosimama patakatifu.
  • Waisraeli watatubu na kuokolewa mwishoni mwa miaka 7 ya Dhiki Kuu na kumtambua Yesu kuwa ndiye Masihi wao (Zek 12:10; Rum 11:26). Hii itatokea kabla Yesu hajaja mara ya pili kutawala dunia kwa miaka 1000.
 
This timeline follows a pre-millennial and pre-tribulation view of eschatology.
Inawezekana mpangilio huu ukatofautiana kidogo na jinsi ulivyojifunza wewe. Kama ni hivyo, andika hapa jinsi unavyojua wewe tujadili pamoja. Asante.
 
Mpangilio ni 1.

Tangazo la amani na usalama,yani hizi vuguvugu za vita unazoziona hakuna vita itakayotokea Kwa Hawa wafalme wa kaskazini na kusini yani Marekani na Urudi

2. Wakitangaza kuungana watapiga mareufuku ibada,na wanaofanya ibada ya kweli tu ndiowatakaoendelea licha ya katazo Hilo,yani Kisha wataingia kipindi Cha dhiki juu

3. Harmagedon, vita ya serikali za wanadamu zilizoungana kupigana na serikali ya Mungu ili kuwashambulia wale waabudu wa kweli, serikali za wanadamu zitaangamizwa ndipo ule utawala wa miaka elfu1000 wa Yesu Kristo akiwa mbinguni pamoja na wale anakondoo 144000 ambao Yesu alisema anaenda kuwaandalia makazi,alipo na wao watakuwepo, hiyo miaka elfu1000 Dunia itageuzwa kuwa paradiso, ufufuo utafanyika n.k,

4. Baada ya miaka1000 kuisha wwanadamu wote ambao wapo katika Dunia paradiso watafikia ukamilifu wa Adamu kama alivyokuwa kabla ya kutenda dhambi, Kisha shetani ataenda kuwajaribu mara ya amwisho,watakaomuunga mkono shetani watakufa milele yani hawatakuwepo tena, na watakaomuunga mkono Yesu watapata nafasi ya kuishi milele, Kisha Yesu ataurudusha ufalme Kwa baba yake
 
Baada ya hapo Watakatifu watasherehekea pamoja na Kristo arusi ya Mwanakondoo. Hii ndiyo arusi(wedding banquet) niliyoizungumzia katika Mwaliko niliowapa members wote wa JF!
Arusi hii ni Arusi ya Mwanakondoo, Bwana wetu Yesu Kristo. Ameiandaa kwa ajili ya Bibi arusi wake—Kanisa lake takatifu!

Ufunuo 19:7
"Tufurahi na kushangilia; tumtukuze, kwani wakati wa arusi ya Mwanakondoo umefika, na bibi arusi yuko tayari."

Bibi-arusi ni wale wote waliotubu dhambi zao na kumwamini Yesu Kristo. Ni wale wanaoendelea kujiweka tayari kwa ujio wake kwa kuishi maisha matakatifu (Ebr 12:14).

Sherehe ya arusi itafanyika mbinguni baada ya Yesu kuja kulinyakua kanisa.

Siku na saa hatuijui, lakini dalili zinaonyesha Yesu yuaja upesi(Ufu 22:12)

Kiingilio ni WOKOVU tu.
Kama hujaokoka, sali(omba) sala hii ya toba, utapata tiketi ya kuingia mbinguni kusherehekea Arusi hiyo:

Omba(fuatisha) sala hii kwa moyo wako wa dhati:
“Mungu Baba, natambua mimi ni mwenye dhambi. Sina tiketi ya kuingia mbinguni. Leo nakuja mbele zako nikiomba msamaha wako. Natubu dhambi zangu zote na kuziacha. Nakiri kuwa Yesu Kristo ni Bwana, na Yeye ndiye Mwokozi wa ulimwengu. Yesu karibu moyoni mwangu utawale maisha yangu kuanzia leo. Naomba unipe nguvu ya kushinda dhambi na kuishi maisha matakatifu hadi siku utakayokuja kutunyakua na kutupeleka mbinguni. Namkataa shetani na kazi zake zote. Asante Yesu kwa kuniokoa. Katika Jina la Yesu Kristo, naomba na kushukuru. Amen.”

Kama umeomba sala hiyo kwa moyo wako wa dhati, tayari umeokoka. Umepata tiketi ya kuingia mbinguni kwenye sherehe ya Arusi ya Mwanakondoo. Anza kusoma Biblia kila siku na kumuomba Mungu akusaidie kuendelea vizuri kiroho. Tafuta pia Kanisa lolote linalohubiri wokovu na kufundisha utakatifu ujiunge nalo; ujifunze mambo mengine yakupasayo kufanya wakati huu tunapoendelea kumgojea Bwana Arusi Yesu Kristo. Ubarikiwe sana!
 
Arusi hii ni Arusi ya Mwanakondoo, Bwana wetu Yesu Kristo. Ameiandaa kwa ajili ya Bibi arusi wake—Kanisa lake takatifu!

Ufunuo 19:7
"Tufurahi na kushangilia; tumtukuze, kwani wakati wa arusi ya Mwanakondoo umefika, na bibi arusi yuko tayari."

Bibi-arusi ni wale wote waliotubu dhambi zao na kumwamini Yesu Kristo. Ni wale wanaoendelea kujiweka tayari kwa ujio wake kwa kuishi maisha matakatifu (Ebr 12:14).

Sherehe ya arusi itafanyika mbinguni baada ya Yesu kuja kulinyakua kanisa.

Siku na saa hatuijui, lakini dalili zinaonyesha Yesu yuaja upesi(Ufu 22:12)

Kiingilio ni WOKOVU tu.
Kama hujaokoka, sali(omba) sala hii ya toba, utapata tiketi ya kuingia mbinguni kusherehekea Arusi hiyo:

Omba(fuatisha) sala hii kwa moyo wako wa dhati:
“Mungu Baba, natambua mimi ni mwenye dhambi. Sina tiketi ya kuingia mbinguni. Leo nakuja mbele zako nikiomba msamaha wako. Natubu dhambi zangu zote na kuziacha. Nakiri kuwa Yesu Kristo ni Bwana, na Yeye ndiye Mwokozi wa ulimwengu. Yesu karibu moyoni mwangu utawale maisha yangu kuanzia leo. Naomba unipe nguvu ya kushinda dhambi na kuishi maisha matakatifu hadi siku utakayokuja kutunyakua na kutupeleka mbinguni. Namkataa shetani na kazi zake zote. Asante Yesu kwa kuniokoa. Katika Jina la Yesu Kristo, naomba na kushukuru. Amen.”

Kama umeomba sala hiyo kwa moyo wako wa dhati, tayari umeokoka. Umepata tiketi ya kuingia mbinguni kwenye sherehe ya Arusi ya Mwanakondoo. Anza kusoma Biblia kila siku na kumuomba Mungu akusaidie kuendelea vizuri kiroho. Tafuta pia Kanisa lolote linalohubiri wokovu na kufundisha utakatifu ujiunge nalo; ujifunze mambo mengine yakupasayo kufanya wakati huu tunapoendelea kumgojea Bwana Arusi Yesu Kristo. Ubarikiwe sana!
Kwa nini kondoo of all the animals, kwa nini si mbuzi au ng'ombe au mbwa au paka au twiga au chui.
 
KWA UPANDE WA UISLAM MAMBO YATAKAYOTOKEA KABLA YA KURUDI KWA MASIHI MWANA WA MARIAM.

1- Kufunguliwa/kuachwa huru kwa Al -Masihi Dajjal ( Anti-christ/ Fake Messiah/ Masihi wa uongo)

Mtume Muhammad (s.a.w) alielezea kuwa hakuna mtume au nabii ambaye hajauonya umati au watu wake juu ya ujio wa huyu kiumbe-(Anti-christ).

Toka kuumbwa kwa wanaadamu hakujawahi kutokea mtihani mzito zaidi ya ujio wa Masihi dajjal (The Anti-christ).

2- Kabla ya kuja kwake dunia itakumbwa na balaa kubwa la njaa. Miaka mitatu kabla ya kutokea mbingu na ardhi zitazuia nusu ya maji yake , mwaka unaofuata mbigu na ardhi zitazuia theluthi mbili za maji yake na mwaka unaotuata hakutakuwa na mvua kabisa hapa duniani. Watu watakumbwa na balaa kubwa la njaa, mifugo itakufa kwa kukosa maji n.k
Ndipo huyu kiumbe atatokea uelekeo wa mashariki akitokea katika nchi ya IRAN maeneo ya jiji la Isfahan akiongozana na kundi kubwa la mayahudi wapatao 70,000 watakaovaa vitambaa vya rangi ya blue na nyeupe.

3- Masihi dajjal ataitembea dunia nzima kwa muda wa siku 40...Siku moja itakuwa na urefu wa mwaka mzima na siku zinazofuata zitakuwa mithili ya mwezi. Ataingia kila mji hapa duniani isipokuwa Mji wa Makkah na Madinah kwani ni miji ambayo Mungu ameiwekea ulinzi mkali wa Malaika. Hivyo Masihi Dajjal hataweza kuiingia miji hii.

Mwanzo atajinadi kuwa yeye ndiye Masihi, Wayahudi watamkubali na kuwa chini yake. Atakumbana na upinzani mkali kutoka kwa waislam kwasababu walishaelezwa vizuri juu ya sifa zake. Mpinga kristo ni kiumbe mwenye jicho moja...kwa maana jicho lingine ni chongo (limetuna mithili ya zabibu) juu ya paji lake la uso ana maandishi KFR (kwa maana ya KAFIRI).

Atapewa uwezo wa kufanya miujiza mingi kama vile kuwaletea watu waliopigwa na ukame mkali ,mvua na kuotesha mazao yao na kunenepesha mifugo yao na kupata mavuno hapo kwa hapo. Kisha atajitangaza kuwa ni MUNGU. Watu wengi watamkubali kuwa ni Mungu. Atakuwa na pepo na moto wake. Wale watakaokubali wataingia katika pepo yake na wale watakaomkataa atawarusha katika mto wake wa moto. Mtume Muhammad (s.a.w) anasema akikupa uchague kati ya moto na pepo yake , wewe jitose katika moto maana ni kinyume chake.

Wafuasi wake wengi watakuwa ni wanawake. Mtume alieleza kuwa iwapo utamsikia anakuja uelekeo wa mji wako basi chukua watu wako na mifugo yako ukimbilie juu ya milima ili upate kusalimika na fitina zake.

Ataeneza uasi na uovu ulimwengu mzima.

NDIPO MASIHI MWANA WA MARIAM ATAKAPOREJEA TENA DUNIANI KUJA KUPAMBANA NAE
 
Unapoandika miaka jaribu kuzingatia miaka 1000 kwa mwanadamu ni sawa na siku 1 kwa Mungu.
Mungu miaka anaihesabu tofauti na anavyohesabu binadamu, sasa kwa nini mnajifanya werevu mnahesabu miaka kivyenu mnaacha kuhesabu kama anavyohesabu Mungu? Je masaa, siku na wiki navyo anahesabu tofauti nanyi binadamu?
 
Kwa nini kondoo of all the animals, kwa nini si mbuzi au ng'ombe au mbwa au paka au twiga au chui.
The lamb (kondoo) symbolizes innocence, purity, and sacrifice, aligning with the qualities of saints and Jesus Christ. In biblical tradition, lambs were used for sacrifices, foreshadowing Jesus as the ultimate sacrifice for humanity’s sins (John 1:29). Unlike goats, which often symbolize stubbornness (Matthew 25:32-33), or other animals like cows and cats, which lack strong biblical symbolism for holiness, the lamb represents obedience, meekness, and redemption.
Umeelewa mkuu?
 
KATIKA IMANI YA UISLAM

YESU (YESHUA/ISA/JESUS) mwana wa Mariam atarudi tena duniani. Na Mtume Muhammad (s.a.w) alieleza kuwa ujio wa masihi mwana wa mariam utakuwa ni moja ya dalili kubwa za kukaribia kwa Saa ya Qiyama (Mwisho wa dunia).

YESU atashuka katika jiji la DAMASCUS nchini Syria akiambatana na malaika wawili. Atashuka Alfajiri katika mnara mkubwa mweupe wa msikiti mkuu jijini Damascus. Atakutana na kundi dogo la waumini watakaokuwa wamejiwekea ngome wakijiandaa kwenda kupambana na majeshi ya Masihi Dajjal (Anti-christ). YESU atashuka na waumini watamtambua kuwa ndiye mwana wa mariam, watamuomba awaswalishe ila atakataa na kumwambia kiongozi wa Waislam kipindi hicho atakajulikana kama Al-Mahdi aongoze ibada ya Alfajiri. Kisha Yesu atawaambia wafungue malango ya eneo hilo aende kumsaka Masihi Dajjal.

Taarifa za ujio wa Masihi Yesu mwana wa mariam zitamfikia Masihi Dajjal ambaye atakuwa amekimbilia Palestina. Yesu atakutana uso kwa uso na Dajjal katika mji unaoitwa LUDD ( upo katika ardhi ya Israel ya leo). Dajjal atapukutika kama mwamba wa chumvi mara baada ya kumuona Yesu, Nuru ya yesu itamyeyusha na Yesu atamuua Dajjal kwa kutumia mkuki.

Hapo ndipo itakuwa mwisho wa Dajjal.

Yesu atamaliza mzozo wa dini ipi ni ya kweli kati ya Uislam,Ukristo na Uyahudi. Atavunja misalaba na kuua nguruwe.

Baada ya kuondoka kwa Masihi Dajjal wataachiliwa viumbe wengine waliofungiwa katika safu za milima kwa miaka mingi, viumbe hao wanajulikana kama Yajuj wa maajuj (Gog and Magog). Yesu ataamrishwa apande na waumini juu ya mlima Turr kwasababu hakuna mwanadamu atakayeweza kupambana na majeshi ya yajuj wa majuj. Atapanda mlimani ambapo watakaa kwa muda mrefu mpaka pale Mungu atakapowaua hao yajuj wa majuj kwa kuwapelekea wadudu mithili ya minyoo itakayotoboa shingo zao. Watakufa wote na mizoga yao kuzagaa kila pande. Mungu atashusha mvua kubwa kwa muda wa siku 40 na kusafisha ardhi yote ndipo Yesu atateremka milimani na kuja chini ambapo ataishi kwa muda wa miaka 40 ataishi kama kiongozi wa waislam,mfuasi wa Mtume Muhammad, ataoa na atakufa na kuzikwa jijini Madinah karibu na kaburi la mtume Muhammad (s a.w). Kipindi cha Yesu atakapoishi hapa duniani kitakuwa na neema kubwa, ardhi itayoa mazao mengi ,wanyama watanenepa na kutoa maziwa mengi, wanyama wa mwituni watachanganyika na wanyama walao nyasi bila ya kudhuriana kwa chochote. Kitakuwa ni kipindi bora katika maisha ya ustawi wa wanadamu kupata kutokea hapa duniani.

Mwisho kabisa Baada ya kufa kwa masihi wanaaadamu watarudi tena katika njia zao za kale watafabya ufisadi na uovu mwingi na ndipo mwisho wa dunia utakapokuja na hii ni baada ya Mungu kuwafisha waumini wote , dunia itabaki na watu waovu tu.

HIVI NI KWA UCHACHE WA MATUKIO YA UJIO WA MASIHI WA UONGO NA MASIHI WA KWELI
 
Unapoandika miaka jaribu kuzingatia miaka 1000 kwa mwanadamu ni sawa na siku 1 kwa Mungu.
Nafikiri comment yako inatokana na 2 Petro 3:8

"Lakini, wapenzi, msisahau jambo hili moja, ya kuwa kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja."

Hii haimaanishi kwamba miaka 1,000 ya utawala wa Yesu duniani itakuwa siku moja halisi. Hapana. Petro alitumia mfano huo kueleza kwa nini Yesu hajarudi haraka. Kwa Mungu, maelfu ya miaka ya wanadamu ni kama siku moja tu machoni pake kwa sababu Yeye ni wa milele.

Maandiko yako wazi kwamba Ufalme wa Yesu utakuwa wa miaka 1,000 halisi:

Ufunuo 20:4 – “Nao wakatawala pamoja na Kristo miaka elfu moja.”
 
Haleluya! Yesu atakapokuja miili yetu itabadilishwa. Tutavikwa miili isiyozeeka wala kufa!
1 Kor 15:52-53
"...kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika. Maana sharti huu uharibikao uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa.
 

Ufunuo 19:9​

"Heri walioalikwa katika karamu ya arusi ya Mwana-kondoo. Akaniambia, Maneno haya ni maneno ya kweli ya Mungu."
 
Back
Top Bottom